Tuesday, May 29, 2012

MLIPUKO MKUBWA WATOKEA TENA KENYA!

NAIROBI,KENYA, Mlipuko mwingine umetokea sehemu yenye maduka mengi  katikati ya jiji la Nairobi karibu na Chuo kikuu cha Mount Kenya na kujeruhi watu wapatao 16 kwa mujibu wa  polisi.
habari zilizotolewa leo na chanzo cha polisi zimesema mlipuko huo umetokana na bomu.
Mlipuko mkubwa ulitokeamnamo saa 7:10 mchana saa za Afrika mashariki katika moja ya majengo yaliyopakana na maghorofa maeneo hayo , baadhi ya mashuhuda wamesema wanamhisi mtu aliyekuwa na begi aliyekuwa akija na kuondoka  eneo hilo.
Majeruhi walionekana wakipewa huduma na watu wa afya ambao walijaribu kuwaondoa mamia waliokusanyika katika eneo hilo kama mashuhuda.Picha za televisheni za Kenya zilionesha moshi mkubwa ukitoka katikakati ya majengo hayo.
Ingawa bado haijathibitka imeaminiwa kuwa kundi la kigaidi la nchini Somalia la Al-Shabab limehusika na mlipuko huo.Kundi hilo liliahidi na limehusika kutekeleza mashambulio kama hayo yaliyotokea nchii humo hivi karibuni, baada ya serikali ya Kenya kuingia nchini Somalia kwa lengo la kuendesha operesheni ya kulisambaratisha kundi la Al-Shabab.

VURUGU ZAENDELEA ZANZIBAR.

Vurugu zilizozuka tangu juzi na kutulia kwa muda zilizuka tena hapo jana baada ya  Mhadhiri wa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislam Zanzibar (Jumiki), Sheikh Musa Juma Issa kurudishwa rumande. Vijana waliokuwa wakipinga kurudishwa rumande kwa Mhadhiri huyo walichoma matairi barabarani na kuzua
 tafrani.
Vurugu hizo zimetokea baada ya utulivu uliojitikeza baada ya Dk Emmanuel Nchimbi na Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Said Mwema kuitisha mkutano uliojumuisha taasisi mbalimbali kwa lengo la kupata ufumbuzi wa vurugu hizo.
Hata hivyo kitendo cha kurudishwa rumande kwa Sheikh Issa aliyeshindwa kutimiza masharti ya dhamana kulizua vurugu tena  katika maeneo ya Mwanakeretwe na  Amani .

Polisi walilazimika kutuliza vurugu hizo kwa kutumia mabomu ya machozi ili kuwatawanya vijana hao

Hadi jana jioni, maeneo ya Chumbuni, Amani, Mwembaladu hali ilikuwa bado tete huku polisi wakifunga barabara kwa ajili ya kudhibiti vijana hao.