Msanii mkongwe wa Hip Hop Proffesor Jay amesema kuwa kushindwa kwa Diamond kuchukuwa tuzo za MTV kusimvunje moyo kwakuwa alikuwa anashindana na wasanii wakubwa sana Africa.
Akizungumza na mtandao huu leo
,Proffesor Jay amesema kuwa nafasi aliyopata Diamond na kushindana na
wasanii hayo ni ushindi mkubwa wake.
“Diamond
lazima ajue katika mashindano kuna kushinda na kushindwa, Kitu ambacho
ninaweza kumwambia Diamond asikate tamaa, ameshindanishwa na wasanii
wakubwa sana ambao pia ni advantage kwake ,msanii kama Davido pamoja na
kufanya muziki mzuri tutambue kuwa nyuma yake kuna Wanageria zaidi ya
milioni 150, ambao kiukweli wenzetu wameamka sana kuchangia kuwa support
wasanii wao, sisi Watanzania tumekuwa tunazungumza kwa maneno mengi
kulipo vitendo ,so mtu kama Davido ameshinda kwa kupigiwa kura na watu
wake wengi na muziki wake umefika afrika nzima. Kwaiyo kushindwa kwake
Diamond asichukulie kukata tamaa ,yeye achukulie kama changamoto na
kuwashawishi Watanzania na mashabiki wake kuendelea ku support muziki
wake ili afike mbali zaidi, naamini kuna kila dalili kwa Diamond kuendelea kufanya vizuri zaidi hapo mbeleni, pia nataka niwaambie Watanzania
kwamba mtu anapoiwakilisha Tanzania tujitaidi kuweka tofauti zetu nyuma
na kum,support wasanii wetu kwa sababu ushindi wake ni mafanikio
makubwa ya muziki wetu,wasanii na wetu, na taifa kwa ujumla” Alisema Proffesor Jay.
Katika hatua nyingine Proffesor Jay amesema kuwa kesho anaingia mzigoni kuanza kushoot video ya ‘Kipi Sijasikia’ “Kesho
naanza ku,shoot video ya Kipi Sijasikia, kilichotokea nilikuwa
namsubiri tu Diamond, kwa sababu ratiba yake ilikuwa imebana sana, kila
kitu sasa hivi kipo set, na tunafanya na Adam Juma, kilichotufanya tu
delay kidogo ni kwa sababu alikuwa ameagiza Red na vitu vingine, kwaiyo
vikawa vimechelewa kidogo lakini baada ya kuingia vyombo vyake, kesho
tunaanza lakini ataujajua tutamaliza lini.Adam amenivutia
sana sasa hivi kwa sababu ya kubadilisha kamera , Adam ana skills kubwa
ya kutumia kamera , lakini kamera ambazo alikuwa akitumia mwanzo
zilikuwa zinambana kidogo lakini sasa hivi kwa kuleta kamera hiyo Red na
vitu vingine kama hivyo tunategemea uwezo wake anaweza akaonyesha kwa
mapana zaidi , na pia tumejaribu tunatumia advantage ya Diamond huko
anakozunguka kujaribu kufanya connection, kwa sababu Diamond anaweza
kusaidia muziki wetu kifika mbali zaidi”Alisema Proffesor.