Thursday, May 22, 2014

SOMA HISTORIA NZIMA YA MAISHA YA MREMBO WEMA SEPETU AKA MAMAAA PLATNUMZZZZZZZ

Credit:http://www.williammalecela.com
Taja wasichana wote wa Bongo Movies wanaotamba Tanzania, usipoliweka jina la Wema Sepetu orodha haijakamilika. Wema Sepetu ni supastaa asiyefutika kwenye vichwa vya habari vya magazeti ya udaku na websites/blogs. Mfahamu zaidi kwa undani leo anaposherehekea siku yake ya kuzaliwa katika mahojiano haya aliyoyafanya na Bongo5 kwaajili ya jarida la Mzuka.Kwenu mko wangapi na wewe ndio mtoto wa mwisho?
Kwetu sisi tuko wanne na mimi ndio mtoto wa mwisho, nina dada watatu. Wa kwanza na wa tatu wako Marekani, wa pili yupo hapa hapa, ameolewa ana familia yake. Wa kwanza yuko kule anafanya kazi ana mtoto mmoja. Wa tatu yuko kule anasoma na anafanya kazi 
Miaka mitano kabla ya mwaka 2006, Wema alikuwa ni msichana wa aina gani?
Wema alikuwa ni msichana wa kawaida. Wakati ule ulikuwa ukiniuliza unataka kuwa nani ukikua ningekujibu nataka kuwa air hostess sababu dreams zangu zilikuwa ni kuwa air hostess, sijawahi kufikiria kabisa kuingia kwenye fame. Though nilikuwa nawaangalia watu kama Ray C, K-Lynn, Kwasababu mimi nilikuwa nasoma academic na shuleni kwetu nakumbuka tulikuwa tukitoka ile home time kulikuwa na duka fulani hivi la mpemba tunaenda tunakula sambusa nini, so magari yatapita nini and we would see Ray C and everybody will go like ‘you see Ray C’ you know, kwahiyo we go crazy over superstars na watu famous. 

Kiukweli I never so myself kuwa katika this position ambayo niko. Kwahiyo nilikuwa tu msichana ambaye sina ndoto za kuwa star lakini nilikuwa tu nawashangaa masupastaa. My dad amekuwa anapenda sana mashindano ya Miss Tanzania and kila mwaka alikuwa anamake sure kwamba amenunua tiketi ya kwenda kuangalia Miss Tanzania. 


So nakumbuka ilikuwa ni mwaka wa akina Sylvia Bahame tumekaa nyumbani amekosa tiketi. Akakaa akasema ‘kumbe ukiwa umekaa nyumbani ndio unaenjoy vizuri kuliko hata kwenda pale’ akasema ‘one day nawish one of my beauties hata kama hatoshinda, nikilipia tiketi naenda nikijua kabisa nimeenda kumlipia binti yangu. 

