Saturday, June 28, 2014

WEMA SEPETU AKUNATA USO KWA HUSO NA PENNY ALIYEKUWA MPENZI WA DIAMOND..!! HIKI NDICHO KILICHOTOKEA

Katika hali isiyotarajiwa, mchumba wa Mbongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’, Wema Sepetu na aliyewahi kuwa mchumba wa msanii huyo, Penniel Mungilwa ‘Penny’ walikutana studio na kila mmoja akamkwepa mwenzake.

Tukio hilo lilitokea juzikati maeneo ya Posta, jijini Dar katika Studio za Amaya ambayo ni saluni inayotumika kurekodia vipindi mbalimbali vya Mkasi vinavyorushwa kupitia Runinga ya EATV.
Kwa mujibu wa chanzo makini, mwigizaji Aunt Ezekiel alialikwa na mtangazaji wa kipindi hicho, Salama Jabir kwenda kufanya mahojiano, akaambatana na shosti wake Wema ndipo ghafla wakakutana na Penny ambaye naye alialikwa kwa wakati wake.
Chanzo kilizidi kumwaga data kuwa, baada ya Aunt na Wema kufika studio hapo, Salama aliwakaribisha na wakaanza kurekodi kipindi hicho, lakini walipokuwa wakiendelea na mahojiano, Penny naye aliwasili bila kujua kama Wema alikuwepo.

“Penny alipofika alizama ndani na kukutana na Salama ambaye alimwambia kuwa kuna watu wanatoka ndani muda si mrefu hivyo wakati bado wanaongea, Wema na Aunt walitoka studio ambapo Penny alikimbilia kwenye gari lake kukwepa kuonana na Wema ambaye pia alionekana kutotaka kuonana na Penny,” kilisema chanzo na kuongeza:
“Kwa kuwa Wema naye alimuona kwa mbali Penny, alimtaka Aunt waingie kwenye gari fastafasta na kuondoka eneo hilo.”




Mapaparazi wetu baada ya kuunyaka mchongo huo, walimtafuta Penny ili kumsikia anazungumziaje ishu hiyo. Alipopatikana, alijibu hivi:
“Mimi sikumkimbia Wema na itambulike kuwa wakati naenda pale sikujua kama Wema alikuwepo hivyo nilifika na kusubiria muda wangu wa mahojiano nikiwa ndani ya gari, sikuwa na haja ya kujua Wema yupo ama la.”
Jitihada za kumpata Wema hazikuzaa matunda lakini alipotafutwa Aunt Ezekiel, alitiririka:
“Nilimuona Penny kweli pale studio ingawa mwanzo nilitahamaki maana sikujua kama naye alikuwa akisubiria tutoke aingie kwenye kipindi ila Salama alinishtua sana baada ya kusema kabla hatujatoka ndani tusubiri aandae uwanja wa ngumi, alitania.”
Wema na Penny wanadaiwa kuwa picha haziendi baada ya Wema kumtuhumu Penny ambaye alikuwa rafiki yake kuwa alimwibia Diamond wake kabla hawajamwagana na kurejea tena mikononi mwake

Tuesday, June 10, 2014

SOMA ALICHOSEMA PROF J BAADA YA DIAMOND KUKOSA TUZO

Msanii mkongwe wa Hip Hop Proffesor Jay amesema kuwa kushindwa kwa Diamond kuchukuwa tuzo za MTV kusimvunje moyo kwakuwa alikuwa anashindana na wasanii wakubwa sana Africa.

