Tuesday, June 05, 2012

SYRIA YARUHUSU MASHIRIKA YAKUTOA MISAADA.


 hatimayeserikali ya Syria imesalimu amri na kuyaruhusu mashirika ya kutoa misaada kuanza shughuli zao katika mikoa minne ya  Homs, Idlib, Deraa na Deir al-Zour iliyopatwa na mapigano makubwa kati ya majeshi ya Serikali na Waasi.
Kwa mujibu wa Umoja Wa mataifa  serikali ya Syria imekubali kuyaruhusu mashirika ya kutoa misaada kufanya kazi katika mikoa hiyo. Afisa mmoja wa Umoja huo amesema kuwa serikali ya Syria imekubali kwa maandishi kuwaachia wafanya kazi wa kutoa misaada pamoja na magari yenye vyakula na misaaada mingine kuingia. ndani ya mikoa hiyo.
Afisa huyo alisema kuwa suala hilo litakuwa ni kipimo kikubwa cha Syria kwa jumuiya ya kimataifa kama ina nia nzuri na wananchi wake.

RAIS WA NIGERIA ATEMBELEA ENEO LA AJALI YA NDEGE.

Rais wa Nigeria, Goodluck Jonathan

http://www.dw.de/image/0,,15996043_401,00.jpg

LAGOS, NIGERIA

©Jonathan Rebboah/Wostok Press/Maxppp France, Paris 25/11/2011 Le president du Nigeria Goodluck Jonathan arrive au palais de l Elysee The President of Nigeria Goodluck Jonathan at the Elysee PalaceRais wa Nigeria Goodluck Jonathan amehahidi kuwa serikali yake itaimarisha usafiri wa anga baada ya hapo jana watu  153 kufariki baada ya ndege ya shirika la Dana abiria kuanguka nchini humo.
Rais Jonathan ametoa ahadi hiyo  wakati alipolitembelea eneo la kitongoji cha mji wa Lagos, ambako ndege ya abiria ya shirika la Dana ilianguka jana na kuwaua abiria wote 153 waliokuwemo katika ndege hiyo.
"Tumekuwa tukijizatiti kuboresha sekta ya usafiri wa ndege hapa nchini. Ajali hii ni pigo kubwa kwetu na nitahakikisha ajali kama hii haitokei tena humu nchini,"alinukuliwa rais huyo baada ya kushuhudia ajali hiyo.


Uchunguzi wakwama;
Kwa mujibu wa taarifa ya mwandishi wa habari wa shirika la AFP, polisi walilazimika kutumia vitoa machozi wakati watu takriban 2,000 walipojaribu kuingia eneo lililofungwa na polisi wakitaka kushuhudia athari za ajali hiyo na hivyo kutatiza uchunguzi.
hadi leo  waokoaji wamefaulu kutoa maiti zisizopungua 62 kutoka kwa mabaki ya ndege hiyo. Kanisa, jengo la makazi ya watu la ghorofa mbili na duka la huduma za uchapishaji liliharibiwa vibaya katika eneo la ajali.  Moshi bado unafuka katika eneo la ajali na wafanyakazi wa zimamotowamekuwa wakiendelea na juhudi za kuuzima moto unaoendelea kuwaka kwenye mabaki ya ndege hiyo.
Solomon Omotayo ni miongoni mwa mashuhuda wa ajali hiyo ya  ndege  ikipoteza muelekeo muda mfupi kabla kuanguka katika kitongoji cha Iju jijini Lagos. "Tulipoiona, ilkuwa chini mno! Dakika kama mbili baadaye tukasikia mlio. Tuliufuata moshi hadi hapa. Maafisa waliondoa maiti lakini sijui ni ngapi. Ni hasara kubwa na maiti nyingi zingali zimefunikwa."alisema Solomon.

Kipanya na Muungano!

MBWANA SAMATA AFUATILIWA NA MAN CITY.

 ABDJAN.IVORY ,COAST
Mpelelezi wa vipaji wa timu ya Manchester City Joe Mulberry  ya Uingereza alikuwepo nchini Ivory Coast kuangalia vipaji vya wachezaji wa Afrika magharibi naKumfuatilia mchezaji wa Taifa Stars anayecheza Nchini Kongo katika klabu ya TP MazembeMbwana Samata.
Mpelelezi huyo alipanga hoteli moja na Taifa Stars na kuangalia mechi yake na Ivory Coast kwa mujibu wa vyanzo vya habari. Ingawa mwanzoni alifanya siri suala hilo baadaye baada ya kubanwa na mwandishi wa habari Edo Kumwembe alikiri na kusema anamchuguza Samata kuangalia maendeleo yake huku akionesha kuwa na rekodi kamili ya mchezaji huyo kutokana kuwa na taarifa lukuki za mchezaji huyo ikiwemo magoli 2 aliyoyafunga katika ligi ya Klabu bingwa Afrika.

Hata Hivyo mpepelezi huyo alisema licha ya Mbwana kuwa mchezaji mzuri bado atahitaji kutafutiwa ligi nyingine za Ulaya kabla ya kucheza ligi kuu ya uingereza ili kukomaa na kuweza kuhimili mikiki mikiki ya ligi hiyo maarufu duniani.