 
So sikukiweka kichwani hicho kitu lakini after kuingia katika whatever na nini, so siku nimekaa na dad nikamwambia ‘dad unakumbuka kuna siku ulisema hivi’ akasema ‘yes I remember’ . Hata Mange Kimambi alivyokuja kuniapproach, alivyoniona Sleep Way akaniambia kwamba anataka niingie katika mashindano, nikamwambia kwamba mimi nina wazazi wangu, siwezi nikaamua tu mimi mwenyewe na mimi nakaa na wazazi, so nilivyoongea na mama akasema ‘ongea na baba yako’ nikampigia simu baba alikuwa kipindi hicho Dodoma, akaniambia ‘fanya my beauty nitakusupport’, hakuthink twice alinipa go ahead kabisa.
Kabla ya Miss Tanzania, ni watu wachache sana waliokuwa wakimfahamu Wema Sepetu, ni vipi Miss Tanzania ilibadilisha maisha yako hasa kutokana na watu kuanza kufuatilia maisha yako na chochote unachofanya?
Ni kitu ambacho nilikipata bado nina umri mdogo and nilikuwa sijajiandaa, nilikuwa naichukulia tu poa this whole issue ya kuwa kwenye spotlight. Nilikuwa sidhani kama itakuwa vile kwasababu kama wanavyosema experience ni bora uexperience mwenyewe usione kwa wenzako so nilivyokuwa naichukulia ni tofauti na ilivyokuja kuwa kwasababu mimi nilikuwa naichukulia tu ‘kuwa star raha’ umeenda watu wamekushangaa nini lakini nilivyokuwa nimeingia sana katika ile spotlight nikasema kumbe ooh my God it’s this hard.
Kwahiyo ikawa ni kitu kilichonipa wakati mgumu sana kukizoea like mpaka sasa hivi naweza kusema kwamba ile umetoka kila mtu kakuangalia nini, it’s not an easy task, yaani haizoeleki hiyo hali yaani kila siku unazidi kuiona mpya kwasababu there is no place unaweza ukaenda ukawa na privacy yako, yaani upende usipende lazima utakuwa ni attention kwa watu, lazima watu watakuangalia. Sometimes natamani tu na mimi niwe Wema lakini huwezi sababu all eyes on you. And a lot of times as a normal human being kuna time unahisi you just be yourself lakini inakuwa ni time chache chache sana. The only place where I can be myself is in my room and in my house, out of my gate you cannot be yourself.
Kuna wakati wowote uliwahi kujuta maisha ya ustaa baada ya kuwa Miss Tanzania?
Yes, nimewahi kujuta lakini mwisho wa siku huwaga nasema kwamba mwenyezi Mungu ndio anapanga kwasababu kama mwenyezi Mungu ndio amenipangia hivi nisingefika hapa kwanza, kwahiyo regrets zinatokea kwa kila mtu, lakini siwezi kusema kwamba zimetoka kwa mara nyingi, labda mara moja mara mbili na zinatokea pale tatizo linapotokea, hauwezi ukapata regrets kama hakuna tatizo.
Ukiwa staa kila mtu atataka awe rafiki yako, na kabla ya kuwa Miss Tanzania ni wazi ulikuwa na marafiki uliokuwa ukihang out nao hapa na pale, uliendelea kuwa na urafiki nao, ama baada ya kuingia maisha hayo ikakuwia vigumu kuwa nao tena pamoja?
Nina marafiki mpaka sasa ninahangout nao wanakuja mpaka nyumbani lakini hatushei sana zile common interests kama zamani because once upon a time tulikuwa tuko wote on the same rank. So nilivyokuwa nipo kwenye spotlight obvious nimekutana na watu wengine wapya watu ambao naonana nao katika kazi zangu za kila siku, because apart from being Miss Tanzania, I am also an actress, kwahiyo nakutana na wasanii wengine ambao labda nakaa nao kwa muda mrefu sana kwahiyo utajikuta tu unashare nao common interests sababu unafanya nao kazi pamoja. 
Ulikuwa na boyfriend tayari? 
Yes nilikuwa naye
Kuna wakati wowote aliwahi kujihisi inferior kutokana wewe kuwa maarufu? Ulifanyaje kumweka sawa?
Well, si unajua zile za kishuleshule, zile za kitoto naweza kusema. Sana sana ukishafika ile o-level nini utakuwa na yule boyfriend ambaye unaamka tu asubuhi umeshavaa unasema sasa hivi naenda kuonana na boyfriend wangu, ukisharudi kutoka shuleni from there nyumbani, no boyfriend. Yeah nilikuwa naye, in the beginning alivyojua kwamba nashiriki Miss Dar Indian Ocean akaniambia kwamba ‘ukishiriki mimi nisahau, sitaweza kuwa na wewe tena’, nikamwambia, why? Akaniambia ‘utakuwa upo kwenye public’ nikamwambia ‘okay fine’, nikamdanganya kwamba sishiriki. 
So siku moja gazeti la Mwananchi pale katikati kulikuwa na picha yangu kubwa ‘Miss Dar Indian Ocean kushindana kesho’ and lile gazeti kuanzia naingia shuleni naingia kila mtu ananiambia ameniona kwenye gazeti. So kitu cha kwanza nikafikiria ‘Mungu wangu yule mtu akiliona’ so sikuonana naye the whole day.
Nikiwa nyumbani ndio nikamuona anakuja kalishikilia, nikawa namsikiliza. Akaniambia, ‘nimeona gazeti lako and ndio hivyo kwahiyo umeshanidhihirishia kwamba umechagua hiyo issue, so fine we endelea’. Basi nikajaribisha kuongea naye lakini hakuweza kunisikiliza lakini luckily the next day wakati ndio nashiriki nimekaa pale time ya kujibu swali namuona pale anapiga picha kwahiyo he was there na alinisupport mpaka nilipofika Miss Tanzania lakini after that sababu nilikuwa ambassador wa Vodacom nikawa nafanya kazi Vodacom nikawa sionani naye vile kama kawaida, kila akinipigia simu nipo busy, yeye mwenyewe akasema tu ‘bwana mimi siwezi’. Basi tulielewana vizuri na mpaka kesho tunaongea, tunasalimiana’

 
Uwewahi kusema bila Kanumba usingeingia kwenye movies, marehemu alikuwa ana mchango gani kwako?
 
Nakumbuka nilipokutana na marehemu nilikuwa niko na dada yangu mimi nilikuwa nakaa na dada yangu, kwasababu once nilishawahi kuishi na mama yangu and then from there unajua baada ya kuingia kwenye nini nini nikawa busy. Dada yangu mimi kaolewa lakini kwa dada yangu nilikawa nahisi kama pako free zaidi, kwamba mama ukirudi ‘umetoka wapi sijui nini na nini hivyo, alikuwa haelewi. So ikabidi tu nianze kuishi na dada yangu.
 
Kwahiyo dada yangu akawa ananielewa, kwasababu hayupo sana protective kama mama. Siku hiyo tunabadilisha seating arrangement ya pale nyumbani kwa dada yangu tukawa tunatafuta carpet like different furnitures, so tukawa tumeenda hapa kulikuwa na hili duka kubwa hivi la Mwanamboka kulikuwa kuna furniture center, Pentagon, so tukawa tumeenda pale wakati tunaenda tulimkuta Kanumba wapo nje wameweka makamera yao nini ,wanashoot Lost Twins. So sisi tumeingia tunaona tu makamera, tumepark gari tumeingia ndani tunaangalia furniture. Akatokea Maya tukasalimiana akaniambia, ‘ jamani nakupenda’ na mimi nikamwambia na mimi napenda unavyoigiza’ nini na nini. 
Tukatoka nje tukakutana tena na Maya akaniambia ‘jamani jamani kama unaweza pita kidogo tu hata uonekane, hata usalimie’.
 
