Friday, August 15, 2014

MICHEPUKO NOMAAAAAA........YAZIDI KULETA MADHARA ,HUYU AFANYIWA KITU MBAYA

 
Mbuva, akiwa na majeraha usoni baada ya kumwagiwa mafuta ya moto.
MWANADADA aliyefahamika kwa jina moja la Mbuva, mkazi wa Gongo la Mboto jijini Dar, hivi karibuni amejikuta akiharibiwa uso wake kwa kumwagiwa mafuta ya moto na shosti wake aitwaye Mama Sofia, kisa kikidaiwa ni mume wa mtu. Tukio hilo lilitokea mwishoni mwa wiki iliyopita ambapo inadaiwa mama Sofia alimfanyia mwenzake unyama huo akimtuhumu kutembea na bwana wake.Akisimulia ilivyokuwa, Mbuva alisema: “Mama Sofia alipewa maneno ya uongo kwamba akiwa safarini eti nilitembea na bwana wake. 

“Siku ya tukio alinipigia simu akaniita kwake, nilikuwa sipajui ila akanielekeza, ile nafika tu majirani zake wakamwambia mimi ndiye nilikuwa nakwenda kulala pale na mume wake.“Nikajaribu kujitetea lakini hakunielewa. Nikaondoka, baadaye akaniita tena, kufika pale nikakuta ugomvi kati ya mama Sofia na mumewe, ghafla mama Sofia akatoka akiwa na kikombe cha mafuta ya moto akanimwagia usoni. 

“Nikaanza kupiga kelele, watu wakajaa  ndipo tukachukuliwa wote na kupelekwa katika Kituo cha Polisi cha Mazizini na tukaandikisha, mimi nikakimbizwa hospitali. Ameniharibu uso wangu bila kosa, Mungu atanilipia kwani naamini malipo ni hapahapa duniani.” 
Mama Sofia hakuweza kupatikama mara moja kuzungumzia tukio hilo.

Mapya kuhusu ndege ya Malaysia iliyopotea, ripoti Ya benki zinaonesha abiria wameendelea kuchukua pesa

Mapya kuhusu ndege ya Malaysia iliyopotea, ripoti Ya benki zinaonesha abiria wameendelea kuchukua pesa Ndege ya Malaysia Flight MH 370 iliyopotea miezi mitano iliyopita imerudi tena kwenye vichwa vya habari ikiwa na ripoti za kushangaza.Ripoiti ya benki ya Kuala Lumpur, Malaysia inaoensha kuwa akaunti za abiria wanne wa ndege hiyo zimechukuliwa pesa July 18 mwaka huu fedha ambazo zitajwa kuwa zaidi ya £20,000.Msaidizi wa mkuu wa upelelezi wa makosa ya jinai Malaysia, Izany Abdul Ghany ameiambia Mirror kuwa wanaendelea kufanya uchunguzi kufahamu jinsi ambavyo pesa hizo zilivyopotea.

 “We are investigating the case as unauthorised access with intent to commit an offence,We are getting CCTV footage from the bank to identify the suspects involved.”
Ameeleza kuwa pesa hizo zilitolewa katika akaunti ya abiria watatu na kuwekwa katika akauti ya abiria wanne kabla ya kutolewa kabisa.
Ndege ya Malaysia ilipotea March 8, 2014 ikiwa imebeba wafanyakazi 12 na abiria 227 kutoka katika mataifa mbalimbali na bado haijapatikana huku maafisa wakitangaza kuwa watu wote waliokuwa kwenye ndege hiyo wamepoteza maisha.
CHANZO TIMES FM

MADAI YA NDOA YA JIDE KUVUNJIKA GARDNER AFUNGUKA.

 
Staa wa muziki wa Kizazi Kipya, Judith Wambura ‘Lady Jaydee’ au ‘Jide’ akiwa na  mumewe Gardner G. Habash wakati wa harusi yao.

HABARI kubwa ya mjini hivi sasa, hasa kwenye mitandao ya kijamii ni juu ya madai mazito ya kuvunjika kwa ndoa ya selebriti wawili Bongo, staa wa muziki wa Kizazi Kipya, Judith Wambura ‘Lady Jaydee’ au ‘Jide’ na mtangazaji maarufu wa Radio Times FM, Gardner G. Habash, iliyofungwa Mei 14, 2005, Ijumaa linamaliza utata.
KABLA
Kabla ya Gardner kufunguka, habari zilidai kwamba wawili hao walikuwa kwenye gogoro zito ambapo Gardner aliamua kuondoka katika nyumba waliyokuwa wakiishi pamoja iliyopo Kimara-Temboni, Dar.
Ilidaiwa kwamba baada ya kuondoka nyumbani eti Gardner alikwenda kukaa kwa mmoja wa ndugu zake.
Habari hizo za kwenye mitandao ambazo hazitaji chanzo cha kuvunjika kwa ndoa hiyo, zilidai watu wa karibu na familia hiyo walisema hiyo siyo mara ya kwanza kwa wawili hao kutengana, lakini mzozo wa safari hii unaweza ukawa wa moja kwa moja.


ACHA BWANA!
Ilidaiwa kwamba ni kutokana na kutemana huko, ndiyo maana Jide msanii anayetajwa kuwa ni miongoni mwa wenye mafanikio kimaisha Bongo, hakwenda Kituo cha Polisi Oysterbay, Dar kumwangalia mumewe ambaye aliwekwa korokoroni kufuatia kitendo chao cha kuwakimbia askari wa usalama barabarani akiwa na Ephraim Kibonde hivi karibuni.