MPELELEZI wa vipaji vya soka toka klabu tajiri England, Manchester City, Joe Mulberry alitua kwa siri mjini Abidjan na kupiga kambi kwenye hoteli ya Ibis Plateau, ambayo pia Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) ilifikia na lengo lilikuwa moja tu kuwachunguza wachezaji wa timu hiyo, Mwananchi limebaini.
Mulberry, raia wa Uingereza mwenye jukumu la kuchunguza vipaji kwa nchi za Afrika Magharibi, alifanya kazi ya kuipeleleza Stars bila kutaka mtu yeyote kufahamu kabla ya mwandishi wa habari hizi kumbaini.
Awali, Mulberry aliyeweka makazi yake nchini Ghana alipanga kwenye chumba namba 604 cha hoteli ya Ibis Plateau.
Baada ya gazeti hili kupata fursa ya kuongea naye muda mrefu, lilimbaini na ndipo naye alipomfichua siri kwamba alikuja Abidjan kwa ajili ya kuangalia pambano la Stars dhidi ya Ivory Coast.
Kwa mujibu wa uchunguzi wake wa haraka, Mulberry alivutiwa na kipaji cha mshambuliaji Mbwana Samata na cha kushangaza katika kipindi kifupi tayari alikuwa amekusanya habari zote za Samata.
Miongoni mwa dodoso muhimu alizokusanya ni pamoja na mabao mawili aliyofunga wakati wa mchezo wa Ligi ya Mabingwa wa Afrika dhidi ya Dynamo ya Zambia na El Merreikh ya Sudan akiwa na timu yake ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Mulberry alikiri Samata alikuwa na kipaji kikubwa lakini akataka amuone zaidi siku za usoni kujua kama alikuwa na uwezo mkubwa wa kufunga kama ilivyo katika kuuchezea mpira.
“Nitasafiri kwenda Ghana kumtazama kwa ajili ya pambano la ligi ya mabingwa kati ya Berekum Chelsea dhidi ya TP Mazembe pale Accra, Julai 5. Kama atakuwa yuko safi tena nitajaribu kuzungumza na timu yake.”
Hata hivyo, Mulberry alisema Samata hawezi kucheza katika Ligi Kuu ya England kwa sasa na badala yake anaweza kupelekwa katika ligi nyingine kabla ya kupata uzoefu wa kucheza ligi kubwa Ulaya. 

VIPEPERUSHI VYA UTENGANO UNGUJA NA PEMBA VYASAMBAZWA ZANZIBAR-Mwanzo wa Mpasuko Mwingine?




Takribani miaka 17 tangu baba wa taifa hayati Mwalimu Julius kambarage Nyerere aionye Tanzania juu ya ubaguzi, 'maono' yake yameanza kutimia baada ya kusambazwa kwa vipeperushi vinavyowataka wananchi wenye asili ya Pemba kuondoka Unguja siku chache baada ya Jumuiya ya Uamsho Mihadhara ya Kiislamu (Jumiki) kuukataa muungano wa Tanzania na kutaka Zanzibar ijitenge na Tanzania bara(Zamani Tanganyika). Vipeperushi hivyo vinavyosambaza na kundi lililojitambulisha kama 'Watu wa Unguja' limetoa tahadhari kwa watu wa Pemba kuondoka Unguja huku likiwatuumu kwa kuchochea vurugu na kuanyang'anya ardhi yao.

Kundi hilo pia katika vipeperushi hivyo limeushutumu Jumuiya ya Uamsho Mihadhara ya Kiislamu (Jumiki) kuwa ni kundi la kisiasa linalojitokeza kama kundi la dini.
“Watu wa Unguja tunatoa ujumbe mahususi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete…. Tumechoka kuishi na Wapemba katika kisiwa chetu cha Unguja, kwani ni watu wasio na fadhila ya aina yoyote ile,” isehemu ya kipeperushi hicho inasema na kuendelea;
“Hivyo, tunakuomba ufanye mazungumzo na Rais wa Zanzibar ili Wapemba wapewe kisiwa chao cha Pemba.”

Vipeperushi hivyo pia vimewatuhumu wapemba kuwa na asili ya Msumbiji na kutaka Pemba iondolewe katika Muungano na Tanganyika irudishwe na kufanya Muungano na Unguja kwani wanaochochea vurugu hizo ni watu kutoka Pemba. huku kikiwataja baadhi ya viongozi kwa majina.

 Tamko la Jumki:

Kwa upande wake  Jumuiya ya Uamsho Mihadhara ya Kiislamu (Jumiki) imepuuzia vipeperushi hivyo na kuviita havina maana, msemaji wa kundi la Jumki Sheikh Farid amesema kundi la Jumki lliundwa na watu wa Unguja na Pemba kwa nia ya kusambaza dini na kuongeza kuwa dini ya kiislamu inaruhusu waumini wake kushiriki katika siasa, “Katiba ya Zanzibar inasema kuwa kila mtu ana haki ya kushiriki kwenye uongozi wa nchi. Hata Mtume Muhammad (S.AW), alikuwa ni rais wa eneo lake na alikuwa kiongozi wa dini… Siasa ni neno la Kiarabu likiwa na maana ya uongozi na uongozi una mambo mengi. Kwa hiyo tuna haki kabisa ya kushiriki siasa,” alisema Sheikh Farid.


Uzushi?: 

Wakitoa maoni yao katika baadhi ya mitandao ikiwemo Facebook na jamii Forum wananchi wenye asili ya Zanzibar wamekuwa na mitazamo tofaouti ambapo wapo waliowatuhumu  watu wa bara kuwa ndio wenye kueneza Propaganda hizo zenye chuki huku wakidai kuwa wo ni wamoja na wanataka zanzibar huru, huku wengine wakiunga mkono hoja ya kundi la 'watu wa Unguja'.