Sunday, December 02, 2012

RAIS ABBAS APOKEWA KISHUJAA PALESTINA .

Ramallah wakisherehekea kukubaliwa na Umoja wa Mataifa

RAMALLAH,
Amekaribishwa kama shujaa baada ya kufanya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kupiga kura kupandisha hadhi ya Wapalestina.

Akiwahutubia wafuasi wake mjini Ramallah, Ufukwe wa Magharibi, Rais Abbas alisema njia ilikuwa ndefu na shinikizo nyingi sana, lakini Wapalestina walisimama kidete na kushinda:
"Tulikwenda New York, tumebeba ujumbe wa uchungu na ndoto ya watu wetu kukabidhi kwa ulimwengu ujumbe wa haki na uhuru.

Ulimwengu umetoa kauli kwa sauti kubwa. Umesema: ndio liwepo taifa la Palestina.Haki za Wapalestina, ndio.Uhuru wa Palestina, naam. 
Uhasama, la.Makaazi ya walowezi, hapana.Kuikalia Palestina, sivyo"Alisema rais huyo.(CHANZO BBC)

ANDAKI LAANGUKA NA KUUA WATATU JAPAN-WENGINE WAKWAMA NDANI.

TOKYO ,JAPAN.

Police officers and firefighters gather in front of the Sasago Tunnel on the Chuo Expressway in Otsuki, Yamanashi prefecture, in this photo taken by Kyodo December 2, 2012. REUTERS/Kyodo


Smoke is seen from the Sasago Tunnel on the Chuo Expressway in KoshuWatu watatu wameripotiwa kufariki  jumapili ya leo huko mjini Tokyo Japan baada ya sehemu ya andaki la barabara lenye urefu wa km 4.7  kuanguka na kufunika magari yaliyokuwa yanapita juu yake.kwa mujibu wa televisheni ya Japan juhudi za kuwaokoa watu wengine wliokwama ndai ya andaki hilo zinaendelea.Kumekuwepo na kufuka kwa moshi ingawa vikosi vya kuzima moto nchini humo vimesema vimedhibiti moto huo ingawa kuna dalili za tishio la kuanguka zaidi kwa andaki hilo.

TUTAPUNGUZA MAAMBUKIZI YA UKIMWI-JK


LINDI-TANZANIA, RAIS Jakaya Kikwete ameeleza mikakati ya Serikali yake kuwa ni kuhakikisha inamaliza kabisa maambukizi mapya ya virusi vya Ukimwi ifikapo mwaka 2015.
Akilihutubia taifa kwenye kilele cha maadhimisho ya Siku ya Ukimwi duniani Rais Kikwete alisema: “Tunataka tupunguze maambukizi na ikiwezekana mpaka 2015, kuwe na maambukizi sifuri kabisa. Huu mradi tumeshauanza, ila leo ni kama tunauzindua upya.”
Katika maadhimisho hayo yaliyofanyika kitaifa mkoani Lindi, Kikwete alitaja mikakati mbalimbali aliyosema Watanzania hawana budi kuifuata ili kufikia kwenye hatua hiyo.
Miongoni mwa miakakati hiyo ni kuhamasisha watu kupima, waathirika kutumia Dawa za Kupunguza Makali ya Ukimwi (ARV), kuzuia maambukizi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto, elimu ya Ukimwi kutolewa shuleni na kwamba Serikali yake itahakikisha waathirika wanapata dawa bila malipo.
Alisema kwamba Serikali itahakikisha inaliingiza somo la kujikinga na Ukimwi katika mitalaa ya elimu nchini na kuongeza kuwa atatafuta fedha, ili kuhakikisha kuwa elimu inatolewa kwa watoto hao.
Rais Kikwete alifafanua kuwa katika mpango huo wa kutoa elimu ya Ukimwi kwa wanafunzi,  Serikali imeweza kuwafikia asilimia 65 ya wanafunzi wa shule za msingi na asilimia 75 wa shule za sekondari.
“Wapo wanaosema  tunawafundisha watoto tabia mbaya, lakini hao wanaosema hivyo, ndiyo wamekuwa vinara wa kuwapeleka watoto wao Jando na Unyago,” alisema na kuongeza:
“Mangariba  wanatakiwa kuwapa watoto hawa elimu juu ya Ukimwi,  jinsi ugonjwa huu unavyoambukizwa na jinsi ya kujikinga.”
Aliwataka pia wazazi kutoona aibu kuwafundisha watoto wao jinsi ugonjwa huo unavyoambukizwa na kwamba wakifanya hivyo watakua wameokoa vifo na kumaliza maambukizi mapya.
Kikwete alisema pia kwamba kuna mradi wa kutokomeza maambukizi ya Ukimwi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto, ambapo aliwataka wajawazito kupima afya zao ili waweze kupewa ushauri wa jinsi ya kumkinga motto ili azaliwe bila kuwa na maambukizi.
Alitaja jambo jingine muhimu kuwa ni kuwahimiza Watanzania kupima afya zao kwa hiari na kwamba hadi sasa watu 17 milioni nchini wameshapima.(CHANZO-MWANANCHI)

