Thursday, January 03, 2013

HATIMAYE FAMILIA YA SAJUKI YARIDHIA MAREHEMU KUZIKWA DAR SIKU YA IJUMAA

Taarifa ambazo zimeridhiwa na maamuzi ya familia na ndugu wa karibu, zinasema marehemu Juma Kilowoko aka Sajuki atazikwa siku ya ijumaa katika makaburi ya Kisutu.

Taarifa ambazo pia zimetoka kwa msemaji wa Bongo Movie na wahusika wa maandalizi ya mazishi hayo, wanasema ndugu wa Sajuki wameridhia marehemu kuzikwa hapa na sio Songea kama wengine wanavyotangaza. Kuhusu kusogeza mpaka ijumaa, msemaji huyo akasema, ni kutokana na kusubiri ndugu wa marehemu wanaotoka sehemu mbali mbali kuja Dar kwa ajili ya mazishi hayo, wengi wakitokea Songea.

Sajuki ambae alifariki usiku wa kuamkia tarehe 2, atazikwa siku ya ijumaa ya tarehe 4 katika makaburi ya Kisutu, ambapo mazishi hayo yataanza muda wa saa 5 asubuhi.

Mungu ailaze roho ya marehemu Juma Kilowoko (Sajuki) mahala pema peponi, Amen

BREAKING NEWS: SAJUKI AFARIKI DUNIA LEO ALFAJIRI

 
Breaking News:Msanii Juma Kilowoko (SAJUKI)amefariki dunia leo alfajiri katika hospitali ya Taifa Muhimbili.Kwa mujibu wa Katibu wa chama cha waongoza Filamu Wilaya ya Ilala,Rajabu Amiri hivi karibuni Sajuki alikuwa anasumbuliwa na tatizo la upungufu wa damu
Alilazwa hapo kwa wiki mbili ambapo alikua anasubiri kupata urahisi wa kusafiri kurudi India kwenye matibabu ambayo alipangiwa kurudi tena december 2012. 
Dinno ambae ni rafiki wa karibu wa Sajuki amesema kwamba tatizo kubwa lililomzuia Sajuki kurudi India ni pumzi ambapo walikua wanatafuta ndege yenye huduma ya gesi.

Baada ya kuhangaika sana, dakika za mwisho ndio walikua wamepata ndege ambayo imekubali kutoa huduma ya gesi kwa Sajuki ambapo Shirika la ndege la Emirates ndio lilikua limekubali kutoa huduma hiyo.

Msiba upo Tabata, Mwenyenzi Mungu amlaze pema Sajuki.