Nikamwambia siwezi kwasababu nipo kwenye mkataba, akina Uncle Hashimu wataniua wakiniona nimefanya kazi au nimetokea kwenye nini bila kuwaconsult so akaniambia ‘basi sawa tuachie namba yako’. Wakati ananiambia tuachie nambo yako, Kanumba huyo anapita, ‘Kaka kaka ngoja umemuona Wema?’ Aliniringia sana.
 
‘Mambo’ nikamwambia ‘fresh vipi’ ‘safi’ nikamwambia poa,’Kaka basi chukua namba yake ya simu tunaweza baadaye like tunaweza tukamtumia kwenye movies’, ,Kanumba akamwambia achukue simu yake ndani. Basi nikamwangalia mimi mwenyewe basi ndio ninamwona mara ya kwanza, ‘Hee Kanumba’, kwasababu nimeangalia sana michezo yao. 
Basi, so baada ya hapo akaleta akachukua namba yangu akanibeep nikamsave, basi mimi nikaondoka zangu. Sijafika mbali naona namba inanipigia ambayo nimeisave vilevile Steven Kanumba, nikapokea ‘Hello’ akaniambia ‘vipi, safi Kanumba hapa’ nikamwambia ‘namba yako nimeisave’ ‘haya basi sawa basi baadae’ nikamwambia ‘poa’.
 
Mara like jioni jioni hivi akaanza kunitext ‘mambo’ ‘Safi’ ‘vipi uko wapi?. Basi kila siku tukawa tumejengeana tabia ya kutextiana kila siku tunandelea for one weak tunatext mara yeye ataniuliza umekula nini, mara sijui nini, obvious kwa mwanamke unakua tu unajua kwamba mwanaume akiwa ana interest na wewe. Kidogo tukaanza kuulizana una boyfriend una girlfriend sijui nini, hivyo. Akaniambia mimi ‘nipo kambini Lamada’ akanielekeza nikafika.
 
Basi nimefika siku hiyo tumekaa pale garden akaniambia ananipenda na nini, hivyo. Kipindi hicho nilikuwa sina boyfriend nilikuwa very very single, so nikamdanganya nikamwambia ‘mimi na boyfriend wangu sijui nini’ akaniambia ‘naomba tu just like nifikirie basi’ Nakumbuka tulivyokuwa tunaondoka ndo tukakiss, it was our first kiss. Basi nikaondoka, akaniambia ‘unaweza kurudi tena nikamwambia siwezi akaniambia please, please naomba urudi tena unikiss’ nikamwambia ‘sawa’ basi nikarudi then akaniambia ‘l love you, love you too, mapenzi yakaanza.
 
Basi kwenye mapenzi yetu ndo akaniambia like ‘nataka kuact movies na wewe’ nikamwambia ‘mimi siwezi kuact’ akaniambia ‘mimi nahisi unaweza kuact hujajua tu’ nikamwabia sijawai kufikiria kuact, akaniambia ‘unaweza kulia’, nikamwambia ‘nilie nina sababu gani ya kulia’ akaniambia ‘basi kama huwezi kulia tutakumenyea vitunguu, ‘vitunguu ukimenya si unalia, basi tutakuwa tuna kumenyea vitunguu’ .
 
Akaniambia niende kuonana na bosi wake. Nilivyofika tu ofisini nikaonana na Mtitu Game. Akanipa script akaniambia nikasome kama story akaniambia ‘wakati unasoma uwe unasoma sana concentrate kwenye Dina. Basi vile tukiwa tukikutana tunafanya mazoezi nini, akaniambia ‘sawa basi wewe you are ready to shoot. Nilivyo shoot movie yangu kwanza, hauwezi amini, I just felt yaani kwanza niliona iko very easy. Kwa wengine wanaona it’s hard unajua.
 
Baada ya hapo ndo nilikuwa tayari nimetoa taji, I had to go back to school. Nikasafiri nikaelekea Malaysia kufanya kozi yangu ya mwaka ya International Business, wakati niko Malaysia nikatumiwa movie yangu ya Point of No Return. Tumekaa tunaangalia na marafiki zangu nikaona kwamba kumbe it’s nice, it’s fun. Nikampigia simu, ‘narudi for likizo soon naomba uniandalie script nataka ni shoot movie nyingine’
 
Nimerudi kweli ndo tukashoot Red Valentine, Family Tears, White Maria yaani tukashoot movie movie nyingi hivi so from there nikawa nimeshajikuta katika movie, so that why I keep saying kwamba without him nisingejua.

Hebu tuzungumzie uhusiano wako na Diamond ambao katika mahusiano yako yote ndio ulioandikwa zaidi kwenye magazeti, unakumbuka mlikutana wapi?
 
