Monday, April 28, 2014

HAFLA YA MIAKA 50 YA UHURU WA TANZANIA YAFANA VIWANJA VYA IKULU

1Rais  wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dr. Jakaya Mrisho Kikwete  na Rais wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar Dr. Ali Mohamed Shein wakikata keki katika sherehe ya Miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ulioasisiwa na Mwalimu J.K.Nyerere na Mzee Abeid Amani Karume Aprili 26 mwaka 1964 hafla hiyo iilifanyika jana kwenye viwanja vya Ikulu na kuhudhuriwa na Makamu wa Rais Dr. Gharib Bilal, Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Seif Ali Idd, Waziri Mkuu Tanzania Mh. Mizengo Pinda na viongozi mbalimbali wa serikali taasisi za dini na vyma vya siasa, Kushoto  ni Mke wa Rais mama Salma Kikwete na kushoto ni Mkewa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-DAR ES SALAAM) 3Rais  wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dr. Jakaya Mrisho Kikwete  na Rais wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar Dr. Ali Mohamed Shein wakiwalisha keki wake zao katika hafla hiyo.
4Rais  wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dr. Jakaya Mrisho Kikwete akibonyeza kifaa maalum cha kufyatua mafataki wakati wa hafla ya kuadhimisha miaka 50 ya uhuru wa Tanzania.6Mafataki yakilipuka katika viwanja vya ikulu ikiwa ni moja ya burudani katika sherehe hizo.7Naibu Waziri wa Sayansi na Teknolojia Mh. Januari Makamba akiwa katika picha ya pamoja na Msanii MwanaFA aka Binamu.8Wazee wa Politiko Lifo Chipaka na Fahmi Dovutwa kulia wakifurahia Muungano.9Wasanii mbalimbali walikuwepo katika hafla hiyo.9aWadau kutoka Lugumi Enterprises walihudhuria katika hafla hiyo.10Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa Jembe Jesca Msambatavangu kushoto na Katibu wa CCM Wilaya ya Mufindi Miraji Mtaturu wakiwa katika hafla hiyo.11Mama Arafa Ridhiwani akiwa na ndugu zake katika hafla hiyo.12Mke wa Waziri Mkuu mama Tunu Pinda katikati akiwa katika picha ya pamoja na Mama Arafa Ridhiwani Kikwete kulia pamoja na ndugu zake.