Monday, July 21, 2014

DIAMOND AMVISHA TENA PETE YA UCHUMBA WEMA SEPETU...JIONEE MWENYEWE HAPA.


Beautiful Onyinye, Wema Isaac Sepetu (25) akionyesha pete aliyovishwa na Diamond.

Wema Isaac Sepetu (25) ameibua viulizo baada ya kuonekana akirandaranda na pete ya ndoa kidoleni ikidaiwa kuwa amevalishwa na Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ kwa siri kubwa, Ijumaa Wikienda lina stori exclusive.

Baada ya kuwepo kwa habari nyingi kuhusiana na ishu hiyo, Ijumaa Wikienda liliingia mzigoni kusaka ukweli wa ishu hiyo na kujua mbivu na mbichi.

Kwa mujibu wa rafiki wa karibu wa mkali huyo wa sinema za Kibongo, hata mashosti zake hawajui kinachoendelea zaidi ya kuulizana wao kwa wao kuhusu nini kinaendelea huku kukiwa na hisia kuwa huenda wawili hao wamefunga ndoa ya siri.
 
Muonekano wa karibu zaidi wa pete hiyo katika kidole cha Wema.

 ALISHAMVISHA YA UCHUMBA
Kuna maelezo kwamba Diamond alifanya hivyo ili kuzuia mwanaume mwingine kumvisha Wema pete ya ndoa kwani alishamvisha ya uchumba tangu mwaka 2011 kwenye Ukumbi wa New Maisha ulipo Masaki jijini Dar.
WEMA LAIVU
Wiki iliyopita jitihada za kumnasa Wema akiwa na pete ya uchumba zilizaa matunda ambapo mwanahabari wetu alimuweka ‘mtukati.

Saturday, July 19, 2014

WEMA SEPETU AMLIPUA KAJALA, KISA UNAFIKI



Wema Isaac Sepetu (25), amemlipua aliyekuwa shosti wake, Kajala Masanja ‘K’ ambaye wiki iliyopita alimwita mnafiki, habari  ambayo  ilisambaa  katika  mitandao  mbalimbali  ya  kijamii.
 
Katika habari hiyo, Kajala alikaririwa akisema kwamba licha ya watu wengi kuamini wamepatana, hakuna ukweli kwani rafiki yake huyo ni mnafiki kufuatia kutomthamini na kutokuwa karibu naye kama zamani likiwemo suala la kumsifia mtu ambaye alikuwa na ugomvi na Kajala (Dacutee).

Akizungumza na mwanahabari wetu, Wema alisema alishangaa kuona Kajala anamwita mnafiki wakati hakuwahi kupatana naye tangu walipotofautiana kipindi cha nyuma kama alivyosema.
 
“Nashangaa Kajala ananiambia mimi ni mnafiki ‘ok fine’ na huo unafiki wangu unakuja pale nilipomu-wish Dacutee siku yake ya kuzaliwa, alitakaje eti? Yaani kwa kuwa yeye ana bifu la kumchukulia bwana’ke na mimi nijiingize kwenye bifu lao?
 
“Au tofauti zangu mimi na yeye, Aunty Ezekiel aingilie, itakuwa sahihi kweli kama wanavyofanya hao watu wake anaozurura nao siku hizi? Wanaingilia vitu ambavyo hawavijui kiundani wake? Nasema siyo sahihi kabisa mimi nitabaki kama Wema Sepetu na yeye atabaki kama Kajala Masanja na asifikirie kuwa nitakuja kuwa kama zamani na yeye halafu kama anamaindi kuhusiana na Dacutee mbona Petit Man ambaye ana uhusiano naye aliweka picha ya Dacutee na kumu-wish hajammaindi?” aliwaka Wema.
 
Akiendelea kutema cheche, Wema alisema anachopaswa kuzungumza Kajala ni ukweli wa matatizo yao na siyo kusingizia watu wengine.
 
“Mbona siku ile niliwahadithia kila kitu (waandishi) kuhusiana na tatizo letu, si nimetoa kinyongo changu ambacho nilikuwa nacho siku nyingi hivi sasa najiona mwepesi na kama na yeye anataka kusafisha moyo wake anatakiwa afunguke, kuanzia leo nataka niseme sitaki kusikia na kuulizwa suala la mimi na Kajala kwani nimechoka na nina mambo mengi ya kufanya,” alisema Wema.
 
Akizungumzia ishu ya kukutana na Kajala na kupiga picha za pamoja wakiserebuka hivi karibuni, Wema alisema alifanya vile kuonesha kwamba hana kinyongo na ndiyo maana alivyoombwa apige picha na Kajala, hakusita kufanya hivyo.
 