Mi na Diamond tuliwahi kukutana mara moja tu Billcanaz na hatukuwahi kusalimiana kabla ya kuanza uhusiano lakini tulikuwa tunaangalia sana, so nakumbuka alikuwa yupo smoking room kwahiyo tukawa tumepeana migongo, nilikuwa na rafiki zangu wawili. Nikamuona akaniona yeye alikuwa na rafiki yake, hatujasaliamija hatujafanya chochote mimi nimechukua vinywaji tukatoka nje na marafiki zangu tumesimama hapo nje nikawa naambiwa ‘yule ndio ameimba Kamwambie’ kipindi hicho nilikuwa namuona wa ajabu sana ila tu alijiseksisha kiasi fulani (kicheko kirefu).
Kipindi hicho mimi nilikuwa natoka na Chaz Baba so nakumbuka hiyo ndio ilikuwa the first and last day tumeonana. Mimi nikasafiri nikaenda Marekani, nilipofika kipindi hicho Kamwambie ndio ilikuwa hot na Mbagala ndio karelease. Dada zangu walikuwa wanampenda sana Diamond yaani just from the songs. Dada yangu wa kwanza ana miaka 14 yupo Marekani na hajawahi kurudi Bongo toka aondoke kwahiyo alikuwa anaona Bongo inafanya vizuri sasa hivi akaniuliza kama tuna urafiki na Diamond nikasema sio sana tunajuana tu. 
Akaniambia nimwambia aende Marekani kufanya show sababu kila party tuliyokuwa tunaenda lazima watapiga Kamwambie halafu kila mtu anaipenda. So watu wakaanza kuniambia like ‘hebu find contact naye huku kuna mapromoter aje kufanya show’na kipindi hicho Profesa ndio alikuwa amekuja nikamwambia basi sawa mi nitamtafuta.
 
Nikamwabia Da Rehema, Ray C anitafutie contact zake. So siku moja nikaona anaplan kwenda kufanya show London, nika mclick Diamond Platnumz nikamtext, nikamwambia ‘hey mambo vp mzima upo London’ akaniambia ‘No mamie sipo London sijui ni nini’ nikamwabia ‘anyways Wema hapa nipo Marekani halafu it happens una fans wengi, akaniambia basi sawa acha nimalize issue ya London halafu nitakuambia. 
 
Basi tukajenga tu mazoea tukawa tunachat nini yaani ikawa yeye anaingia Facebook kuchat na mimi naingia kuchat naye, washkaji tu yaani. Akawa ananiambia ‘bado uko na Chaz na nini’ nikamwambia yeah nipo na Chaz. Sasa ilikuwa ni kama mwezi wa nane wa tisa kama sikosei. Mimi wakati nipo Marekani nilikuwa naambiwa sana news kuhusu Chaz, mara Chaz sijui yupo na mwanamke gani, hiyo hiyo Facebook watu wananitumia mpaka picha nikumuuliza anakataa.
 
Sasa mimi nakumbuka dada yangu alikuwa anampenda sana Chaz so siku ya siku amekutana naye yupo sijui na mwanamke gani alipoaniambia nikasema, basi. So nikajikuta namuelezea matatizo Diamond. Siku niliyoamua kabisa mimi and Chaz are done nikamwambia mimi siwezi. So tukawa tunawasiliana na Naseeb hivyo. Siku moja tukanuniana, alikuwa amealikwa Ikulu halafu nikawa namtext hajibu, nikimpigia simu hapokei akaja akatoka akanipigia simu nikawa sijibu. Akanitumia meseji ‘baby I am sorry, we ndio faraja yangu sijui ni nini…. I LOVE YOU. Sikuona kitu kingine chochote nikaona tu hiyo. Basi nami nikamjibu sawa nimekusamehe lakini sijakusamehe sana, nimekusame kidogo. Akaniambia ‘niambie kitu kizuri’ na mimi nikamwambia I LOVE YOU. Basi akaniambia ‘mwenzio nakupenda, nachanganyikiwa’ basi no mapenzi yakaanza hapo.So niliporudi kutoka Marekani mimi na Naseeb tukaanza kuishi pamoja.


 
Mwaka jana alipooenda kutumbuiza kwenye Big Brother Africa, alidai kuwa ameweza kuongea Kiingereza kwasababu yako, ulikuwa ukimfundisha ama ulikuwa ukipenda kumuongelesha Kiingereza zaidi?
 
Yes. Naseeb alikuwa hajui Kiingereza, alikuwa anajua cha juu juu. Ila mimi na Naseeb tumekaa pamoja mwaka mzima kama mke na mume. So mimi nilivyo kidogo nimetupia Kiingereza kwahiyo hiyo ilikuwa inampa tabu kwenye the first two months kwahiyo most of the times nikawa naongea naye Kiingereza. Lakini he is smart, Naseeb is very smart yaani akiwa haelewi kitu ‘hivi baby hapa kwenye has na have unafanya nini, hapa natumia tense gani? Niweke ing niweke nini?’ mwisho wa siku nikajikuta like tunatumia most of the time kufundishana. Akisema kitu ambacho sicho namwambia ‘usije ukarudia tena kusema hivyo mbele za watu watakucheka’. So akajikuta tu anaweza.
 
Kwanini mliachana?
Mimi na Naseeb tuliachana baada ya yeye kunicheat na Jokate .Nilikuwa sijui and maisha yangu yote tangia nimeanza mapenzi na Naseeb naweza kusema kuwa sikuwahi kuwa unfaithful. I used to be very faithful to him na tulikuwa tunapendana sana. With Naseeb nilikuwa nimesharidhika na maisha ambayo niko nayo na hata kama yalikuwa not good, whatever lakini tayari nilikuwa nipo satisfied with me and him nilikuwa tayari nimesharidhika naye. 
 
