Meneja msaidizi wa Castle Lite, Victoria Kimaro akizungumza katika
uzinduzi wa kampeni ya shindano la Lite Up The Weekend ambapo washindi
watajipatia VIP tiketi ya kushiriki katika Yacht Party. Katikati ni
Meneja wa Castle Lite Geofray Makau na pembeni ni meneja masoko wa
Castle Lite Vimal Vaghmaria.
Wanahabari wakielekea eneo la maegesho ya Yacht itakayotumika katika kilele cha cha kampeni ya Lite Up The Weekend.
Muonekano wa Yacht itakayoandaliwa maalum kwa ajili ya washindi wa shindano la Lite Up the weekend.
Mmoja ya wadau wadau wa Castle Lite katika pozi ndani ya Yacht.
Meneja masoko wa Castle Lite Vimal Vaghmaria na Stanley Kafu wa Aggrey & Clifford wakifurahia ndani ya Yacht.
Wanahabari katika pozi la pamoja na wadau wa Castle Lite.
Dar es Salaam, Aug 11, 2014:
Bia maarufu ya Castle Lite, inayozalishwa na
kusambazwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) leo imezindua rasmi promosheni ya
aina yake itakayojulikana kama “Lite Up
The Weekend”. Promotion hii ya aina yake hapa nchini itadumu kwa kipindi
cha miezi mitatu kuanzia mwezi Agosti hadi Octoba 2014.
Akizungumza katika uzinduzi huo, meneja wa Bia ya
Castle Lite Geoffrey Makau alisema; Bia ya Castle Lite kwa mara nyingine tena
inawaletea wapenzi wa bia hii habari nzuri na za kuvutia. Leo tunazindua
promosheni kubwa itakayojulikana kama “Lite Up The Weekend”.
Hii ni promosheni kubwa itakayoendeshwa nchi nzima.
Washindi watashiriki kwenye hii promosheni kupitia chupa za bia ambazo
watatakiwa kutuma nambari ya siri iliyochini ya kizibo cha bia ya Castle Lite.
Tumewaandalia wateja wetu zawadi mbalimbali
zitakazokuwa zikitolewa kila wiki, ikiwa ni pamoja na zawadi za pesa taslimu,
zawadi za vifaa vya kusikilizia muziki (headfone) n.k, lakini zawadi kubwa
zaidi ni ile ya washindi kupata fursa ya kusherehekea kwenye VIP Party ndani ya
Boti ya kifahari. Sherehe hii itajulikana kama “Castle Lite VIP Yacht Party”
Mteja atatakiwa kununua bia ya Castle Lite ya chupa
yenye ujazo wa mililita 375 au 330 na kuangalia chini ya kizibo cha Bia, ambapo
atakuta namba za siri, kisha atatuma namba hizo kwenda 15499 au kutembelea
website yetu ambayo ni, www.castlelite.co.tz, ili apate nafasi ya kushinda
zawadi za kila wiki au zawadi kubwa ya “Castle Lite VIP Yacht Party”.
Washindi wa zawadi kubwa kutoka mikoa mbali mbali
ya Tanzania, watapata fursa yakuparty na wenza wao kwenye boti la kifahari aina ya yacht, ambayo itaondoka
Dar kuelekea kisiwa kizuri kilicho andaliwa kwa ajili yao, huku wakiburudishwa kwa
chakula, vinywaji na muziki
Promosheni hii pia itapewa msukumo mkubwa kupitia
Radio, ambapo wapenzi wa Castle Lite watapigiwa simu na watatakiwa wapokee kwa
kuanza na neno ya “Lite Up My Weekend”. wateja watakaofanya vizuri watapata
zawadi mbalimbali kila wiki. Alisema Makau.
Zaidi ya zawadi za kila wiki, wateja pia watashinda
nafasi za kuhudhuria matamasha mbalimbali yanayoambatana na muziki hapa nchini.
Ninawaomba sana wapenzi wa bia hii ya Castle Lite, kushiriki mara nyingi
iwezekanavyo ili kushinda zawadi hizi za kuvutia, aliongeza Geoffrey.