Thursday, February 09, 2012

IVORY COAST YAIFUATA ZAMBIA FAINALI, YAWATOA MALI.



Goli la nguvu na juhudi binafsi lake Mchezaji mahiri wa Ivory Coast anayeichezea Arsenal ya uingereza Yao Gervinho jana lilikuwa tosha kuwaingiza tembo kutoka magharibi ya Afrika katika fainali.
Gervinho ambaye tangu mwanzo wa mashindano haya kuanza alionekana kuwa katika chini ya kiwango jana aligeuka mwabi makali kwa goli lake hilo mahiri kabla ya kipindi cha kwanza kuisha.
Ivory coast ambao walionekana kuwa moto tangu mwanzo wa mchezo kwa kuwakosa mali katika dakika ya 6 ya mchezo baada ya kichwa cha Didier Drogba kugonga mwamba na kurudi uwanjani.
Dakika kumi baadae baada ya shambulizi hili Salomon kalou alitoa pasi murua iliyomkuta Yaya Toure katika nafasi nzuri ya kufunga ingawa safu ya ulinzi ya Mali iliokoa shambulizi hilo.

Mwishowe katika dakika ya 45 Gervinho aliiandikia Goli timu yake baada ya juhudi binafsi ambapo alitumia kasi aliyonayo kusonga mpaka golini kutoka kati kati ya uwanja akitumia upande wa Kushoto na baadae kurudi kulia akiwa ndani ya eneo la kumi na nane na kufunga kwa mguu wa kulia.

katika kipindi cha pili hakukuwa na ushindani mkali kama kile cha kwanza ingawa timu zote mbili zilitengeneza nafasi ya kufunga, lakini bahati mbaya kwa Mali ambao hawakuweza kurudisha goli hilo mpaka mwisho wa mchezo.

Kwa matokea hayo mali watacheza na zambia siku ya Jumamosi kumtafuta mshindi wa 3, huku Ivory coast wakiwafuata Zambia katika fainali zitakazochezwa hapo jumapili ya tarehe 12 wezi huu Katika mji wa libreville.


MGOMO WA MADAKTARI TANZANIA WAFIKIA KIKOMO-Katibu mkuu na mganga mkuu wasimamishwa kazi.

DAR ES SALAAM-TANZANIA,
Mgomo wa Madaktari wa hospitali za umma nchini tanzania hatimaye umefikia kikomo leo hii huku kukishuhudiwa katibu mkuu wa Wizara ya Afya ndugu. Blandina Nyoni na mganga Mkuu wa wa serikali bw. Deo Mtasiwa wakisimamishwa kazi kupisha Uchunguzi dhidi yao.

Hatua hiyo imekuja wakati waziri mkuu wa Tanzania Mh.Mizengo Kayanza Pinda alipokutana na madaktari hao pamoja na wawakilishi wa wale wa mikoani kujadili suala hilo.
Katika kikao hicho serikali imekubali kuyashugulikia madai ya madaktari hao ambayo ni pamoja na Nyongeza ya mishahara, mazingira mazuri ya kazi na Marupurupu mengine ambay madaktari hao wanaidai Serikali.

Kwa Makubaliano hayo serikali na madaktari hao wamekubaliana kusitisha mgomo huo na Kurudi kazini kuanzia hapo kesho siku ya Ijumaa.
Mgomo huo umedumu kwa muda wa wiki tatu na kusababisha adha kubwa kwa wananchi wa kawaida ambao serikali za umma ndio kimbilio lao.

AFCON 2012- ZAMBIA YAIDUWAZA AFRIKA , YAITOA GHANA.


Zambia hapo jana wameiduwaza Afrika na Ulimwengu mzima baada ya kuwatoa mabingwa mara nne wa michuano ya mataifa ya Afrika Ghana 'The Black Star' kwa kuwafunga Goli 1-0 katika nusu fainali ya kwanza Uwanja Wa Bata Huko Gabon.

Kwa matokeo hayo Zambia wameingia fainali za michuano hiyo ikiwa ni mara ya kwanza tangu mwaka 1994 walipofungwa na Nigeria Ambapo safari hii wanaenda kuktana na Ivory coast ambao jana wamewatoa mali kwa goli 1-0.

Ghana itabidi wajilaumu wenyewe kwa kupoteza nafasi nyingi ikiwemo ile ya Penati iliyokoswa na Asamoah Gyan, huku nyota huyo na mwenzake john Mensah ambao ndio tegemeo la timu hiyo wakicheza chini ya kiwango.
Mayunga ambaye aliingia kumbadili James Chamanga katika kipindi cha pili alionesha uwezo na uwepo wake uliwapa tabu walinzi wa Ghana.

Ghana walimaliza Mpira huo wakiwa watu 10 baada ya Mchezaji wake Derek b
oateng kupewa kadi nyekundu dakika sita kabla ya dakika 90 kumalizika bada ya kupokea kadi ya pili ya njano kutokana na faulo aliyoicheza.
Zambia wanaingia katika fainali hizo wakiwa na kumbukumbu mbaya ya miaka 19 iliyopita huko gabon ambapo iliwapoteza wachezaji wake wote 25 baada ya ajali ya ndege iliyokuwa imewabeba wachezaji hao.