Nadhani pia inacost mwanaume akishajua kwamba anakutawala in one way or another so labda ni shetani au ni ibilisi alimuingilia baada ya kutaka kuanza kushoot video ya Mawazo ndo rumors zilianza, nikawa siamini kwanza. Siku moja ndio nikapigiwa simu na rafiki yangu anafanya kazi Piccolo akaniambia ‘Diamond yuko hapa na Jokate na wanakiss’. Nilitoka, nikachukua taxi nikaenda mpaka Piccolo, kitu cha kwanza niliona gari yake. Nilivyofika nikawakuta sijui wamewekeana miguu. Nilivyofika pale nikawasalimia wakawa wako kimya na nimeona ile kitu nikawaaga nikaondoka zangu. Nikaliaaaa, amerudi wakati huo bado tunaishi pamoja akanikutana napanga nguo, hakutaka kuongea sikutaka kuongea, tukachuniana, sikulala mimi na Naseeb kitandani for one week. Anaiona ile hali lakini hataki kuanza. Nikachoka, nikaja tu siku nimepanga nguo zangu nikaenda kwa dada yangu ndio ikawa kimoja. Basi mimi nikamwacha CREDIT : BONGO5

Monday, May 19, 2014

SAJENT ATINGA NA KIVAZI CHA KLABU KWENYE KITCHEN PARTY

MWIGIZAJI Bongo Movies, Husna Idd ‘Sajent’ amewashangaza waalikwa baada ya kutinga na kivazi cha klabu kwenye kitchen party katika Ukumbi wa Mawela, Sinza jijini Dar. 
Mwigizaji Bongo Movies, Husna Idd ‘Sajent’ (kushoto) akiwa na Shilole.
Sajent alipoingia ukumbini aliwafanya watu wote kumgeukia huku baadhi wakihoji namna ambavyo wazazi wa biharusi watamtathmini.
Hata hivyo, mwenyewe hakujali kwani aliingia ameongozana na msanii mwenzake, Salma Jabu ‘Nisha’ ambaye walishikana kama mtu na matroni wake.

PROF JAY (Joseph Haule): SOMA HISTORIA YAKE YA MAISHA NA MUZIKI NA ALIPOFIKIA.


Joseph Haule (amezaliwa tar. 29 Desemba1975) ni msanii wa muziki wa hip hop kutoka nchini Tanzania. Anafahamika zaidi kwa jina lake la kisanii kama Professor Jay. Katika Tanzania, Prof. Jay anatazamika kama msanii aliyeweza kuwateka wazee waweze kusikiliza muziki wa Bongo Flava. Hasa kwa kibao alichofanya wakati yupo na kundi la Hard Blasters Crew – Chemsha Bongo. Professor Jay anatokea kundi la Hard Blasters Crew. Kundi hili ni moja ya makundi yaliyofanya muziki huu ambao hujulikana kama ‘muziki wa kizazi kipya’ kukubaliwa na sehemu kubwa ya wa Tanzania.
Maisha ya muziki
Professor Jay alianza shughuli za muziki mnamo miaka ya 90 hivi na alijiunga na kundi la ‘Hard Blasters Crew‘(HBC) mnamo mwaka 1994. Mwaka 1995 Jay na HBC walishinda kuwa kundi bora la Hip Hop nchini Tanzania. Jay na HBC walitoa albamu ya kwanza iitwayo ‘Funaga Kazi’ mwaka 2000 Albamu hiyo inaaminika kwamba ilileta mapinduzi makubwa sana ya muziki wa Hip Hop nchini Tanzania. Albamu hii yenye ujumbe mzito ina nyimbo kama ‘Chemsha Bongo’ na ‘Mamsapu’ ambazo zilichangia kufanya muziki wa ‘Bongo Flava‘ kuwa wa kila rika na kupewa heshima. Kabla ya hapo muziki huu ulionekana kuwa ni muziki wa wahuni

Msanii Binafsi.

Professor Jay aliamua kuwa msanii binafsi mnamo 2001 na muda mfupi baada ya hapo akatoa albamu yake ya kwanza iitwayo “Machozi Jasho na Damu”. Albamu hii ilivuma haraka sana na kumfanya Prof. Jay kupata tuzo ya kuwa mtunzi bora wa Hip Hop nchini Tanzania kwa nyimbo yake ya ‘Ndio Mzee’ kutoka kwenye albamu hiyo. na ikifuatiwa na Nyimbo ya “Piga Makofi na Bongo Dar es Salaam“
Mwaka 2003 Alitoa albamu ya pili iitwayo “Mapinduzi Halisi” ambayo nayo ilishinda tuzo ya Kili Music Awards kuwa albamu bora ya Muziki wa Hip Hop nchini Tanzania kwa mwaka 2003. Albamu hii imebebanNyimbo kama “Zali la Mentali”, “Msinitenge,” na “Promota Anabeep”
Mwaka 2006 Januari alitoa albamu ya tatu iliyoitwa “J.O.S.EP.P.H”. Jina la albamu hii lilitokana na nyimbo iliyotoka Mwanzo kabla ya Albamu kutoka. Nyimbo hii ilichaguliwa kuwa nyimbo bora ya Bongo Flava kwenye BBC na Radio One Awards.
Mpya imewahi kuteuliwa kuwa ni albamu bora ya Hip Hop , Mtunzi bora wa nyimbo za Hip Hop, na Nyimbo bora ya Hip Hop ya mwaka kwenye Kili Music Awards. 2006.”Nikusaidieje”. na Baadae Kisima Music Awards ya Kenya ilikuwa Nyimbo bora ya Hip Hop na Video bora ya Hip Hop kutoka nchini Tanzania.

