Saturday, May 19, 2012

MKUTANO WA G8 WAANZA:

 MAREKANI, Mkutano wa nchi tajiri za kwa viwanda umeanza hapo jana huko Camp David,Maryland, Marekani ambapo moja ya Ajenda muhimu ni usalama wa chakula Afrika na hali ya uchumi ulaya hasa katika nchi zenye migogoro ya kiuchumi ikiwemo Uturuki na Ugiriki.
Mkutano huo wa siku mbili unawakutanisha viongozi wa Uingereza,Ufaransa,Ujerumani,Italia,Japan,na Marekani ambaye ni mwenyeji wa mkutano huo.

Moja ya ajenda katika mkutano ni pamoja na Hali ya uchumi Ulaya, Hali ya nyuklia Iran, Hali ya Syria, Pia usalama wa chakula na nishati duniani ikiwemo Afrika.

Hata hivyo licha ya ajenda hizo bado wengi hawana matumaini na mkutano huo kwani iliyotangulia haikuzaa matunda kama ilivyotegemewa.

MAELFU WAKIMBIA MAPIGANO DRC

Moja ya kundi la wakimbizi wakiwa njiani Goma.

Bunagana, DR Congo - Mapigano yanayoendelea huku Kivu Kaskazini mashariki ya Kongo yamewalazimisha wakazi wa maeneo hayo kukimbilia nchi za jirani za Rwanda na Uganda kuokoa maisha yao.Wanawake na watoto ni moja ya kundi kubwa katika msafara huo.


Wananchi hao wanakimbia kuhofia kushambuliwa na waasi wanaoipinga  serikali ya kinshasa wakiongozwa naaliyekuwa kamanda wa jeshi la kongo Jenerali Ntaganda.
Tumesikia mapigano kati ya waasi na Serikali, kwa hiyo tumekimbia huku kujiokoa kwa sababu kubaki kule ni kuhatarisha maisha yetu" alisema kajambere seberera  ambaye yupo nchini Uganda baada ya kukimbia mapigano hayo.


Hata  hivyo hali sio nzuri katika kambi za UNHCR  Kisoro nchini Uganda ambapo licha ya kufunguliwa sehemu hiyo bado chakula, malazi na maji vimekuwa ni tatizo.Baadhi ya wakimbizi hao wamelazimika kulala nje huku wengine wakirudi Kongo mchana kutafuta maji na Chakula.


Hali imekuwa ngumu zaidi kwa watoto na akinamama waliovuka mipaka ambao idadi yao ni kubwa.


Mapigano hayo kati ya majeshi ya serikali na yale ya majeshi ya Kamanda muasi Jenerali Ntaganda yalianzayamesababisha usumbufu mkubwa katika eneo hilo la Kivu na maeneo menginene nchini humo.

MKURUGENZI WA TBS ASIMAMISHWA KAZI.

Mkurugenzi wa TBS Charles Ekerege.
 Dar es Salaam, Siku chache baada ya kuteuliwa waziri wa viwanda Mh.Abdallah Kigoda ametoa maagizo ya kusimamishwa kazi kwa Mkurugenzi mkuu wa shirika la Viwango tanzania TBS Bw Charles Ekelege. Akiongea na waandishi wa habari hapo juzi Waziri kigoda amesema Moja ya sababu za rais kuamua kuvunja baraza la mawaziri lililokuwepo ni pamoja na tuhuma nzito zilizokuwa zikielekezwa TBS hivyo ni vyema mkurugenzi huyo akasimamishwa kupisha uchunguzi na hatua zaidi za kisheria.


Wachunguzi wa mambo wanahisi hiyo ni sehemu ya ahadi alizotoa rais Kikwete katika hotuba yake siku alipokuwa akitangaza baraza jipya la Mawaziri ambapo aliahidi kuwawajibisha watendaji wa ngazi za chini pia ambao mara nyingi ni chanzo cha mawaziri kuwajibika.

Imekuwa ni kawaida kwa watendaji wengi wa ngazi za chini katika wizara kuzembea kwa kuelewa kuwa wao sio wawajibikaji wa moja kwa moja zitokeapo tuhuma pengine hatua hizi zitasaidia.

MPENDWA PATRICK MAFISANGO AAGWA TCC.

Mwili wa mafisango Ukiwa Umebabwa na wachezaji wenzake.
Juma Kaseja Akilia Kwa uchungu.
Mdogo wa marehemu Akisaidiwa baada ya kuishiwa nguvu.
Kocha wa Simba Milovan.
Dar Es Salaam, Mwili wa aliyekuwa mchezaji wa Simba na timu ya taifa ya Kongo, Patrick Mutesa Mafisango umeagwa rasmi katika viwanja vya TCC Chng'ombe Jijini dar es Salaam,na mamia ya wanamichezo wakiongozwa na waziri wa michezo Dr.Fennela Mukangala.

Waombolezaji wengine(Picha zote kwa hisani ya millardayo.com na Global Publishers)
Wengi wa mashabiki na wapenzi hao wa soka walionekana kuwa na majonzi huku wachezaji wenzake,pamoja na kocha wa Timu ya Simba Milovan wakishindwa kujizuia kwa machozi.

mwili wa mafisango umesafirishwa jioni ya Ijumaa hii kuelekea nyumbani kwao Nchini Kongo kwa ajili ya mazishi yatakayofanyka siku ya Jumapili mchana.

Patrick mafisango mchezaji wa timu ya Simba na Timu ya taifa ya Kongo alikuwa mfungaji namba tatu wa ligi kuu ya Vodacom msimu huu na alikuwa na msaada mkubwa katika kufanikisha Timu ya Simba kupata ubingwa Msimu huu, Anga za Kimataifa Inaungana na wadau wote wa Michezo pamoja na familia ya marehemu Kumuombea heri ; MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALA PEMA PEPONI, AMEN.

SINGLE BOY OFFICIAL VIDEO-ALI KIBA FT JAY DEE.