Thursday, August 14, 2014

MASHAUZI MAPYA YA JINI KABULA

MWIGIZAJI wa sinema za Kibongo, Miriam Jolwa ‘Jini Kabula’ amefunguka kuwa licha ya penzi lake na msanii Maximilian Bushoke kuwa na sarakasi nyingi lakini anaamini atamuoa.

Mwigizaji wa sinema za Kibongo, Miriam Jolwa ‘Jini Kabula’
Akizungumza na paparazi wetu, Jini alisema watu wengi wamekuwa wakiuponda uhusiano wake kwa kuwa Bushoke anaishi Afrika Kusini na kuona hakuna mapenzi ya kweli lakini ukweli anaoujua yeye ndoa ipo.
Msanii wa Bongo Fleva Maximilian Bushoke.

“Piga ua garagaza, Bushoke ndiye mwanaume ambaye anajua kunipa tiba nzuri ya mapenzi, hakuna mwingine, atanioa tu kwa sababu sioni kipingamizi,” alisema Jini Kabula.
GPL

MARTIN KADINDA AJIBU MASHABIKI WA WEMA BAADA YA KUULIZWA KAMA AMESHINDWA KAZI YA UMENEJA MAANA WEMA ANASHUKA.


Wema akiwa na Meneja wake Martin Kadinda
Ok hapo juu ndo ujumbe alioandikiwa Meneja wa mrembo Wema Sepetu anaeitw @mrekebishatabia. Maswali mengi yamekuja baada ya Wema kufanya show Mwanza mpenzi wake alipokuwa akiperform jukwaani, pamoja na hayo mashabiki waliyo wengi wametaka kuona Wema akijishughulisha kuliko hivyo anvyo zunguka na hawajui anafanya nini. Wema ana mashabiki wengi sana wanaompenda na kutaka mafanikio yake. Baada ya swali hilo hapa chini ndo jibu alilitoa kaka Meneja wa Wema amejielezea vizuri sana.