Friday, January 30, 2015

Polisi wamkatama Wema Sepetu

Katika hali ya kushangaza, polisi walijikuta wakipata shughuli pevu kumkamata staa asiyeishiwa matukio Bongo, Wema Sepetu ambaye alidaiwa kupiga muziki kwa sauti kubwa usiku kucha pasipo kuwa na kibali, Amani linakupa mchapo.

Tukio hilo lilitokea Jumanne iliyopita, nyumbani kwa mwigizaji huyo, Kijitonyama jijini Dar kulikokuwa na bethidei ya rafiki yake aliyejulikana kwa jina moja la Neema.
Awali, mapaparazi wa GPL walipokea simu ya mmoja wa majirani wa Wema ambaye alidai mwigizaji huyo amekuwa na tabia ya kufanya sherehe kwake na kufungulia muziki mkubwa ambao unasababisha kero.
“Kwa kweli ni kero, kila mara amekuwa na tabia ya kupiga muziki mkubwa katika sherehe zake ambazo hazina kichwa wala miguu. Kama jana (usiku wa Jumatatu) muziki ulifunguliwa kuanzia saa mbili usiku mpaka asubuhi na majirani walimfuata Wema mara kadhaa kumtaka apunguze sauti lakini aliwajibu vibaya.
“Njooni mshuhudie wenyewe, tumeita polisi wamkamate,” alisema jirani mmoja.
Mapaparazi wetu walichukua usafiri wa pikipiki na kuwahi fasta na kukuta polisi wakihangaika kwa muda mrefu kumkamata mrembo huyo lakini ikashindikana kwa kuwa alikuwa amelewa na kukimbia hovyo huku akiwa nusu utupu.

“Kwa sababu hiyo walimkamata mmiliki wa muziki ambaye jina lake halikupatikana mara moja na mwenye sherehe (Neema) kisha kwenda nao katika ofisi za mtendaji, Kijitonyama  kwa ajili ya hatua za kisheria,” alisema.
Akizungumza na GPL, mwenyekiti wa mtaa huo, Mzee Haogwa, alithibitisha kuletewa malalamiko ya Wema na kufika nyumbani hapo ambapo pia alidai alishangazwa na kitendo cha kuwakuta wanaume tata kwenye sherehe hiyo.
Picha: Timu iliyofika nyumbani kwa Wema Sepetu kumkamta kwa usumbufu aliosababisha kwa majirani.Wakachikua spika na kumbeba mwenye sherehe, Neema( rafiki wa Wema Sepetu) kwenye bajaji.GPL

Monday, January 26, 2015

MKE WA WAZIRI MKUU MAMA TUNU PINDA ATUNIKIWA SHAHADA YA UZAMILI YA USIMAMIZI WA MIRADI.


Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania Dkt. Asha-Rose Migiro akimtunuku shahada ya uzamili ya usimamizi wa miradi mke wa Waziri Mkuu mama Tunu Pinda katika mahafali ya 27 ya chuo hicho yaliyofanyika mjini DODOMA. Kushoto anayeshuhudia ni Makamu mkuu wa chuo hicho 
Profesa Tolly Mbwete.
 Mke wa Waziri Mkuu mama Tunu Pinda  akitoka kupokea shahada ya uzamili ya usimamizi wa miradi. Akiongea baada ya hapo Mama Pinda ametoa wito kwa kinamama wa Tanzania na Afrika kwa jumla kujiendeleza kielimu ili kukomboa mataifa yako kutoka katika dimbwi la umaskini
 Kikundi cha wake wa viongozi kutoka Dar es salaam kikimpongeza mlezi wao Mama Tunu Pinda kwa kutunukiwa shahada ya  uzamili ya usamamizi miradi ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania katika mahafali ya 27 iliyofanyika Mjini Dodoma. Toka  kushoto ni  Mama Mashiba,  Mama Lukuvi na Mama Malima .

Uzinduzi wa Sherehe za CCM Miaka 38 Kisiwani Pemba.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Viongozi wa CCM wakati alipowasili katika uwanja wa  Gombani Wilaya ya Chake chake Pemba leo kuzindua sherehe za maadhimisho ya miaka 38 ya kuzaliwa Chama cha Mapinduzi CCM,
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) Katibu Mkuu CCM Taifa Abdulrahman Omar Kinana na Nainu katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai (kulia) Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kusini Pemba Bakari Mshindo (wa tatu kushoto) Spika wa Baraza la Wawakilishi Pandu Ameir Kificho na Mke wa Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman Iddi (kushoto) wakipiga makofi ulipopigwa wimbo wa Chama kumpokea Dk.Shein alipofika kuzindua Sherehe za maadhimisho ya miaka 38 ya kuzaliwa CCM katika uwanja wa Gombani Wilaya ya Chake chake Pemba leo,

