Whitney ambaye hivi karibuni alianza kurudi jukwaani tangu mwaka 2006 alipotalakiana na mumewe Bobby Brown baada ya ndoa yao ya miaka 14, wakiwa na mtoto wao Bobbi Kristina ,ambapo alifanikiwa kufanya wimbo mmoja na mwanamuziki Akon uliotambulika kwa jina la "Like I never Left" na katika siku za hivi karibuni kabisa akipata mwaliko wa kutumbuiza katika tamasha la utangulizi la utoaji wa uzo za Grammy kwa mwaka 2012 ingawa katika mazoezi sauti yake ilionekana kuwa dhaifu na isiyo na makali ya miaka ile tena.
Katika mafanikio yake whitney alivuma kama mwanamuziki bora wa kike duniani huku album zake zikishika chati za juu na kumuwezesha kuwa moja ya wasanii waliowahi kuuza zaidi duniani. Pia Whitney amewahi kuvuma katika anga za filamu ambapo alicheza katika filamu za "The Bodyguard" na "Waiting to Exhale" huku nyimbo zake zikitumika kama soundtracks na kumpatia mauzo ya kiwango cha juu.
Akiwa Binti mdogo Whitney mtoto wa muimbaji wa nyimbo za dini Cissy Houston na marehemu John Houston aligunduliwa kipaji chake na clive Davis aliyekuwa Producer katika lebo ya Arista Records mwanzoni mwa miaka ya 1980 ambaye alimuongoza kuuza jumla ya nakala milioni 170 za sauti na video huku nyimbo zake za "I will always love you" na " The Greatest Love of All".
Hata hivyo maisha ya mwanamuziki huyo baadae yalitawaliwa na matumizi ya pombe na dawa za kulevya hali iliyomuathiri afya yake.
Pamoja na yote Whitney Houston atakumbukwa kwa mchango wake mkubwa katika muziki ambao umewaathiri vizazi vya sasa wakiwemo wanamuziki Brandy, Monica, Mariah Carey, Beyonce na Christina Aguilera ambao wameiga mfano wake, pia atakumbukwa kwa kujishighulisha na masuala ya kijamii ikwemo haki za wamarekani weusi hasa katika masuala ya Elimu.
MwenyeziMungu mwenye Rehema ailaze mahali Pema Peponi roho ya mpendwa wetu Whitney Houston Amen!