Sunday, April 08, 2012

LEMA AVULIWA UBUNGE ARUSHA.

                        ARUSHA,
Mahakama kuu ya Kanda Mjini Arusha imetengua matokeo ya ubunge katika jimbo la Arusha na kumvua rasmi Ubunge mbunge wa sasa wa Jimbo hilo ndugu Godbless Lema kwa makosa ya Udhalilishaji, kashfa dhidi ya Mpinzani mwenzake wa Chama Cha Mapinduzi Dk.Batilda Burian.Baada ya kusomwa hukumu hiyo vilio vilisikika ndani ya mahakama hiyo.


Mpaka sasa haijafahamika nini uamuzi wa Mbunge huyo na Chama Chake kwani kwa mujibu wa Jaji Gabriel aliyesoma hukumu hiyo Lema ana haki ya kukata rufaa.

STEVEN KANUMBA AFARIKI DUNIA!!

Kanumba 'The Great" Hivyo ndivyo atakavyokumbukwa na wengi! alikuwa gwiji nambari moja katika uigizaji wa Filamu za Kitanzania akianza wakati wa maigizo ya kwenye televisheni kupitia Kundi la Kaole Sanaa Group mpaka kufikia kumiliki kampuni ya utengenezaji filamu na kuwa kinara katika mafanikio ya filamu kwa Tanzania na Afrika mashariki.Steven kanumba ndivyo anavyofahamika rasmi ambaye hapo jana Usiku amefariki dunia na kuacha majonzi makubwa kwa watanzania na wapenzi wake kwa ujumla.
Chanzo cha kifo kimeelezwa kuwa ni kuanguka na kujigonga sehemu ya nyuma katika kichwa.ambapo taarifa zinasema marehemu alisukumwa na kuanguka na kugonga kichwa chini upande wa Nyuma na kusababisha kifo chake.
Polisi mkoani Dar es Salaam imethibitisha kuwa inamshikilia kwa mahojiano msanii mwenzake wa kike kutokana na kuhusika na kifo cha Kanumba, ambaye alijizolea umaarufu mkubwa katika ukanda wa Afrika Mashariki na kati na hadi Afrika Magharibi baada ya kuwashirikisha katika filamu zake baadhi ya wasanii Maarufu wa Kinigeria akiwemo Mercy Johnson na Noah Ramsey.

.Kanumba alizaliwa mnamo mwaka 1984 huko Shinyanga na kupata Elimu yake ya Msingi katika Shule ya Bugoyi huko Shinyanga na Elimu ya Sekondari katika shule tofauti ikiwemo Mwadui Sekondari ya Shinyanga na Christian Seminary ya Dar es salaam kwa O-level na baadae jitegemee kwa kidato cha tano na sita .
Kanumba atakumbukwa kwa filamu zake maarufu zikiwemo  Johari, Revenge, Dar to Lagos, Devil Kingdom, Uncle JJ na nyingine nyingi nyinginezo ambao kwa hakika zilileta msisimko katika tasnia ya Filamu Tanzania na Afrika Mashariki.

Anga za Kimataifa inatoa pole kwa familia,ndugu, jamaa na wapenzi wa Mpendwa wetu Steven kanumba Mungu ailaze Roho ya Merehemu mahala pema Peponi. Amen!


JOYCE BANDA AAPISHWA KUWA RAIS MALAWI.






LILONGWE-MALAWI,
Siku mija baada ya kutangazwa rasmi kwa kifo cha aliyekuwa rais wa Malawi bw.Bingu wa Mutharika makamu  wa rais wa malawi mama Joyce Banda ameapishwa rasmi na kuwa rais wa nchi hiyo;
Bi Joyce banda anakuwa mwanamke wa kwanza kuwa Rais katika ukanda wa Kusini mwa Sahara baada ya Bi.Helen Johnsen wa Leberia Magharibi mwa Afrika.
kabla ya kuapishwa kwake kulikuwa na hofu kuwa pengine wafuasi wa Marehemu Mutharika wangebadili katiba na kumwapisha kaka wa marehemu Ndugu.Peter Mutharika kutokana na Bi. Banda kufarakana na rais mwaka 2010 na kufukuzwa kutoka katika chama cha DPP na kuunda chake cha People's Party.
Mwanamke huyo alishangiliwa kwa nguvu kabla na wakati wa kuapishwa ndani ya ukumbi wa bunge huko Lilongwe.
Bingu Mutharika alifariki hapo jana kutokana na matatizo ya Moyo.