Wajumbe wa Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM Zanzibar walipokuwa wakiwasalimia WanaCCM wa Mikoa miwili ya Pemba wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya Sherehe za miaka 38 ya kuzaliwa kwa CCM zilizofanyika leo katika uwanja wa  Gombani Wilaya ya Chakechake Mkoa wa Kusini Pemba,mgeni rasmi akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein 
Vijana wa Chipukizi wa CCM Kisiwani Pemba wakiimba Wimbo Maalum wa kuzaliwa CCM wakati wa Sherehe za maadhimisho ya miaka 38 katika uwanja wa Gombani Wilaya ya Chake chake Pemba leo,ambapo mgeni rasmi akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein(hayupo pichani)
Picha ya Muasisi wa Chama cha Mapinduzi CCM na Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere ikinyanyuliwa juu wakati Wimbo maalum ukiimbwa na Vijana wa Chipukizi walioshiriki halaiki katika uzinduzi wa maadhimisho ya Sherehe za miaka 38 ya kuzaliwa kwa CCM zilizofanyika leo katika uwanja wa  Gombani Wilaya ya Chakechake Mkoa wa Kusini Pemba

Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai alipokuwa akisema machache na kumkaribisha katibu Mkuu wa CCM Taifa Abdulrahman Omar Kinana ili awaslimie wananchi wa Mikoa ya Pemba wakati wa  uzinduzi wa maadhimisho ya Sherehe za miaka 38 ya kuzaliwa kwa CCM zilizofanyika leo katika uwanja wa  Gombani Wilaya ya Chakechake Mkoa wa Kusini Pemba
Baadhi ya WanaCCM wa Mikoa miwili ya Kisiwa cha Pemba wakiwa katika Uzinduzi wa Mkutano Maalum wa Sherehe za kuadhimisha miaka 38 ya kuzaliwa CCM uliofanyika leo katika uwanja wa Gombani Wilaya ya Chakechake Mkoa wa Kusini Pemba uliohutubiwa na  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akiagana na  Katibu Mkuu CCM Taifa Abdulrahman Omar Kinana baada ya kumalizika kwa Mkutano wa maadhimisho ya sherehe za miaka 38 ya kuzaliwa kwa CCM uliofanyika leo katika uwanja wa Gombani Wilaya ya Chake chake Mkoa wa Kusini Pemba,[Picha na Ikulu.

Sunday, January 11, 2015

Utafiti umefanyika kuhusu wanaopenda SELFIE, matokeo yanaonyesha wana hii tabia…

Selfie Woman
Wale wapenzi wa SELFIE naomba kushare na nyie watu wangu hii story.
Kuna utafiti uliofanywa na Ohio State University Marekani, unahusu masuala ya athari zinazoweza kusababishwa na watu kupendelea kupiga Selfie na kupost kwenye mitandao kama Istagram.
Jumla ya watu waliofanyiwa utafiti huo walikuwa 800, umri wao ulikuwa kati ya miaka 18 na 40.
Matokeo yanaonyesha kuwa watu wanaopenda kujipiga Selfie wakiwa peke yao wanakuwa na tabia ya ubinafsi na hawapendi kujichanganya na watu wengine.
Tabia hiyo inaonenaka ‘imekomaa’ zaidi kwa wale wanaopenda kuedit Selfie zao kabla hawajapost kwenye mitandao.
Hayo ni matokeo yao, wewe unasemaje hapo mtu wangu, eti ni kweli? Nitafurahi ukiniandikia chochote kuhusu hii.

Wednesday, January 07, 2015

Watu 11 wauawa katika shambulio katika shambulio lililotekelezwa na watu wasiojulikana Ufaransa

  1. Shambulio katika kituo kimoja cha magazeti nchini Ufaranza
  2. Takriban Watu 11 wameuawa na watano kujeruhiwa katika shambulio lililotekelezwa na watu wasiojulikana.Shambulio hilo lililitekelezwa kwenye ofisi ya gazeti la Charlie Hebdo jijini Paris nchini Ufaransa.
  3. Watu wenye silaha waliingia kwenye jengo na kuanza kufyatua risasi wakiwa na silaha ambapo inaelezwa milio takriban hamsini ya risasi ilisikika, kisha Watu hao walikimbia kwa gari.
  4. Polisi wanafanya jitihada za kuwapata waliohusika na shambulio hilo. Mji wa Paris umewekwa katika taadhari kubwa ya kiusalama.

Messi mchezaji ghali zaidi duniani

  • shirikishe mwenzako
Lionel Messi ni ghali zaidi ya Christiano Ronaldo
Mshambuliaji wa Klabu ya Barcelona Lionel Messi ambaye jina lake limekuwa Maarufu katika mchezo wa soka duniani amekuwa ghali Zaidi ya Wachezaji wengine ambao wanashindana na Messi katika ubora wa kiwango Duniani
Orodha hiyo imeyonyesha majina ya wachezaji na viwango vya fedha ambazo zimekuwa zikutumika kuwasajili wachezaji hao kwenda katika vilabu Tajiri.
Lionel Messi £172.6m 2. Cristiano Ronaldo £104.3m 3. Eden Hazard £77.6m 4. Diego Costa £65.9m 5. Paul Pogba £56.4m 6. Sergio Aguero £51m 7. Raheem Sterling £49.4m 8. Cesc Fabregas £48.6m 9. Alexis Sanchez £47.8m 10. Gareth Bale £47m
Mchezaji mwingine ambaye amekuwa anahusishwa kuingia katika ushindani ni Luis Suarez, ambaye alikuwa nyuma ya Messi na Cristiano kwa kwa kiwango cha paundi 107,000,000 kabla ya Kombe la Dunia na baada ya miezi minne.