 
Maselebriti, ‘Lady Jaydee’ au ‘Jide’ na Gardner G. Habash wakipata ukodaki kwenye Red kapeti.

MAFUMBO?
Ilisemekana kuwa hisia za kuachana huko zinachochewa pia na baadhi ya maandiko ambayo mwanamuziki huyo wa Kibao cha Yahaya, amekuwa akiyaweka katika akaunti zake za mitandao katika siku za hivi karibuni.
Ilielezwa kwamba katika akaunti yake ya Mtandao wa Istagram, Jide aliweka picha yake akiwa amesimama nje ya gari lake kisha akasindikiza kwa kuandika hivi: “Walking away from troubles”, maneno ambayo kwa tafsiri isiyo rasmi yanamaanisha kujiondoa kwenye matatizo.
BINTI MACHOZI?
Ilidaiwa kuwa kabla ya hapo, katika mitandao inaandikwa kuwa Jide pia aliweka picha yake akionekana kuwa na huzuni huku Binti Machozi akilengwalengwa na machozi na kusindikizia na maneno akiuliza: “Sijui nisemaje?”
IJUMAA MZIGONI
Kufuatia tetesi hizo, gazeti hili liliamua kuzifanyia kazi ili kupata ukweli.
GARDNER ANASEMAJE?
Mtu wa kwanza kupigiwa simu alikuwa ni Gardner ambaye aliipokea na kabla hajaelezwa chochote, alisema alikuwa katika sehemu ambayo asingeweza kuzungumza, hivyo angempigia mwandishi wetu baada ya robo saa.
JIDE VIPI?
Baada ya kukata simu, mwandishi wetu alimwendea hewani Jide na baada ya kuita kwa muda, simu yake ilipokelewa na Gardner akasema: “Mpigie baada ya robo saa.”

 
‘Lady Jaydee’ au ‘Jide’ akipozi.

DAKIKA 20 BAADAYE, GARDNER AFUNGUKA
Dakika ishirini baadaye, Gardner alimtumia ujumbe mfupi wa simu mwandishi wetu na kumweleza kuwa alikuwa Kituo cha Polisi Oysterbay, Kinondoni jijini Dar ambako aliitwa kwa ajili ya soo lao la kuwakimbia trafiki.
Baada ya kubadilishana maneno kadhaa, baadaye aliamua kupiga na mazungumzo kati yake na Ijumaa yalikuwa kama ifuatavyo;
Ijumaa: Ebwana hivi hizi habari kwenye mitandao juu ya kuvunjika kwa ndoa yako na Jide zimekaaje?
Gardner: Hamna kitu bwana, watu wanaunganisha tu vitu sijui kwa sababu gani.
Ijumaa: Sasa kama ni hivyo kwa nini Jide hakuja kukuona siku ile ulipolala polisi?
Gadner: Unaona sasa, wao wanajua hivyo, lakini siyo kweli, Jide alikuja usiku sana kwa sababu alikuwa anawaogopa mapaparazi.
Unajua Jide yeye huwa hapendi hayo mambo. Alikuja usiku sana, lakini hata hivyo polisi nao walimgombea sana kumpiga picha.
Ijumaa: Wanasema Jide kuna maneno amepost kwenye akaunti zake mitandaoni zinazoonyesha kuchoshwa na wewe, unasemaje?
Gardner: Si ndiyo kama hivyo nimekuambia, watu wanaungaunga tu vitu ambavyo hawavijui na sisi hata hatujui malengo yao.
Wakati ule uliponipigia simu mara ya kwanza nilikuwa naye kwenye gari ananipeleka pale polisi, lakini akapaki mbali kwa sababu hiyohiyo niliyokuambia kuogopa mapaparazi na si unakumbuka hata ulipompigia kwenye namba yake nilipokea mimi?
Ijumaa: Kwani upo naye hapo sasa hivi nimsalimie?
Gardner: Hapana tumeachana mimi niko kwenye usafiri mwingine naelekea kazini na yeye yupo kwenye misele mingine.
Ijumaa: Haya kaka basi poa.
Gardner: Poa kaka, mchana mwema.
HUKO NYUMA
Si mara ya kwanza kwa mastaa hao kudaiwa kutibuana kwani walisharipotiwa kutaka kutengana lakini mara nyingi huwa wanakaa chini na kuyamaliza kimyakimya.

MWAKA WA TUZO KWA DIAMOND, ASHINDA TUZO NYINGINE BURUNDI

Diamond ashinda tuzo nyingine Burundi CV ya Diamond katika muziki inazidi kupanda na mwaka huu unaweza kutajwa kuwa mwaka wa tuzo kwa mwimbaji huyo ambaye amevuka mipaka na kuzinyakua au hata kutajwa tu kuziwania
.Wimbo wa My Number One wa Diamond umeshinda tuzo ya Wimbo Bora wa Afrika Mashariki katika tuzo za Burundi zinazojukana kama TTM Awards.
“Asante sana kwa Media wadau na Mashabiki zangu pendwa kwa kuifanya Number One kuwa Nyimbo Bora ya East Africa ya Mwaka kwenye tunzo za #TTTMAwards nchini Burundi.....” Ameandika Diamond kwenye Instagram akiambatanisha na picha ya mtu aliyempokelea tuzo hiyo.
NA TIMES FM