Albamu

Aluta Continua ( 2007 )
J.O.S.E.P.H. ( 2006 )
Mapinduzi Halisi ( 2003 )

MachoziJasho na Damu ( 2001 )

Imeandaliwa na DJCHOKA MUSIC
CREDIT:http://victormachota.blogspot.com/

Sunday, May 11, 2014

MANCHESTER CITY WAMEJITANGAZIA UBINGWA. HAKUNA WA KUWASHUSHA MABIGWA HAWA WA MANCHESTER.

20140511-183236.jpg


By Israel Saria on May 11, 2014


Hatimaye Manchester City wamefanikiwa kunyakua ubingwa wa England katika siku ya mwisho ya Ligi Kuu, ambapo walikuwa wakihitaji pointi moja tu kutawazwa wafalme.

Vijana hao wa Manuel Pellegrini hawakufanya makosa walipoingia uwanjani nyumbani dhidi ya West Ham, kwani Samin Nasri na nahodha Vincent Kompany walihakikisha wanaipatia timu yao mabao, huku ngome ikihakikisha haivuji.

Wakati City wakipata ushindi huo, Liverpool waliokuwa wakiunyemelea ubingwa pia kwa kusubiri kuteleza kwa City, walianza vibaya baada ya Martin Skirttel kujifunga bao walipocheza dhidi ya Newcastle United na kuwafisha moyo washabiki dimbani Anfield.

Hata hivyo, Liverpool walizinduka baadaye, wakasawazisha kisha kufunga bao la ushindi lakini kwa kuzingatia matokeo ya City, Liver walishindwa kutimiza ndoto ya kutwaa ubingwa huo ambao waliupoteza tangu 1990.

City walikuwa wakipewa nafasi nzuri zaidi ya kutwaa ubingwa huo, hasa baada ya Liverpool kuteleza hivi karibuni kwa kukubali kichapo kutoka kwa Chelsea, kabla ya mechi iliyopita kwenda sare ya 3-3 na Crystal Palace katika mchezo ambao vijana wa Brendan Rodgers walikuwa wanaongoza kwa mabao matatu kwa bila.

Nafasi ya tatu imekwenda kwa Chelsea ambao walianza vibaya mechi yao ya mwisho dhidi ya Cardiff kwa kutangulia kufungwa, lakini walisawazisha na kuongeza bao la ushindi katika kulindwa heshima yao. Nafasi ya nne imeshikwa na Arsenal waliowalaza Norwich 2-0.

Timu hizo nne ndizo zimeingia kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya (UCL) wakati Everton waliowafunga Hull mabao 2-0 na Tottenham Hotspur waliowakandika Aston Villa 3-0 wamefuzu kucheza Ligi ya Europa.

Manchester United wamemaliza msimu kwa sare ya 1-1 na Southampton.


Swansea waliwakung’uta Sunderland 3-1, West Bromwich Albion wakalala 2-1 kwa Stoke na Fulham wakatoka 2-2 na Crystal Palace.Norwich wameungana na Cardiff na Fulham kushuka daraja.

Friday, May 09, 2014

MISS IFM USIKU WA LEO: Maneno ya Prezzo kuhusu Miss Ifm leo.


Credit:Millardayo.com
07dimondLeo ni siku rasmi anayotafutwa Miss Ifm ambaye ndiye atakua mwakilishi kuelekea ngazi ya juu zaidi ikiwemo ya Miss Tanzania,Kutoka 254 Cmb Prezzo ndiye msanii pekee aliyepata mwaliko wa kutumbuiza kwenye show hii ambayo mbali na wanachuo wa Ifm inategemea pia kuwakutanisha watu mbalimbali.
06dimond
Millardayo.com imepata nafasi ya kuongea na Prezzo kuhusu show hii ambayo amesema>>’Usiku wa leo utakua balaa koz sisi tumeiandaa,nikisema sisi namaanisha team Prezoo ikiwa pamoja na madancer wangu yaani full kamiligado meen’
Prezzo kwa mwaka huu itakua ni show ya tatu kufanya Tanzania na itakua ya kwanza kwa Dar es salaam tangu 2014 ianze,amefanya show tatu kwa Tanzania ya kwanza ilikua Mwanza yapili ilikua Arusha na ya tatu ndo hii hapa 88.5 Dar es salaam.

KAJALA SASA KWISHA KAZI....WEMA SEPETU APATA USHAHIDI .....ATAFUTE MLANGO WA KUTOKEA.

Credit:Blogu ya wananchi
Wema Sepetu.
Unaweza ukaficha siri na ukaamini hakuna atakayejua bila kukumbuka kuwa hakuna siri ya watu wawili! Hatimaye Wema Isaac Sepetu amenasa ushahidi wa aliyekuwa rafikiye kipenzi, Kajala Masanja wa kumwibia aliyekuwa bwana’ke, Clement au CK, yule kigogo wa ikulu. 
MIL. 13 KISINGIZIO TU
Habari za mjini kwa wiki nzima ni kusambaa kwa ujumbe mfupi (SMS) za kimapenzi za Kajala na CK ambazo sasa zimefunua kisa kamili cha mastaa hao kuhitilafiana huku Sh. Milioni 13 zikiwa kisingizio tu. 
WEMA ALIKUWA ANATAFUTA USHAHIDI?
Kwa mujibu wa chanzo makini kilicho karibu na mastaa hao, kupatikana kwa meseji hizo ni kama mpango wa Mungu, kwani sasa kitendawili kimeteguka. 