Akizungumza na mtandao huu leo ,Proffesor Jay amesema kuwa nafasi aliyopata Diamond na kushindana na wasanii hayo ni ushindi mkubwa wake.
“Diamond lazima ajue katika mashindano kuna kushinda na kushindwa, Kitu ambacho ninaweza kumwambia Diamond asikate tamaa, ameshindanishwa na wasanii wakubwa sana ambao pia ni advantage kwake ,msanii kama Davido pamoja na kufanya muziki mzuri tutambue kuwa nyuma yake kuna Wanageria zaidi ya milioni 150, ambao kiukweli wenzetu wameamka sana kuchangia kuwa support wasanii wao, sisi Watanzania tumekuwa tunazungumza kwa maneno mengi kulipo vitendo ,so mtu kama Davido ameshinda kwa kupigiwa kura na watu wake wengi na muziki wake umefika afrika nzima. Kwaiyo kushindwa kwake Diamond asichukulie kukata tamaa ,yeye achukulie kama changamoto na kuwashawishi Watanzania na mashabiki wake kuendelea ku support muziki wake ili afike mbali zaidi, naamini kuna kila dalili kwa Diamond kuendelea kufanya vizuri zaidi hapo mbeleni, pia nataka niwaambie Watanzania kwamba mtu anapoiwakilisha Tanzania tujitaidi kuweka tofauti zetu nyuma na kum,support wasanii wetu kwa sababu ushindi wake ni mafanikio makubwa ya muziki wetu,wasanii na wetu, na taifa kwa ujumla” Alisema Proffesor Jay.

Katika hatua nyingine Proffesor Jay amesema kuwa kesho anaingia mzigoni kuanza kushoot video ya ‘Kipi Sijasikia’ “Kesho naanza ku,shoot video ya Kipi Sijasikia, kilichotokea nilikuwa namsubiri tu Diamond, kwa sababu ratiba yake ilikuwa imebana sana, kila kitu sasa hivi kipo set, na tunafanya na Adam Juma, kilichotufanya tu delay kidogo ni kwa sababu alikuwa ameagiza Red na vitu vingine, kwaiyo vikawa vimechelewa kidogo lakini baada ya kuingia vyombo vyake, kesho tunaanza lakini ataujajua tutamaliza lini.Adam amenivutia sana sasa hivi kwa sababu ya kubadilisha kamera , Adam ana skills kubwa ya kutumia kamera , lakini kamera ambazo alikuwa akitumia mwanzo zilikuwa zinambana kidogo lakini sasa hivi kwa kuleta kamera hiyo Red na vitu vingine kama hivyo tunategemea uwezo wake anaweza akaonyesha kwa mapana zaidi , na pia tumejaribu tunatumia advantage ya Diamond huko anakozunguka kujaribu kufanya connection, kwa sababu Diamond anaweza kusaidia muziki wetu kifika mbali zaidi”Alisema Proffesor.

MWANAMKE ALIYEFANYA MAPENZI NA SAMAKI AINA YA DOLPHIN AONGEA KWA MARA YA KWANZA.

mager
Unaweza kushangaa na kuona ni kitu cha ajabu lakini hii imetokea ambapo mwanamke ambaye alifanya mapenzi na samaki aina ya Dolphin ikiwa ni sehemu ya utafiti wa kisayansi amezungumza kwa mara ya kwanza juu ya hatua hiyo.
Mwanamke huyo Margaret Howe Lovatt ambaye ni mtafiti wa wanyama amesema alikuwa sehemu ya utafiti huo uliofanyika katika kisiwa cha Virgin nchini Marekani kwa ajili ya kuwafundisha viumbe wa baharini wenye akili jinsi ya kuongea kiingereza.
Margaret Lovatt Howe
Margaret Howe Lovatt anasema alikuwa akijaribu kumfundisha Peter (the dolphin) jinsi ya kuongea kiingereza lakini uhusiano wao ulikwenda mbali zaidi.
Ilikuwa mnano wa mwaka 1963 ambapo walimsaidia kutengeneza bwawa la Dolphin nyumbani kwake ambako wanasayansi wangeweza kuwasoma wanyama hao wakiwa nyumbani, ndipo hapo Margaret alipokuna na Peter ambaye ni samaki aina ya Dolphin kwa wakati huo akiwa bado mdogo ambapo wawili hao wakapatana na mahusiano yao kukua zaidi kimwili.
Margaret amenukuliwa akisema kuwa “Peter (Dolphin) alipenda kuwa na mimi, mara nyingi alikuwa akijisogeza mwenyewe karibu yangu kwenye mguu wangu au mkono na kuruhusu kitendo hicho.”
dolphin
Anaendelea kusema kuwa “Haikuwa shida kwangu kwani Peter alikuwa akihisi uwepo wangu na kuona ni kitendo cha kimapenzi kwa upande wake lakini kwangu niliona ni kitu cha kawaida kama sehemu ya masomo yangu.”

