Thursday, May 02, 2013

WAASI WA M23 WAISOGELEA KAMBI YA MONUSO HUKO DRC


Baadhi ya askari wa kundi la M2

RUTSHURU-DRC,Ujumbe wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa huko Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, Monusco umesema kuwa waasi wa Kundi la M23 wamesogeza mbele Ngome yao kwenye mita 30 karibu na makao makuu yao Huko Kiwanja mtaani Rutshuru.

Katika hatua nyingine msemaji wa Monusco Felix Prosper Bass anasema zaidi ya wapiganaji 65 kutoka kundi hilo la M23 wamejisalimisha na hivyo kupokelewa kwenye Tume hiyo na kwamba hilo linaweza kuwa ndiyo sababu ya wao kusogeza ngome yao.
Kwa upande wake kiongozi wa Kundi la M23, Betrand Bisimwa amesema kuwa Hizo ni propaganda za serikali ya Kinshasa ikiwa imeshirikiana na Monusco katika kudhihirisha nia yao ya kutaka kuanza mapigano.
Nayo Mashirika ya Kiraia katika Jimbo la Kivu ya kaskazini kupitia naibu mwenyekiti na msemaji wa mashirika hayo, Omari Kavota pia yamethibitisha taarifa hiyo na kusema kuwa kundi hilo la M23 limeweka vizuizi katika maeneo kadhaa huko mashariki mwa Kongo.
Hatua iliyochukuliwa na kundi la M23 inaelezwa kuongeza wasiwasi miongoni mwa raia huko Mashariki mwa DRC pamoja na kuzorota kwa hali ya amani.
Hayo yanatokea wakati Umoja wa Mataifa ukiendelea na maandalizi ya kupeleka kikosi maalum cha kimataifa kitakachojumuisha wanajeshi kutoka Tanzania, Malawi na Afrika Kusini.

Kocha wa Bayern Munich atamba kutwaa ubingwa Klab Bingwa Ulaya.


wachezaji waBayern Munich katika moja ya mechi zao.

BAYERN MUNICH-UJERUMANI,Kocha wa Klabu ya Bayern Munich Jupp Heynckes amesema kuwa kipigo walichokipata katika mechi ya fainali ya klabu bingwa Ulaya msimu uliopita kutoka kwa Chelsea utachochea timu yake kupata ushindi katika mchezo wa fainali ya mwaka huu itakapokwana na Borussia Dortmund.

Bayern Munich itakutana na Borussia Dortmund baada ya hiyo jana kuilamba kwa jumla ya bao 7-0 katika michezo yote miwili nyumbani na ugenini Barcelona ya Hispania.
Kocha huyo amesema kuwa kuna mengi ya kujifunza katika ushindi na kushindwa na ana matumaini kuwa vijana wake watatumia uzoefu wa kushindwa katika fainali za mwaka jana na Chelsea ili kutwaa ubingwa wa mwaka huu.
Timu yoyote kati ya timu hizo mbili itakayoshinda itakua ni mara ya kwanza kwa timu ya Ujerumani kutwaa ubingwa huo tangu mwaka 2001 pale Bayern Munich ilipotwaa Ubingwa wa Klabu Bingwa Ulaya.