“Mimi ni mtoto wa Kiislamu na nina imani na upendo kwa kila mtu, siwezi nikamkatisha mtu furaha yake na ndivyo ilivyotokea, niliombwa nipige picha ya pamoja na Kajala siku ile ya shughuli na nilifanya hivyo baada ya pale nikaenda zangu kulala,” alimalizia kusema Wema.
 
Bifu la mastaa hao wakali wa Bongo Movies liliibuka baada ya Wema kumtuhumu Kajala kuwa ametembea na aliyekuwa bwana’ke, kigogo aliyetajwa kwa jina la CK.

MSANII ELIZABETH 'LULU' MICHAEL AFUTURU NA WATOTO YATIMA SINZA [PICHA].



Msanii wa maigizo Elizabeth Diana Michael aka Lulu jana jioni aliwakumbuka watoto yatima wa kituo cha ''Chakuwama'' kilichopo Sinza Meeda na kujumuika nao kwenye #Futari iliyo andaliwa na msanii huyo.. Lulu aliambatana na Mama yake mzazi, Mama Kanumba, Dk. Cheni na watu mbali mbali... Mlezi mkuu wa kituo hicho Bi Saida Hassan amesema wamefarijika sana kuona Lulu amewakumbuka.
Watoto wakipakua futari 
Mama Kanumba nae alikuwepo 
 Dr Cheni akipata futari
 Lulu akiwa na mmoja wapo wa mtoto wa kituo hicho

 Lulu na mama Kanumba wakiteta jambo
 Lulu na mdogo wake Eric
 Lulu akikabidhi msaada


Mama mlezi wa watoto hao Bi. Saida Hassan akizungumza na Lulu. Picha kwa hisani ya Bestizzo

Friday, July 18, 2014

MKUTANO WA KUJADILI MASUALA YA KODI AFRIKA WAFANYIKA JIJINI ARUSHA



 Waziri wa fedha Saada mkuya akijadiliana jambo na rais wa kituo cha kimataifa cha ukusanyaji kodi na uwekezaji Daniel Witt wakati wa mkutano wa siku 3 wa majadiliano ya masuala ya kodi Afrika uliofanyika jijini Arusha jana katika hotel ya naura spring.
mkurugenzi mkuu wa TRA Rished Bade akizungumza wakati wa ufunguzi wa  mkutano wa siku 3 wa majadiliano ya masuala ya kodi Afrika uliofanyika jijini Arusha jana


 Picha ya pamoja
 vuiongozi wa kuu
 Waziri Saada Mkuya akihojiwa na wanahabari.

waziri wa fedha Saada Mkuya katikati  akiwa na mkurugenzi mkuu wa TRA kulia Rished Bade na kushoto dr.Jeffrey Owens mtaalam msahuri wa kodi na mhadhiri chuo kikuu cha uchumi na biashara Viena mara baada ya waziri kufungua mkutano wa majadiliano ya masuala ya kodi unaofanyika jijini Arusha

SUPER STAR DIAMOND PLATZNUMZ ANA LAAANA YA BABA YAKE SOMA HABARI KAMILI HAPA


Wakati akimpa mama yake, Sanura Kassim ‘Sandra’ gari la Sh. milioni 38 huku akitawanya mamilioni ya fedha kwenye matukio mbalimbali, staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ anadaiwa kunyemelewa na laana kufuatia baba yake, Abdul Jumaa kuugua na kuvimba miguu bila msaada wowote.
Kwa mujibu wa chanzo makini cha Ijumaa, baba wa staa huyo anayeishi Magomeni-Kagera jijini Dar, amekuwa akisumbuliwa na tatizo la kuvimba miguu na hakuna msaada wowote anaoupata kwani chanzo cha mapato anachokitegemea ni kodi tu ya nyumba ambayo anaipata kutoka kwa wapangaji wachache alionao.



BOFYA HAPA

“Yaani tunashangaa kusikia Diamond ana fedha nyingi, juzikati tuliona katika gazeti kamnunulia mama yake gari la milioni 38 (Toyota Lexus-Harrier) sasa kwa nini asimthamini baba yake hata kidogo? 

“Ukweli ni kwamba baba Diamond anasumbuliwa na tatizo la miguu kuvimba.



“Amekuwa akilalamika mara kwa mara lakini Diamond hatujawahi kumuona,” kilinyetisha chanzo hicho na kuongeza:“Juzikati hapa baba Diamond alishikika kwelikweli miguu, akaugulia mwenyewe ndani pasipo kuwa na msaada wowote tena nasikia mzee huyo hataki hata kuongelea lolote kuhusu Diamond maana haoni umuhimu wa kufanya hivyo wakati amemsusa muda mrefu sana.”



MATIBABU HAYAZIDI MILIONI

Katika aya nyingine, chanzo hicho kilidai kwamba ugonjwa wa miguu ambao unamsumbua mzazi huyo, gharama za matibabu haziwezi kufikia hata shilingi milioni moja za madafu achilia mbali mamilioni anayoyatapanya staa huyo.

