Friday, September 05, 2014

MWANAMKE AKIKUJIBU SMS YAKO HIVI TAFADHALI SANA USIENDELEE KUCHAT NAE MAANA KINACHOFUATA HAPO NI MAJANGA TU.

Ukiona umemtumia mpenzi wako/mchumba wako/mchepuko wako/mke wako au hata rafiki wa kike wakati mwingine SMS ya kawaida tu kwaajili ya kumsalimia lakini yeye akakujibu moja kati ya majibu yafuatayo, tafadhali sana usiendelee kuchat nae maana kinachofuata hapo ni majanga tu.

KWA MFANO: 
1. Ukimtumia sms ''Mambo mpenzi wangu?'' akikujibu ''mambo mabaya'', usimuulize kwanini mambo mabaya, ukimuuliza atakwambia kuwa ''sina hela dear''

2. Ukimtumia sms ''Maisha yanasemaje kipenzi changu'' akikujibu ''maisha magumu hubby wangu we acha tu'' usimuulize kwanini, ukimuuliza kwanini atakwambia ''nimefulia mwenzio kama nini sijui''

3. Ukimtumia sms ''Mbona kimya sana mchumba wangu, umenitupa kiasi hicho'' akikujibu ''sijakutupa wangu yaani mambo hata hayaendi'' usimuulize kwanini mambo hayaendi, ukimuuliza atakwambia kuwa ''yaani sina kitu mpenzi wangu, simu ilikuwa haina hata hela ya kubeep''

4. Au ukiona mwanamke anaanza kwa kukwambia nikwambie kitu? We mkatalie kiutani utani tu, mwambie usiniambie, hata akikomaa vipi akwambie mwambie sitaki uniambie huku unafanya kama utani lakini moyoni unakuwa upo serious.

Ni mara chache sana mwanamke akikwambia kuwa mambo mabaya, maisha magumu au mambo hayaendi huwa na matatizo mengine kama kuumwa, misiba.... n.k lakini THE REST ni wapigaji mizinga tu. Akikwambia maisha magumu mjibu ''pole wangu, mambo mengine vipi?''

Ukipewa majibu kama hayo, chagua moja, either usiendelee kuchat nae mpaka badae kidogo au mbadilishie maada ili kukwepa huo mzinga ambao unakuja mbele yako. 

By Dr. MCHUNGUZI HURU

Monday, September 01, 2014

Pichaz za Feza Kessy, Shaa, Maua na Recho walivyotokelezea kwenye Fiesta ya Moshi.

4Feza Kessy ni miongoni mwa Wasanii waliokua wanasubiriwa kwenye stage ya Serengeti Fiesta 2014 hapa Moshi show iliyofanyika August 30 ambapo staa huyu alieiwakilisha Tanzania kwenye BBA 2013, alipanda kwenye stage na dancers wake watatu wa kiume.
Waimbaji wengine wa kike waliochukua mic kwenye stage ni pamoja na Shaa, Maua na Recho.
5
6
35
Shaa kazini
34
33
32
31
30
29
8
Maua
7
16
Recho
17
18
19