Monday, June 02, 2014

EMMANUEL MBASHA AJITOKEZA, AFICHUA SIRI.

Credit:JestinaGeorge


Kabla ya kufunguliwa kwa faili la tuhuma hizo, msichana huyo alipelekwa Hospitali ya Rufaa ya Wilaya ya Ilala (Amana) ambako alifunguliwa faili la matibabu namba 667. Matokeo ya vipimo ambavyo vilifanywa na daktari kung’amua kama binti huyo aliingiliwa vinaonyesha kuwa kulikuwa na mbegu utokaji wa mbegu usio wa kawaida (HVD).
Dar es Salaam. Emmanuel Mbasha, ambaye ni mume wa mwimbaji nguli wa nyimbo za Injili, Flora Mbasha amejitokeza hadharani na kusema kwamba atakwenda polisi mwenyewe kujibu tuhuma dhidi yake za kumbaka shemeji yake mwenye umri wa miaka 17.

Faili la tuhuma dhidi ya Mbasha lilifunguliwa Jumatatu iliyopita katika Kituo cha Polisi Tabata (Tabata Shule) wakati shemejiye huyo (jina tunalihifadhi), alipotaarifu kuwa Mbasha alimbaka mara tatu kwa siku mbili tofauti. Kesi hiyo ilipewa namba TBT/RB/3191/2014 na TBT/IR/1865/2014.

Tangu siku hiyo, polisi imekuwa ikieleza kuwa inamsaka Mbasha bila ya mafanikio lakini mwishoni mwa wiki mtuhumiwa huyo aliongea na gazeti hili na kuelezea upande wake wa tukio hilo na kwamba yuko tayari kujisalimisha ili ukweli ubainike.

“Tuhuma dhidi yangu ni za kutengeneza,” alisema Mbasha na kufafanua kuwa yote hayo yanatokana na mgogoro wa kifamilia baina yake na Flora na familia yake ambao alisema umedumu kwa siku kadhaa.

“Mimi sijabaka na sijawahi kubaka; sijatenda dhambi yoyote; sijafanya kitu chochote na kibaya haya mambo yote ni ya kusingiziwa tu. Mungu wangu ni shahidi. Na kwa kuwa sijafanya hiyo dhambi kama wanavyodai, basi Mungu wangu atanitetea,” alisema Mbasha ambaye anaonekana zaidi kwenye video ya wimbo wa Maisha ya Ndoa alioshirikiana na mkewe Flora.

“Si wamesema wananitafuta, nitakwenda mwenyewe polisi. Nitawasikiliza na nitatoa maelezo yangu. Kama wakinipeleka mahakamani basi ukweli utajulikana... ipo siku kila kitu kitakuwa wazi.”

Kabla ya kufunguliwa kwa faili la tuhuma hizo, msichana huyo alipelekwa Hospitali ya Rufaa ya Wilaya ya Ilala (Amana) ambako alifunguliwa faili la matibabu namba 667. Matokeo ya vipimo ambavyo vilifanywa na daktari kung’amua kama binti huyo aliingiliwa vinaonyesha kuwa kulikuwa na mbegu utokaji wa mbegu usio wa kawaida (HVD).

 Kadhalika binti huyo alifanyiwa vipimo kuona kama ameambukizwa virusi vya Ukimwi (VVU), pia kupata ujauzito, lakini matokeo ya awali yalionyesha kuwa yupo salama.