SIKU YA UKIMWI DUNIANI YAAADHIMISHWA-MAAMBUKIZI YADAIWA YAPUNGUA KWA 50%



Kwa pamoja twaweza kutokomeza UKIMWI
Kwa pamoja twaweza kutokomeza UKIMWI

Tarehe 1 desemba  kila mwaka ni  siku ya Ukimwi duniani ambapo dunia inaadhimisha siku hiyo huku ikikabiliwa na changamoto mbalimbali huku Shirika la Afya Duniani, WHO likitoa takwimu zinazoonyesha kuwa maambukizi mapya yamepungua kwa asilimia 50 katika nchi 13 za kusini mwa jangwa la sahara.

Kutokana na takwimu hizo kundi la wazee linaonekana kusahaulika katika takwimu za watu wanaoishi na virusi vya Ukimwi kutokana na kundi hilo kuachwa kando katika suala la maambukizi na mapambano dhidi ya ugonjwa huo.

Pamoja na takwimu za shirika la afya duniani kutoa matumaini makubwa kwa nchi za kusini mwa jangwa la sahara bado nchi za afrika mashariki zinawajibika kuongeza jitihada za kukabiliana na maambukizi na huduma kwa watu wanaoishi na virusi vya ukimwi.

Aidha kuwepo kwa maambukizi mapya kunadaiwa kutokana na mambo mengi huku mapenzi baina ya wanaume kwa wanaume na wanawake kuuza miili yao vikioneka kuchagiza tatizo hilo
Hata hivyo safari bado ni ndefu katika kukabiliana na UKIMWI na muhimu ni kutekeleza kauli mbiu ya mwaka huu inayosisitiza kutokuwepo kwa maambukizi ya kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto na maambukizi mapya miongoni mwa jamii na kutokuwepo vifo ifikapo mwaka 2015.
 

RAIS MPYA WA MEXICO APINGWA



Rais mpya wa Mexico Enrique Pena Nieto
Picha na Reuters

Takribani watu 25 wamejeruhiwa katika vurugu kati ya polisi na waandamaji wanaopinga kuapishwa kwa rais mpya wa Mexico Enrique Pena Nieto ambaye alipata ushindi katika uchaguzi wa mwezi julai mwaka huu.

Muda mchache baada ya kuapishwa Rais Pena Nieto alitoa hotuba ambapo ameahidi kuimarisha usalama na uchumi katika nchi hiyo.
Sherehe za kuapushwa kwa rais huyo zilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kimataifa akiwepo makamu wa rais wa Marekani Joe Biden.
Pena Nito aliibuka mshindi dhidi ya mpinzani wake wa karibu Andre Manuel Lopez Obrador ambaye alipinga matokeo hayo na kudai mpinzani alishinda kwa sababu alinunua kura.
Pena Nieto anaingia madarakani akikabiliwa na jukumu kubwa la kuhakikisha anaendeleza vita ya kupambana na magenge ya wauzaji wa dawa za kulevya ambayo ilianzishwa na mtangulizi wake Felipe Calderon.(CHANZO RFI).