Mama yake Diamond,Sanura Kassim ‘Sandra’ akilitesti gari alilokabiziwa na Mwanaye kama zawadi.



“Ingekuwa tatizo kubwa sana, hapo sawa, kwa sababu miguu huwa inamvimba lakini akipata dawa za kutumia huwa inarudi katika hali ya kawaida, kwa nini lakini anamfanyia hivyo baba yake? Amemkosea nini?” Kilihoji chanzo hicho.



UTAJIRI WAKE WAANIKWA

Wakati chanzo hicho kikiweka nukta hapo kwa muda, mapaparazi wetu walipewa malalamiko mengine kutoka kwa jirani mmoja wa baba Diamond ambaye alimsihi amsaidie mzazi wake kwani anaamini uwezo anao kupitia kumbukumbu ambazo Diamond mwenyewe alizithibitisha kupitia vipindi mbalimbali vya runingani kama Take One na Spora Show vya CloudsTV.



Pia kwenye vyombo vingine vya habari zikiwemo redio na magazeti pendwa ya Global Publishers.

Jirani huyo alidai kwamba mwaka jana Diamond alitangaza kuwa ana utajiri wa Sh. bilioni moja ikiaminika kwamba mwaka huu umeongezeka mara dufu.



“Nakumbuka mwaka jana kupitia Kipindi cha Spora Show na kile cha Take One, Diamond alikiri kuwa ana mkwanja usiopungua bilioni moja, hiyo ilikuwa kwa mwaka jana, sasa mwaka huu unadhani atakuwa na shilingi ngapi? Aache hizo bwana, amsaidie baba yake hata kwa kumpa mtaji mdogo wa biashara ambao unaweza kumsaidia,” alisema jirani huyo.



MATANUZI YA DIAMOND, WEMA

Katika kuendelea kuichimba habari hiyo, mapaparazi wetu walinasa malalamiko kutoka kwa jirani mwingine wa mzazi huyo ambaye alieleza masikitiko yake kwa kulinganisha starehe ambazo staa huyo anazifanya na asali wake wa moyo, Beautiful Onyinye, Wema Isaac Sepetu na maisha halisi ya baba yake.



“Mimi ni mfuatiliaji mzuri wa habari za mastaa, naona kila siku kwenye vyombo vya habari jinsi gani Wema na Diamond wanavyotumia fedha nyingi katika masuala ambayo hayana ulazima kiivyo.

“Sisi kama majirani hatupendezwi na hali hii, angekuwa anakuja angalau siku mojamoja kumuona baba yake kuliko kila siku kumhudumia mama yake pekee,” alisema jirani huyo.



Baba yake Diamond, Abdul Jumaa akitafakari jambo.



TATIZO NI NINI?

Mapaparazi wetu waliingia mzigoni kusaka kiini halisi kwa nini Diamond amwage fedha nyingi kwa mama yake pasipo kumkumbuka japo kiduchu baba yake ambapo ilielezwa kuwa staa huyo wa Mdogomdogo hakuwa na ugomvi wowote na mzazi wake huyo.



“Kama ni ugomvi ulikuwepo kati ya mama na baba lakini Diamond hahusiki, tunashangaa kuona kama staa huyo naye anaweza kumsusia baba yake,” kilieleza chanzo na kuongeza:



“Mbaya zaidi nasikia Diamond amekuwa mzito kupokea simu za baba yake, sasa huoni kama siyo jambo la busara, mzazi ni mzazi tu hata iweje. Kwa mtazamo wangu kinachofuata ni laana.



“Kuna mifano ya watu wengi ambao waliingia kwenye laana za wazazi wao na wakajikuta kama siyo kufulia kama (wanatajwa mastaa waliofulia wa muziki Bongo) au hata kukutwa na umauti.

“Jambo hili si la kibinadamu tu, kwa wale wanaosoma vitabu vitakatifu watakuwa na mifano mingi ya watu waliowakosea wazazi wao wakalaaniwa.”



BABA DIAMOND ANASIKITISHA

Ijumaa lilipomtafuta baba Diamond kwa njia ya simu aliongea maneno ya kusikitisha huku akikataa katakata kumzungumzia kijana wake huyo.



“Jamani naomba mumuache Diamond na maisha yake, sitaki kabisa kusikia habari zake maana hata nikiongea naonekana najipendekeza kwake.



“Namshukuru Mungu, kama ni kuumwa kwa sasa naendelea vizuri na maisha yangu, niacheni nipumzike,” alisema mzee huyo kwa unyonge.



DIAMOND ANASEMAJE?

Alipotafutwa Diamond ili kumsikia anazungumziaje madai hayo, simu yake iliita bila kupokelewa. Tunaamini atasoma habari hii hivyo si vibaya akatutafuta ili afunguke kwa upande wake.