Akiwa nje ya kituo cha polisi Jumatatu usiku, binti huyo aliliambia gazeti hili kwamba mara ya kwanza alibakwa mchana Mei 23 na kwamba mtuhumiwa alirudia kitendo hicho Jumapili Mei 25 usiku ndani ya gari katika eneo la Tabata, ambako anadai alifanyiwa kitendo hicho mara mbili.

Hata hivyo, Mbasha alihoji: “Hivi kweli hata kama mimi ni mbakaji, kweli nimbake mtoto wa kumlea mwenyewe mara tatu, yaani Ijumaa halafu nirudie tena Jumapili? Hata kama ni kusingiziwa basi tuhuma hizi zimezidi.”

“Huyu binti nimekaa naye miaka mingi na sijawahi kumfanyia hivyo. Hapo nyumbani kwangu wamekaa mabinti wengi, wakiwamo shemeji zangu wadogo zake na Flora na sikuwahi hata kuwagusa, leo hii kwa nini wananifanyia hivi?”

Mgogoro wa familia

Mbasha alidai kwamba chanzo cha kusingiziwa kwake ni mgogoro baina yake na mkewe Flora, ambao umesababisha mgawanyiko mkubwa ambao umefanya achukiwe na familia nzima ya mkewe.

“Yako mambo mengi tu ambayo yanahusu familia, kwa hiyo ilifika mahali mimi na Flora tukawa hatuishi kwa amani na hata hili jambo limetokea wakati tukiwa na mgogoro huo. Hivyo Flora na ndugu zake waliamua kumlisha binti huyo maneno ili mimi nifungwe,” alisema Mbasha.

Hata hivyo, Flora hakutaka kuingia kwa undani katika suala hilo, akisisitiza kuwa Mbasha bado ni mumewe na kwamba yaliyotokea awali alishamsamehe, lakini akamtaka ajitokeze kutoa maelezo polisi.

“Mimi nilishamwambia kwamba hata kama alifanya au hakufanya, nilishamsamehe kutoka ndani ya moyo wangu maana yeye ni mume wangu wa ndoa na Mungu wangu ni shahidi, lakini kuna suala la kisheria polisi ambalo mimi siwezi kuliingilia,” alisema Flora ambaye alitamba na wimbo wa injili wa “Tanzania” ambao ulimfanya aalikwe katika shughuli mbalimba za kitaifa.

“Tatizo linakuwa kubwa kwa sababu yeye mwenyewe haonekani na taarifa ni kwamba amekimbia,” alidai Flora. “Sasa kama kweli hajafanya kitendo hicho, kwa nini anajificha? Ajitokeze... aende polisi na huko ndiko akatoe maelezo yake. Kuzungumza na vyombo vya habari haisaidii kabisa.”

Mwimbaji huyo, ambaye ni mjukuuu wa muhibiri maarufu wa Injili, Askofu Moses Kulola alisema yeye hana uwezo wa kuingilia kesi hiyo kwani hakuhusika kwa namna yoyote ile kupeleka suala hilo polisi kwa sababu hakuwapo wakati likitokea na kwamba linasimamiwa na familia.

“Inawezekana anatamani nikafute kesi polisi, mimi sina uwezo huo kwa sababu ni suala la kisheria na tuhuma zenyewe ni za kijinai. Pili familia yenye mtoto ndiyo inafuatilia kesi hiyo, lakini hilo halifuti msamaha wangu kwake,” alisisitiza.

 Kauli ya Flora kwamba ameshamsamehe mumewe inafanana na ya Mbasha ambaye pia alisema kwamba kama kuna jambo ambalo mkewe alimkosea, hana tatizo na kwamba alishamsamehe.

 “Flora ni mke wangu, mke wa ujana wangu, ninampenda asilimia 100 na yeye analifahamu hilo, lakini sijui ni kitu gani kimemkuta? Sijui ni nini kimeingilia ndoa yetu?” alisema Mbasha.

