Sunday, June 02, 2013

MAHAKAMA YA KATIBA YAMWAGIZA MUGAMBE KUPANGA TAREHE YA UCHAGUZI MKUU

Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe akitia saini katiba mpya huku waziri mkuu Morgan Tsvangirai akitazama
(Reuters)

Mahakama kuu ya katiba nchini Zimbabwe imemuagiza rais Robert Mugabe kupanga tarehe ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu wa urais, wabunge na ule wa Serikali za mitaa, kabla ya tarehe 31 ya mwezi July.


Akizungumza na wanahabari mjini Harare Zimbabwe jaji mkuu Godfrey Chidya usiku amesema kuwa mahakama kuu imemuagiza rais Robert Mugabe kuandaa uchaguzi mkuu wa nchi hiyo kabla ya tarehe 31 ya mwezi July mwaka huu.


Uamuzi huo wa mahakama unakuja wakati huu ambapo toka rais Mugabe amesaini na kuwa sheria kuanza kutumika kwa katiba mpya, bado serikali ya umoja wa kitaifa haijatangaza tarehe rasmi ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu licha ya kuwa ilitangazwa kuwa ni mwezi July.

Kufanyika kwa uchaguzi huo kutamaliza utawala wa Serikali ya muungano kati ya chama cha ZANU-PF na kiel cha Upinzani cha MDC kinachoongozwa na waziri mkuu Morgan Tsvangirai ambapo waliunda Serikali hiyo mwaka 2009.

Wananchi wa Zimbabwe wanatarajiwa kushiriki zoezi la uchaguzi mkuu wa nchi hiyo chini ya katiba mpya iliyotiwa saini na rais Mugabe juma moja lililopita na kuwa sheria.

Upinzani na wanaharakati nchini Zimbabwe umekuwa kwa muda mrefu ukipigia kelele kufanyika mabadiliko ya katiba ya nchi hiyo ikiwemo kuwa muhula maalumu kwa rais kukaa madarakani.

Rais Mugabe anatarajiwa kusimama tena kutetea nafasi yake kwenye uchaguzi huo ambapo upinzani chini ya chama cha ZANU-PF unatarajiwa kumsimamisha waziri mkuu Morgan Tsvangirai.

"The first respondent (Mugabe) be hereby ordered and directed to proclaim as soon as possible a date for the holding of presidential elections, general elections and elections of members of governing bodies of local authorities... which elections should take place no later than the 31st of July 2013," Chief Justice Godfrey Chidyausiku said.(RFI)

TANZANIA HAITAIOMBA MSAMAHA RWANDA-MEMBE


DODOMA-TANZANIA,Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe amesema kamwe Tanzania haitaiomba radhi Rwanda, baada ya Rais Jakaya Kikwete kuishauri nchi hiyo kufanya mazungumzo na upinzani ili kumaliza vita katika eneo hilo la Maziwa Makuu.
Serikali ya Rwanda iliitaka Tanzania iombe radhi kwa madai kuwa kauli ya Rais Kikwete ni kama tusi kwao na kwamba wao hawawezi kukaa na kuzungumza wapinzani ambao ni wauaji.
“Kama Rwanda haitaki kufuata ushauri wa Rais Kikwete inatakiwa kuuacha na siyo kumtaka aombe radhi,” alisema.
Membe alitoa ufafanuzi huo bungeni jana wakati akijibu hoja mbalimbali za wabunge katika mjadala wa makadirio ya matumizi ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kwa mwaka 2013/2014.
Tamko hilo la Serikali limekuja ikiwa zimepita takriban siku sita tangu Serikali ya Rwanda kutoa tamko la kupinga ushauri huo uliotolewa na Rais Kikwete wakati akiwa katika sherehe za maadhimisho ya miaka 50 ya Umoja wa Afrika (AU), uliofanyika mjini Addis Ababa, Ethiopia.
Akijibu pendekezo hilo la Rais Kikwete, Waziri wa Mambo ya Nje wa Rwanda, Louise Mushikiwabo alisema kuwa Rwanda haiko tayari kufanya mazungumzo na watu ambao walishiriki kwenye mauaji ya kimbari ya mwaka 1994, dhidi ya Watutsi na kwamba kufanya hivyo ni sawa na kuhalalisha mauaji kwa wananchi wake.
“ Wale wote wanaodhani kuwa Rwanda itaanzisha majadiliano na waasi wa FDLR nadhani kwa ukweli hawajui kile wanachozungumza. Rwanda haiwezi kujadiliana na wauaji,” alisema waziri huyo wakati akizungumza na Idhaa ya Kimataifa ya Radio Ufaransa.
Alisema kuwa wakati serikali ya Rwanda imefaulu kuzika mienendo inayopalilia mauaji ya halaiki, lakini bahati mbaya kumesalia makundi ya watu ambayo bado yanahubiri itikadi zinazokumbusha uchungu na kutonesha kidonda kilicholeta maafa makubwa kwa wananchi.
“ Kumbe kuna wasemaji wengi wa kundi la FDLR. Wengine wao wanaendelea kufungamana na itikadi za kundi hili. Rwanda ilifaulu kutokomeza mauaji ya halaiki lakini hatukutokomeza itikadi za kundi hili,” alisema waziri huyo.
Kauli ya waziri huyo imeungwa mkono na baadhi ya wasomi pamoja na wanaharakati waliosema kuwa kuiomba Rwanda ianzishe majadiliano na kundi hilo, wanapaswa kufikiri mara mbili.
Katika ufafanuzi wake Membe alimnukuu Waziri Mkuu wa zamani wa Israel, Isaack Rabin kwamba mwaka 1995 aliwahi kutoa tamko lililosema, ‘Tunajenga amani na tunajadiliana na maadui zetu na si marafiki’.
Alisema kama Serikali ya Rwanda itakuwa imesikia kauli hiyo inatakiwa kufanya mazungumzo ya amani na maadui, na wasingoje kufanya mazungumzo ya amani na Tanzania, ambayo wana uhusiano mzuri na ni nchi rafiki kwa muda mrefu.