Baadhi ya meseji zilizonaswa.
“Wema alikuwa anatafuta ushahidi kama kweli Kajala anatembea na CK hivyo sasa amepata ushahidi. 
“Mwenye macho haambiwi tazama na kama hujui kusoma hata picha huoni? Ama kweli kikulacho ki nguoni mwako!” Kilisema chanzo hicho. 

Habari za ndani zilieleza kuwa meseji hizo zilikutwa kwenye simu ya CK na mwanamke mwingine ambaye naye anadaiwa kutoka na kigogo huyo, aliyetajwa kwa jina moja la Naima aliyekwenda kumbwagia ‘zigo’ Wema kwa ajili ya ushahidi.

Kajala Masanja.
Ilisemekana kwamba Naima alimuomba simu CK kwa kuwa ya kwake ilikuwa mbovu.

Habari zilizidi kudai kuwa baada ya CK kumpa mpenzi wake huyo simu yake, kumbe zile meseji alizokuwa akichati na Kajala alikuwa amesahau kuzifuta ndipo zilipobambwa. 

Mpashaji wetu aliweka wazi kwamba meseji zile zilimshangaza Naima kwa kuwa yeye alikuwa ni mmoja wa watu ambao walikuwa hawaamini kabisa kama kulikuwa na ukweli wowote kuhusu tuhuma za Kajala kutembea na CK. 

NAIMA ACHANGANYIKIWA
“Yaani Naima alipoziona meseji alichanganyikiwa kabisa, alikuwa kama kachomwa sindano ya ganzi kwani alikuwa ni mmoja wa watu ambao  hawaamini kabisa kama kweli Kajala anatembea na CK. 

“Naima alipokaa vizuri ndipo akaanzisha timbwili lenye ujazo mkubwa na CK,” kilisema chanzo hicho.

Mnyetishaji wetu aliendelea kutiririka kuwa katika SMS hizo ambazo zilionesha waziwazi namba ya Kajala, zilikuwa zikielezea namna CK alivyokuwa akimuomba msamaha Kajala kwa kutopokea simu yake.

Kajala na Wema wakati wa ushosti wao.
HUU HAPA MZIGO
Mtiririko na meseji hizo ulikuwa hivi;
CK: “Mama mimi sipendi kukatiwa simu  pze, ok sawa lakini mi nakupenda.
Kajala: Kwa hiyo ndiyo unaniambiaje?
CK: Umeamua kuniblock?
CK: Kwa nini hupokei simu zangu?
CK: Unaponikatia simu wakati mimi naongea sijapenda sijui nijielezeje mama haya sawa.
Kajala: Fanya mambo. 

MZIGO MIKONONI MWA ‘MNYAMWEZI’ WEMA
Ilisemekana kwamba baada ya Naima kuona meseji hizo alizihifadhi ili akamfikishie Wema ‘Myamwezi’ na kumuonesha jinsi rafiki yake alivyokuwa siyo mwaminfu kwake kitu ambacho alikifanikisha.

Habari zilidai kuwa baada ya Wema kuona SMS hizo alipatwa na mshtuko mkubwa kwani alikuwa haamini kama ni jambo analoweza kulifanya rafiki yake Kajala.

Ujumbe mwingine ulionaswa.
  Baada ya ishu hiyo kuwa ndiyo habari ya mjini, gazeti hili lilijiongeza ambapo lilimsaka Wema ili kuzungumzia kuhusu meseji hizo. 
Alipopatikana, Wema alifunguka kuwa  amesikitishwa mno na kitendo cha Kajala.  
Wema alisema bora angefanya mtu mwingine yeyote lakini siyo Kajala aliyejitolea kuyaokoa maisha yake.
“Ukweli kabisa angefanya mtu mwingine yeyote wala isingekuwa ishu lakini siyo K. Aisee K amenishangaza na kuniumiza mno.
“Nilikuwa nimeshapanga niweke naye mambo sawa maisha yaendelee kama zamani lakini kwa hili siwezi kumsamehe tena,” alisema Wema aliyeonekana kukerwa na kucharuka vibaya.  
HUYU HAPA MAMA WEMA
Baada ya kumalizana na Wema, gazeti hili lilimtafuta mama Wema, Mariam Sepetu ili kuzungumzia jambo hilo ambapo alisema kuwa siku zote alimwambia mwanaye kuwa achague marafiki wa kuwa nao lakini hakulitilia maanani.  
“Unajua nilikuwa namwambia Wema kila siku, achague marafiki ambao atakuwa nao. Wengine siyo marafiki wa kweli, ndiyo kama hivyo ilivyotokea, nawaachia wenyewe mimi sina la kusema,” alisema mama Wema.  
KAJALA VIPI?
Hata hivyo, gazeti lilimtafuta Kajala kwa njia mbalimbali lakini lilitonywa kuwa yupo China kwa ‘biashara zake’. Katika mahojiano maalum na gazeti pacha la hili, Ijumaa Wikienda hivi karibuni, Kajala alikana kuwa hata na namba ya CK.
“Katika maisha yangu CK niliwahi kuonana naye mara moja tu, sina hata namba yake ya simu,” alinukuliwa Kajala.  
TEAM WEMA YASHANGILIA USHINDI
Kwa upande wake lile kundi linalojiita Team Wema katika mitandao ya kijamii ilijipongeza kwa kupata ushahidi huo ambao sasa umeleta sura mpya ya ugomvi wa wawili hao.
 
