Saturday, February 28, 2015

Thursday, February 12, 2015

KUMBE HII NDIYO SABABU YA MSANII LADY JAYDEE KUTOFANYA COLABO NA WASANII WA KIKE



Lady Jaydee ametoa nafasi kwa mashabiki na followers wake wa Instagram kumuuliza maswali na kuahidi kuyajibu. Miongoni mwa maswali mengi aliyoulizwa ni pamaoja na kwanini hafanyi collabo na wasanii wa kike, na kuhusu Ugomvi / Tofauti na watu (wasanii) /Radio na mpango wa kupatana nao.
“Duuuh maswali yako mengi sana karibia 300 Ila ki ukweli yote yanafanana So, what i will do I will pick top 10 ya maswali yaliojirudia, halafu nitalijibu moja baada ya jingine. Watu wooote nikiwakusanya, maswali yenu hayazidi 10, Leo mtaelewa kwanini sijibu comments. Sababu nikifanya hivyo itabidi niache kazi zote, Kaeni tayari kwa majibu, moja baada ya jingine” aliandika Jaydee kabla hajaanza kuyajibu.


Haya ni baadhi ya maswali na majibu.
Swali: Kwanini sifanyi collabo na wasanii wa kike?
Jibu :
“Nimewahi kufanya na wasanii mbali mbali wa kike ila sijui kwanini hamjaziskia.
1.Mwasiti amewahi kunishirikiisha
2. Nimewahi kumuandikia na kushiriki kuimba kwenye wimbo wa movements za Albino na Kaysha
3. Nimewahi kumwandikia na kushiriki kuimba nae Nakaaya Sumari
4. Nimewahi kumwandikia wimbo Patricia Hillary
5. Nimewahi kumshirikisha RAY C kwenye wimbo wangu toka Album ya Machozi unaitwa, Nimekubali na wapo wasichana mbali mbali waliopita Machozi Band na kujifunza kuimba leo mnawafahamu.

Kumbukeni tu kuwa kutoka kwa mtu itategemea na nyimbo zake kuwa promoted redioni na mimi sio mwenye hizo redio.
Msaada pekee ni kushiriki kila ntakapotakiwa kufanya hivyo”

Swali: Ugomvi / Tofauti na watu Artists /Radio Na mpango wa kupatana nao
JIBU :
“Nitapatana na mtu atakae kubali kuwa alikosa, km naamini yeye ndio alinikosea itabidi aniombe msamaha. Kama mimi ndio nilikosa nitaomba pia msamaha,Otherwise hakuna miujiza.Siwezi kumuomba mtu msamaha endapo naamini kabisa sijakosa .

Niliowahi kuwakosea nilishawaomba msamaha wooote.Hakuna binadamu asie kosea Ila siwezi ku surrender kiuongo au kwa uoga wa maisha.

Naamini hata nikiuza nyanya bado wapo watu wanaohitaji nyanya, na watanunua. Je! Hili jibu limejitosheleza?.Naamini hata nyinyi mmewahi kutofautiana na watu wenu wa karibu.
Kukubali kosa ndio mpango”

Swali: Siasa
Mchango katika jamii
JIBU:
“Sio mpenzi na sitegemei kujihusisha na siasa, wala chama chochote. Kila binadamu ana mchango katika jamii kwa njia moja au nyingine, Direct au indirect.

Ukitambua moja lolote nililowahi kulifanya likakupa furaha ndio mchango wangu, samahani kwa yaliokuudhi.

Swali la 4 mpk la 10 ntamalizia kesho, yasipoisha hata kesho kutwa.Najua kuna maswali mazito mnayosubiria majibu, yale ya kidaku zaidi. …Na mimi kwa kuwarusha roho nayaweka mwiiiishooo.Yatajibiwa tu, msitie shaka. …”

Friday, February 06, 2015

Vanessa Mdee na Barnaba wamekutana tena, hizi ni picha za utengenezaji wa video yao mpya.

.
.
Vanessa Mdee na Barnaba Elias Feb 6, waliingia location kumalizia utengenezaji wa video mpya ya single yao iitwayo Siri, video hiyo imeongozwa na Hanscana kwenye kijiji cha Makumbusho Dar es Salaam.
Hizi ni baadhi ya picha ambazo nimekuchukulia baada ya kushuhudia utengenezaji wa video hiyo mpya, zicheki hapa zote mtu wangu.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.

Picha,Jibu la Kim Kardashian kuhusu watu anaotaka kupiga nao SELFIE, utashangaa.


Kim k ambaye ni mke wa rapa Kanye West ni miongoni mwa mastaa wenye vitabu ni hivi karibuni anatarajia kutoa kitabu chake cha picha za SELFIE.
Kwenye kujibu maswali machache ya mashabikki wake Kim K aliulizwa kama angepata nafasi ya kuchagua mtu tofauti wa kupiga naye Selfie Kim alijibu
“My Dad, or Jesus, or Marilyn Monroe, siwezi kuamua ”

Wednesday, February 04, 2015

AJALI MBAYA DODOMA! COASTER YAGONGA TRENI. SHUHUDIA



Basi la abiria aina ya Toyota Coaster likiwa limepinduka baada ya kuigonga treni.
Taswira baada ya ajali hiyo.
Wananchi wakiwa eneo la ajali hiyo. Basi la abiria aina ya Toyota Coaster lenye namba za usajili T 932 AFU linalofanya safari zake kati ya Nanenane na Ng'ong'ona mkoani Dodoma limepata ajali leo baada ya kuligonga treni na kupinduka maeneo ya Benki Kuu mkoani humo.

Tuesday, February 03, 2015

Huyu amewekewa mikono ya mtu mwingine!


oppp
Madaktari katika Chuo cha Tiba cha Amrita, Kochi huko India wamefanikiwa kufanya upasuaji wa aina yake wa kupandikiza mikono mipya kwa binadamu aliyekatika viungo hivyo.
Upandikizaji huo uliofanyika Januari 12 na 13, ulifanikiwa kwa mara ya kwanza, baada mwanamume mwenye umri wa miaka 30, aliyekatika mikono katika ajali ya treni kuwekewa mingine ambayo ilichukuliwa kutoka kwa kijana wa miaka 24 aliyefariki katika ajali ya gari.
Mkuu wa kitengo cha upasuaji katika chuo hicho, Prof. Subramania Iyer alisema: “Siku 14 baada ya upasuaji, mikono ilikubaliwa na mwili na ikaanza kujongea, yaani aliyepandikizwa aliweza kuisogeza huku na kule. Mgonjwa alitolewa chumba cha wagonjwa mahututi na huduma nyingine za kumchunguza ziliendelea.”
amrrrr
Moja ya majengo ya chuo cha tiba cha Amrita Kochi
Daktari katika Taasisi ya Mifupa na Mishipa ya Fahamu Hospitali ya Muhimbili (Moi), Prof. John Kahamba aliliambia Gazeti la MWANANCHI kuwa hiyo si mara ya kwanza kwa upandikizaji wa mikono kufanyika duniani kwani ina tofauti kubwa na upandikizaji wa figo au ini.
Profesa Kahamba alisema upasuaji huo unafanyika kwa kuhakiki mambo mbalimbali ikiwamo uwiano wa kundi la damu, uhai wa seli na misuli na mishipa midogo ya fahamu.
Profesa Kahamba alisema kama upandikizaji wa figo unavyofanyika, kadhalika upandikizaji wa mikono unahitaji umakini wa muda.
Anasema iwapo utachelewa kuunganisha mikono baada ya kuitoa, seli zake zinaweza kufa na kushindwa kufanya kazi zitakapopandikizwa kwenye mwili.