Tuesday, February 12, 2013

NECTA WATOA TAMKO RASMI KUHUSU MATOKEO YA KIDATO CHA NNE


Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) limesema matokeo ya kidato cha nne bado hayajakamilika na kuwa habari zilizozagaa wiki hii kuwa yapo tayari si za kweli.

Hata hivyo Baraza hilo limebainisha kuwa licha ya kutokamilika, matokeo hayo yanakaribia kutoka kwa mujibu wa ratiba za baraza hilo ambapo hutakiwa kutoa matokeo hayo mwezi Februari.

Akizungumza na mwandishi jana, Ofisa Habari na Mawasiliano wa NECTA, John Nchimbi alisema uvumi wa kwamba matokeo hayo yako tayari ulitokana na kuzushwa kupitia mtandao wa kijamii (Facebook).

Alifafanua kwamba habari kuwa matokeo hayo yameanza kutoka kisirisiri kabla hayajatangazwa rasmi na kwamba hatua hiyo inalenga kuyachakachua, siyo taarifa sahihi.

Aliwataka wananchi kuwa makini na uvumi huo kwa vile endapo matokeo hayo yatakuwa tayari yatatangazwa na Katibu Mtendaji wa Baraza hilo na pia kuwekwa kwenye tovuti ya Baraza pamoja na wananchi kuweza kuyapata kupitia simu zao za mkononi.
 
Uvumi huu umetokana na mtu asiyejulikana kufungua akaunti ya facebook yenye jina la Baraza na kuanza kuweka taarifa hizo zisizo sahihi. Napenda kuwajulisha wananchi kuwa Baraza letu halina mtandao kama huo hivyo taarifa hizo si sahihi.

Nchimbi alibainisha kuwa matokeo hayo si siri hivyo yakiwa tayari Katibu Mtendaji atayatangaza kupitia vyombo vya habari na baadaye yataanza kusambazwa kwa kutumia mtandao.

Aliwataka wananchi kuwa makini ili wasitapeliwe na wanaojifanya kuwa wanaweza kupata matokeo ya mwanafunzi kabla hayajatangazwa rasmi kwa vile suala hilo haliwezekani.

CCM YATANGAZA WAJUMBE WAPYA WA KAMATI KUU.

 
 
DODOMA-TANZANIA, Halmashauri Kuu ya CCM Taifa imewachagua wajumbe wafuatao kuwa wajumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri  Kuu Taifa wa chama hicho.

BARA:
 1.Ndg Stephen Masatu Wasirra. 2. Ndg Jerry Silaa. 3. Ndg William Lukuvi.

4.Ndg Alhaj Adam Omari Kimbisa. 5. Ndg Prof Anna Kajumulo Tibaijuka.

6.Ndg Pindi Hazzara Chana. 7. Ndg Emmanuel J Nchimbi.

Wafuatao kura hazikutosha-Bara

-Ndg Chriss Chami, Ndg Said Mtanda, Ndg Mohammed Nyundo,
-Ndg George Mwanisongole, Ndg Michael Lekule Laizer.
-Ndg Dr Fenela Mukangara, Ndg Anthony Dialo, Ndg Raphael Chegeni na wengine.

VISIWANI:

 1.Ndg Dr Salim Ahmed Salim, 2. Ndg Prof Makame Mbarawa.
 3.Ndg Dr Hussein A Mwinyi, 4. Shamsi Vuai Nahodha.
 5.Ndg Dr Maua Abeid Daftari, 6. Ndg Khadija Aboud.
 7.Ndg Samia Suluhu Hassan.

Wafuatao kura hazikutosha- Visiwani

Alli A Karume, Juma Shamhuna, Mohammed Aboud na wengine

Kutokana na uchaguzi huo baadhi ya makada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wamempongeza Mwenyekiti wa Chama hicho Taifa, Rais Jakaya Kikwete pamoja na wajumbe kwa kuichagua timu hiyo. Kidumu Chama Cha Mapinduzi.

Mtandao wa www.habarimasai.com umeelezwa kwamba wajumbe waliochaguliwa ni makini na kwamba CCM ina imani nao kuwa wataivusha katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.