Alisema ameshampigia simu mkewe mara nne akitaka waonane ili wazungumze, lakini hakuonyesha utayari, kauli ambayo Flora aliikanusha akisema: “Hajanitafuta maana tangu Jumatatu hapatikani kwenye simu.”


Mwenendo wa upelelezi

Wakati hayo yakiendelea, maendeleon ya kesi hiyo yanasuasua baada ya faili kutokupelekwa Kituo cha Polisi Buguruni kutoka Tabata kwa ajili ya hatua zaidi.

Baadhi ya wanafamilia wa mtoto anayedaiwa kubakwa walisema jalada hilo lingefikishwa Buguruni Jumatano jioni, lakini kutokana na ofisa anayeshughulikia kesi hiyo kuwa na udhuru, ilishindikana.

Mjomba wa Flora ambaye amepewa jukumu la kusimamia kesi hiyo, alisema wamekuwa wakifuatilia Kituo cha Polisi cha Tabata tangu tukio hilo liliporipotiwa, lakini wakaelezwa kuwa kesi hiyo itahamishiwa Buguruni.

“Tuliambiwa lile faili lazima lihamie kituo cha Buguruni. Nilifika hapa nikaonana na kamanda wa polisi wa wilaya ambaye ametupokea vizuri na kuonyesha moyo wa kutusaidia,” alisema.

Kamanda wa polisi wa Ilala, Marietha Minangi alisema bado wanaendelea na uchunguzi wa kesi hiyo na kwamba hafahamu taarifa kuwa faili hilo linacheleweshwa kuhamishiwa Buguruni. “Tunaendelea kuchunguza, ila siyajui hayo masuala ya faili yanayotoka kinywani mwako. Lakini nimepata taarifa kuwa bado wanachunguza,” alisema Minangi.

Mwanzoni mwa wiki jana, Kamanda Minangi alisema kuwa maofisa wake walikuwa wanaendelea kumsaka mtuhumiwa na kwamba walienda mpaka nyumbani kwake, lakini hawakumkuta.

“Nimefuatilia ni kweli hiyo kesi imefunguliwa na maofisa wangu wameniambia walienda nyumbani kwake na hawakumkuta mtu. Waliniambia walikaa pale kwa takribani dakika 20 na ile nyumba ina fence (uzio) na geti waligonga kengele, lakini hakuna mtu aliyekuja kufungua.

“Na baadaye waliwauliza majirani, nao wakasema hawafahamu mtu huyo alipo. Inaonekana ametoweka, lakini sisi kama wasimamizi wa sheria tunaendelea kumtafuta mpaka tutakapomkamata,” alisema Minangi.

Ustawi wa Jamii

Kesi hiyo pia inafuatiliwa kwa karibu na Idara ya Ustawi wa Jamii ya Manispaa ya Ilala kujua usalama na matibabu ya binti huyo. Ofisa ustawi wa jamii anayeshughulikia ulinzi na usalama kwa mtoto wa manispaa hiyo, Fransica Makoye alisema kuwa wanalishughulikia suala hilo kama mengine katika kutafuta haki na usalama wa mtoto na wala hawahusishi na umaarufu wa wahusika.

“Sisi tunafuatilia kama alipata tiba sahihi mara baada ya tukio la kubakwa na kufahamu mahali ambako anakaa kwa ajili ya usalama wa huyo mtoto. Tumeiona PF3 haionyeshi kama alipata matibabu, lakini tutawajulisha zaidi kinachojiri kwa kuwa tutaenda Hospitali ya Amana kwa maelezo zaidi,” alisema Makoye.

