Sunday, July 22, 2012

MAREKANI KUZIPATIA KENYA ,BURUNDI, UGANDA NA DJIBOUT SILAHA DHIDI YA ALSHABAB

Washington D.C -Marekani,

Marekani itaipatia Kenya, Uganda na Djibout vifaa vya kijeshi vya kisasa ili kuwasaidia kupambana na wanamgambo wa Al-shabab imearifiwa.

Kwa mujibu wa gazeti la Wall Street la Marekani katika habari yake hapo juzi tarehe 20,Kenya watapatiwa ndege zinazoruka bila rubani zipatazo nane na vifaa vingine vya kijeshi ikiwemo magari yenye silaha.

Nchi nyingine zilizobaki ambazo ni Uganda,Burundi na Djibout zitapatiwa vifaa vya kijeshi pia kuzisaidia kukabiliana na waasi hao.

RAIS MPYA WA INDIA ATANGAZWA-ni Pranab Mukherjee




INDIA,
 Aliyewahikuwa waziri wa fedha wa zamani wa India Bw.Pranab Mukherjee amechaguliwa kuwa rais mpya wa nchi hiyo kwa kushinda zaidi ya nusu ya kura zilizopigwa na mabunge ya nchi hiyo. Kwa kawaida uchaguzi wa rais nchini India hufanywa na mabunge mawili na rais huwa hana madaraka makubwa kama ilivyo kwa nchi za kijamhuri kama Tanzania.

Mukherjee, 76, mfuasi wa chama cha Congress alikuwa akitumainiwa kushinda kiti hicho kutokana na kukubaliwa na watu wengi wakiwemo wale wa kutoka vyama pinzani tofauti na mpinzani wake Bw.Pumo A. Sangma (64) aliyewahi kuwa spika wa bunge la nchi hiyo anayetoka katika chama cha Bharatiya Janata Party.

 Licha ya kile kilichoonekana imani katika matamshi yake ya mwezi uliopita kuwa nafasi hiyo inatakiwa kutolewa tu na sio kufikiriwa au kuhangaikiwa Bw. Mukherjee amefanya juhudi za ziada kupata nafasi hiyo hasa alipokuwa akitaka uungwaji mkono na wa vyama vya upinzani vyenye mlengo wa kushoto.

Rais wa India huchaguliwa na wabunge 4'896 kutoka majimbo mbali mbali nchini humo na ushindi huo wa Mukherjee utaongeza nguvu ya serikali bungeni, wakati ambao inalaumiwa kwa ukuaji mdogo wa uchumi na tuhuma mbali mbali za utumiaji mbov wa ofisi za umma.

HERI YA MWEZI MTUKUFU!


MWEZI WA RAMADHAN NI MWEZI WENYE KULETA BARAKA KWA KILA MUAMINI, ANGA ZA KIMATAIFA TUNAWAOMBEA KILA LA KHERI WAISLAMU WOTE NA WOTE WENYE NIA NJEMA NA DINI YA KIISLAMU KILA LAKHERI NA BARAKA KATIKA MFUNGO HUU MTUKUFU WA RAMADHAN!!