Wednesday, January 07, 2015

Watu 11 wauawa katika shambulio katika shambulio lililotekelezwa na watu wasiojulikana Ufaransa

  1. Shambulio katika kituo kimoja cha magazeti nchini Ufaranza
  2. Takriban Watu 11 wameuawa na watano kujeruhiwa katika shambulio lililotekelezwa na watu wasiojulikana.Shambulio hilo lililitekelezwa kwenye ofisi ya gazeti la Charlie Hebdo jijini Paris nchini Ufaransa.
  3. Watu wenye silaha waliingia kwenye jengo na kuanza kufyatua risasi wakiwa na silaha ambapo inaelezwa milio takriban hamsini ya risasi ilisikika, kisha Watu hao walikimbia kwa gari.
  4. Polisi wanafanya jitihada za kuwapata waliohusika na shambulio hilo. Mji wa Paris umewekwa katika taadhari kubwa ya kiusalama.

Messi mchezaji ghali zaidi duniani

  • shirikishe mwenzako
Lionel Messi ni ghali zaidi ya Christiano Ronaldo
Mshambuliaji wa Klabu ya Barcelona Lionel Messi ambaye jina lake limekuwa Maarufu katika mchezo wa soka duniani amekuwa ghali Zaidi ya Wachezaji wengine ambao wanashindana na Messi katika ubora wa kiwango Duniani
Orodha hiyo imeyonyesha majina ya wachezaji na viwango vya fedha ambazo zimekuwa zikutumika kuwasajili wachezaji hao kwenda katika vilabu Tajiri.
Lionel Messi £172.6m 2. Cristiano Ronaldo £104.3m 3. Eden Hazard £77.6m 4. Diego Costa £65.9m 5. Paul Pogba £56.4m 6. Sergio Aguero £51m 7. Raheem Sterling £49.4m 8. Cesc Fabregas £48.6m 9. Alexis Sanchez £47.8m 10. Gareth Bale £47m
Mchezaji mwingine ambaye amekuwa anahusishwa kuingia katika ushindani ni Luis Suarez, ambaye alikuwa nyuma ya Messi na Cristiano kwa kwa kiwango cha paundi 107,000,000 kabla ya Kombe la Dunia na baada ya miezi minne.