PAPA BENEDICT XVI ATANGAZA KUJIUZULU


http://l1.yimg.com/bt/api/res/1.2/OghHOUVGAdw5jkaiqHQlag--/YXBwaWQ9eW5ld3M7Zmk9aW5zZXQ7aD0zMzM7cT04NTt3PTUxMg--/http://media.zenfs.com/en_us/News/Reuters/2013-02-11T122658Z_1146797572_GM1E92B1JT301_RTRMADP_3_POPE-RESIGNS.JPG

http://l.yimg.com/bt/api/res/1.2/fBMzX47bwjrUut5Sd2DYZQ--/YXBwaWQ9eW5ld3M7Zmk9aW5zZXQ7aD05MDA7cT03OTt3PTczNg--/http://media.zenfs.com/en_us/News/ap_webfeeds/cef0a2fc2096a524240f6a70670052e7.jpg
 http://l3.yimg.com/bt/api/res/1.2/1bfogd5OFbiezWIzY32kIQ--/YXBwaWQ9eW5ld3M7Zmk9aW5zZXQ7aD01MDY7cT04NTt3PTYzMA--/http://media.zenfs.com/en_us/News/ap_webfeeds/7bca85b520d8a624240f6a70670087f4.jpg
VATICAN-ITALIA,
Kadinali Joseph Ratzinger ama Papa Benedict XVI  ametangaza uamuzi wa kujiuzulu mwishoni mwa mwezi huu baada ya takriban miaka minane akiongoza Kanisa Katoliki kwa hoja kuwa umri wake wa miaka 85 ni mkubwa kiasi kwamba hawezi kuendelea kuhudumu zaidikutokana na kudhoofu kimwili na kiakili.

Makao makuu ya Kanisa Katoliki huko Vatican yanasema yanatarajia Papa mpya atachaguliwa kabla ya mwisho wa mwezi wa tatu, na sherehe za Pasaka.

 Tukio jipya katika karne za hivi karibuni., ambapo papa wa mwisho kujizulu alikuwa ni Papa
Msemaji wa Vatikani Father Federico Lombardi, amesema kuwa hata wasaidizi wa Papa wa karibu mno hawakuwa na fununu juu ya tukio hili.

Kakake Papa huyu mzaliwa wa Ujerumani alipewa ushauri na Daktari wake asifanye ziara nyingine yoyote ya Marekani na kwamba kwa miezi kadhaa Mtakatifu Papa amekuwa akitafakari kujiuzulu.
Akizungumza kutoka nyumbani kwake huko Regensburg, Ujerumani, Georg Ratzinger amesema kuwa Kaka yake alikuwa ameanza kupata shida ya kutembea na kwamba kujiuzulu kwake ni hatua ya kimaumbile.


VIDEO YA PAPA AKITANGAZA KUJIUZULU:

Wakati wa kutawazwa kama Papa, Kadinali Joseph Ratzinger alikuwa mmojawapo wa mapapa wapya kuchaliwa akiwa mwenye umri mkubwa wa miaka 78.
Alitangazwa Papa mnamo mwezi Aprili 2005 kufuatia kifo cha marehemu John Paul wa pili.
Uongozi wake ulitokea wakati wa wimbi kali la ubakaji kulikumba kanisa katoliki katika kipindi cha miongo mingi, ubakaji uliofanywa na watawa dhidi ya watoto wavulana.

Katika taarifa yake, Mtakatifu Papa amesema: "baada ya kujichunguza binafsi na nafsi yangu mbele ya Mola wangu, nimefikia uwamuzi kua uwezo wangu na afya, ukiambatana na umri mkubwa, ni mambo yatakayokwaza jitihada zangu za kuendelea kuliongoza Kanisa Katoliki.

Kuna kipengele katika sheria ya Kanisa kinachosema kuwa kujiuzulu kwa Papa kunakubalika iwapo kitendo hicho kimefanywa kwa hiari na kwa utaratibu unaostahiki.

Hata hivyo kujiuzulu huko kumepokewa kwa hisia tofauti ambapo wapo waliokubaliana na wengine wakionekana kusita akiwemo katibu mkuu wa Papa John Paul II aliyeshikilia wadhifa wake mpaka mwisho wa uhai wake licha ya kuugua,Kadinali Stanislaw Dziwisz ambaye amewaambia waandishi wa habari nchini Polland kuwa "Haikutakiwa  kushuka kutoka katika msalaba".kwa upande wao viongozi wa duni wameupokea kwa hudhuni uamuzi huo ingawa wameuunga mkono.Waziri mkuu wa Ujerumani  Angela Merkel amesema uamuzi wa papa unapaswa kuheshimiwa ikiwa amejiuzulu kwa kujiona ni dhaifu kutekeleza majukumu yake, huku David Cameron waziri mkuu wa Uingereza akisema Papa benedict XVI atakumbukwa kiroho na mamilioni ya wafuasi wa dini".