Sunday, June 01, 2014

DIAMOND NDANI YA WASHINGTON, DC, APIGA PICHA NA MASHABI WAKE, LEO KUFANYA SHOW NEW JERSEY

credit:jestinagrorge blog


 Diamond Plutnumz akiongozana na wasafi pamoja na Dj Romy Jons (Dj wake) kulia wakiwa na mwenyeji wao DMK wakiwasili tayari kukutana na mashabiki wake waliofika kwenye mgahawa wa Safari, Washington, DC kumsubili na kupiga nae picha.
  Diamond Plutnumz akiwa ndani ya mgahawa wa Safari na kruu wake katika picha na mashbiki waliofika kumsabai na kupiga nae picha.
 Mashabiki wa Diamond wakipata ukodak moment na Diamond Plutnumz mara tu alipotua ndani ya mgahawa wa Safari siku ya Ijumaa May 30, 2014.
 Shabiki akiwa bado na kiu ya kupata ukodak na Rais wa Wasfai, Diamond kulia ni DMK poromota wa msanii huyo ambaye ndie anayekimbiza sasa hivi na akiwa nominee wa MTV africa na BET award itakayofanyika nchini Marekani June 29, 2014.
 Diamond akiongea jambo na Mkuu wa Utawala na Fedha Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani, Mama Lily Munanka
 Mashabiki wa Diamond Plutnumza wakipata picha ya pamoja na Rais wa Wasafi.
 Mashabiki kutoka jirani zetu Kenya nao wakipata picha na Prezidaa Diamond Plutnumz walipofika kwenye mgahawa wa Safari uliopo Washington, DC.
 Madancer wa Diamond wakiwa na Prezdaa ndani ya mgahawa wa Safari Washington, DC.
 Mtasha wa Kimarekani aliyewahi tembelea Tanzania nae hakuwa nyuma kupata picha na Diamond ndani ya mgahawa wa Safari ulipo Washington, DC
 Shabiki akiwa na furaha kupata ukodak na Rais wa Wasafi Diamond Plutnumz
 Diamond akiwa na shabiki wake katika picha ya pamoja.
Shabiki wa Diamond hakuwa nyuma katika kupata ukodak wa kumbukumbu.
 Shabiki wa Diamond akipata picha ya pamoja na Prezedaa wa Wasafi.
 Shabiki kutoka kwa jirani zetu nae akipata picha huku akijaribu kupata picha kwenye simu yake.
 Dj Romy Jons akipata picha ya pamoja na mashabiki kwenye mgahawa wa Safari uliopo Washington, DC.
 Shabiki katika picha ya pamoja na Diamond.
 Shabiki na Diamond katika picha ya pamoja.
 Shabiki akipozi kwa picha na Diamond.
Shabiki akipozi kwa ukodak moment na Diamond.
 Shabiki wa Diamond akipata picha na rais huyo wa Wasafi.
 Shabiki akipata picha na Dj wa Diamond, Dj Romy Jons
Shabiki akipata picha na Wasafi.
Mashabiki katika picha ya pamoja na poromota wa Diamond, DMK.

Picha zote na vijimambo blog

AMBWENE YESSAYA aka "AY" AMNUNULIA JENEZA MAREHEMU TYSON

credit: Jestinageorge blog


Msanii wa Hip Hop nchini, Ambwene Yessaya 'AY' (anayehesabu pesa) aliamua kujitole kununua jeneza la kusafirishia mwili w marehemu, jeneza hilo liligharimu kiasi cha shilingi laki sita ambazo AY alizitoa cash!
wakisaidiana kubeba jeneza hilo kuelekea hospitalini baada ya kulinunua
Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania, Simon Mwakifamba (mbele), akiongozana na AY kuelekea hospitalini
Mtangazaji wa kipindi cha Mboni Show, Mboni Masimba akilia kwa uchungu akiwa nje ya Hospitali ya Mkoa wa Morogoro wakati wakisubiri kusafirisha maiti kuelekea Dar. Marehemu Tyson ndiye alikuwa Mtayarishaji wa kipindi chake na walikuwa wote katika safari hiyo, ingawa walikuwa magari tofauti.
Mboni (kushoto) akiwa na Mtangazaji wa ITV, Devota Minja
Mboni akifarijiwa Mkuu wa Wilaya ya Mvomero, Anthony Mtaka.
(PICHA: Dastun Shekidele/GPL Morogoro)