Wednesday, June 06, 2012

MWAKYEMBE AMTIMUA KAIMU MKURUGENZI ATCL.

DAR ES SALAAM, TANZANIA.


Waziri wa Uchukuzi wa Tanzania Dr.Arison Mwakyembe aetengua uteuzi wa Kaimu mkurugenzi wa Shirika la ndege la Tanzania(ATCL) bw Paul Chizi na kuwasimamisha kazi wakurugenzi wanne kwa kukiuka sheria taratibu na kanuni za utumishi wa umma.
 Katika taarifa iliyotolewa na Katibu mkuu wa wizara hiyo Bw.Omary Chambo kwawaandishi wa habari, Waziri huyo amefikia uamuzi huo kutokana nauteuzi wa Kaimu mkurugenzi huyo kutofuata utaratibu,   “Uteuzi wake haukufuata sheria, kanuni na taratibu za utumishi wa umma, hivyo kupitia Sheria Na 8 ya mwaka 2002 na kanuni ya Utumishi wa Umma ya mwaka 2003 Na 17(4), Dk Mwakyembe ametengua uteuzi huo kuanzia jana.” alisema katibu Mkuu huyo.
Kutokana na utenguzi huo Waziri mwakyembe amemteua Kapteni Lusajo Lazaro kuwa kukaimu nafasi hiyo.

Waziri huyo pia amewasimamisha wakurugenzi wengine wanne ambao ni  Kaimu Mkurugenzi wa Fedha, Justus Bashara, Kaimu Mkurugenzi wa Uhandisi, John Ringo, Kaimu Mkurugenzi wa Biashara, Josephat Kagirwana Mwanasheria wa ATCL, Amini Mziray. .

Kwa mujibu wa katibuhuyo pia itaundwa tume maalum kuchunguza matumizi ya fedha kuanzia mwezi Mei mwaka huu.

SUDAN YA KUSINI YAPOKWA DOLA BILIONI 4-Rais Kiir azitaka zirudishwe.











sudan kusini
http://www.mideastnewswire.com/wp-content/uploads/2011/02/Salva_Kiir_Khartoum.jpg
Rais Salva Kiir
 Zaidi ya dola bilioni 4 (sawa na zaidi ya Trilioni 6 za kitanzania) Zimeibiwa kutoka Serikali ya Sudan ya Kusini kutokana na ufisadi imebainika. Ufisadi huo umewahusisha viongozi 75 wa ngazi ya juu wakiwemo mawaziri na viongozi wengine wa serikali. Fedha hizo ni pamoja na zaidi yadola bilioni 2 zilizopotea kutokana na ufisadi katika mauzo ya zao la mtama na nyingine katika mafuta.
Rais wa Sudan Bw. Salva Kiir amewaandikia barua wakuu hao akiwataka kuzirudisha fedha hizo ama sivyo watakutana na mkono mkali wa sheria.Kupitia barua alizowaandikia wakuu hao Rais huyo ameonekana kuudhika sana na kitendo hicho akiwaambia wakuu hao waliweka maslahi ya o mbele zaidi ya taifa'
"Raia wa Sudan Kusini wanapata taabu lakini viongozi hawa wanafikiria tu tamaa zao binafsi" alisema Rais Kiir katika barua hiyo.
Rais Kiir amesema sehemu kubwa ya fedha hizo imewekwa kwenye akaunti zilizo nchi za kigeni  na nyingine kununua mali au majengo katika nchi hizo.

Sudan ya Kusini ambayo ilijitenga naSudan Kaskazini nakuwa taifa huru mnamo mwezi Julai mwaka Jana inategemea mafuta kwa asilimia 98 ya kipato chake ambapo kwa sasa imesimamisha uzalishaji wa mafuta hayo kutokana na mgogorio wake na Sudanya Kaskazini nahivyo kuwa na hali ngumu katika kutoa huduma za kijamii.