Sehemu ya maoni mengi mitandaoni ilisomeka: “Sasa kule kulia kote runingani na mwanaye matokeo yake ndiyo haya? Kama kweli Kajala kamfanyia Wema hivyo, basi anapaswa kuomba msamaha hata kama Wema yupo na mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’

Thursday, May 08, 2014

MAN CITY WAICHAPA ASTON VILLA 4-0 WAKARIBIA UBINGWA

Credit:ndgshilatu.blogspot.com
Man of the hour: Edin Dzeko roars to the Etihad stands after his first goal gives City the lead 
Mtu wa heshima: Edin Dzeko akiunguruma baada ya kufunga bao lake la kwanza leo Etihad dhidi ya Aston Villa.
KWA asilimia kubwa mnuso wa ubingwa wanukia Etihad baada ya Manchester City kuibuka na ushindi mtamu wa mabao 4-0 dhidi ya Aston Villa katika mchezo wa ligi kuu soka nchini England.
Ushindi huu umewarejesha Man City kileleni na sasa wanahitaji pointi moja tu kutwaa taji msimu huu.
Dakika 45 za kipindi cha kwanza zilimalizika kwa milango ya timu zote kuwa migumu.
Baada ya kuingia katika vyumba vya kuvalia nguo, Manuel Pellegrini aliwakumbusha vijana wake kuwa wamebakiwa na kazi ndogo kuchukua taji.
Man City waliporudi kipindi cha pili walikuja na kasi nzuri na katika dakika ya 64 na 72, Edin Dzeko alifunga mabao mawili.

Wakati Aston Villa wakitafuta njia ya kusawazisha, katika dakika ya 89, Stefan Jovetic aliifungia bao la tatu Man City.
Dakika ya 93, mwafrika mwenye kiwango cha juu zaidi, Yaya Toure alihitimisha karamu ya mabao na kuwafanya City wakaribie kuutwaa ubingwa wa pili ndani ya misimu mitatu.

City wameishusha Liverpool kileleni kwa kufikisha pointi 83, huku Liverpool wakibakia nafasi ya pili kwa poini 81. Timu zote zimecheza mechi 37. 
Sare ya mabao 3-3 waliyopata Liverpool jumatatu ya wiki hii dhidi ya Crystal Palace imewafanya wawe katika wakati mgumu wa kufuta ukame wa miaka 24 bila kombe, na sasa wanawaombea dua mbaya Man City wafungwe mechi ya mwisho siku ya jumapili dhidi ya West Ham kwenye uwanja wa Etihad.
And now you've gotta believe us: Dzeko is joined by his City team-mates to celebrate his second goal 
Dzeko akiungana na wachezaji wa Man City kushangilia bao lake la pili.
Kikosi cha Man City leo: Hart, Zabaleta, Kompany, Demichelis, Kolarov, Javi Garcia, Toure, Milner, Silva, Nasri, Dzeko.
Wachezaji wa akiba: Richards, Lescott, Negredo, Clichy, Fernandinho, Pantilimon, Jovetic.
Kikosi cha Aston Villa: Guzan, Lowton, Vlaar, Baker, Clark, Bertrand, El Ahmadi, Westwood, Delph, Weimann, Bowery.
Wachezaji wa akiba: Bacuna, Steer, Sylla, Tonev, Holt, Robinson, Grealish.
Mwamuzi: Michael Oliver
Acrobatic: City captain Vincent Kompany attempts an audacious overhead kick 
Vitu vya hatari vya nahodha wa Man City Kompany
On strike: Villa forward Andreas Weimann (right) shoots past City's Pablo Zabaleta 
Shuti kali: Mshambuliaji wa Villa Andreas Weimann (kulia) akiachia shuti kali lililompita beki wa City Pablo Zabaleta
Can't even watch: Manuel Pellegrini can barely look with his side on the brink of a Premier League title 
Hataki kutazama: Manuel Pellegrini yupo katika asilimia kubwa ya kutwaa taji la ligi kuu.

Lining up: Aleksandar Kolarov attempts to hit a free-kick past the Aston Villa wallAleksandar Kolarov akipiga mpira wa adhabu ndogo

Making his point: Paul Lambert shouts instructions to his side from his technical area 
Zuia kule bwana wewe!: Kocha wa Aston Villa, Paul Lambert akitoa maelekezo kwa wachezaji wake
Near miss: A frustrated Samir Nasri misses from close range for Manchester City 
Almanusura apige vitu: Samir Nasri alikosa nafasi nzuri ya kuifungia bao Manchester City
Battle: Goalscorer Dzeko (left) challenges Aston Villa's Karim El Ahmadi 
Vita: Mfungaji mkali,  Dzeko (kushoto) akichuana na beki wa Aston Villa, Karim El Ahmadi
Signs are there: One cheeky City fan won't let Steven Gerrard forget his crucial slip against Chelsea 
Ishara nazo zipo: Shabiki mmoja wa Man City  akionesha bango la kumkejeli  Steven Gerrard

Pleading: Joe Hart reacts as his side move within inches of the Premier League title 
Maombi kwa sana: Joe Hart akiomba baada ya timu yake kukaribia kutwaa ubingwa wa ligi kuu.
Katika mchezo mwingine, maajabu ya soka yameendelea kutokea kwa Sunderland baada ya usiku wa leo kushinda mabao 2-0 dhidi ya West Brom.