Wednesday, July 18, 2012

HAPPY BIRTHDAY MANDELA!!

http://greencelebrity.info/wp-content/uploads/2012/04/who-is-nelson-mandela-photo-credit-todays-nigeria.jpg

Happy Birthday Mandela!! ndivyo waafrika na wapenda usawa duniani kote tunavyokutakia heri katika siku yako ya kuzaliwa baba wa bara la Afrika mpendwa Nelson Mandela leo unapotimiza miaka 94 tangu ulipozaliwa.

Mchango wako katika kuikomboa Afrika kusini na Afrika nzima kutoka katika mikono ya unyonyaji zitatambuliwa daima! Mungu aendelee kukujalia afya njema Mpendwa Wetu Mandela!

ANGA ZA KIMATAIFA!

MELI NYINGINE YAZAMA TANZANIA

Meli ya SKAGIT iliyokuwa inatoka Dar Es Salam kuelekea Zanzibar ikiwa  imewabeba watu wapatao miambili imearifiwa kuzama katika bahari ya hindi eneo la Chumbe kisiwani Zanzibar.

kwa mujibu wa taarifa za vikosi vya wanamaji , meli hilyo ilianza kupata matatizo baada ya kutokea mawimbi makali.Jeshi hilo la wanamaji nchini Tanzania limeanza shughuli za kuwaokoa watu hao.
 
Polisi nchini Tanzania wamethibitisha kutokea kwa ajali hiyo,ingawa hawajathibitisha idadi kamili ya abiria waliomo kwenye meli hiyo.

WAZIRI WA ULINZI WA SYRIA AUAWA KATIKA MLIPUKO.

Waziri wa Syria aliyeuawa Bw.Daoud Rajha


DAMASCUS-SYRIA,
Waziri wa ulinzi wa Syria na Bw.Daoud Rajha na naibu wake Bw.Assef Shawkat, wameuawa katika mlipuko wa bomu baada ya mlinzi kujitoa mhanga huko Damascus. 

Kwa mujibu wa Televisheni ya Syria waziri huyo wa ulinzi na naibu wake ambaye pia ni shemeji wa Rais Assad wameuawa wakati wakihudhuria mkutano wa mawaziri na wanausalama.Vyanzo vya usalama vya Syria vimesema mlinzi huyo ni wa ngazi ya juu katika nafasi ya ulinzi.


Katika mlipuko huo waziri wa mambo ya ndani bw. Mohammad Ibrahim al-Shaar pamoja na maafisa kadhaa wamejeruhiwa pia, ingawa vyanzo vya habari vimesema rais Assad hakuwepo katika mkutano huo.




Mlipuko huo umekuja wakati mapigano katika mji mkuu wa Syria yakiingia siku ya nne kati ya majeshi ya serikali na waasi wanaowania kuuangusha utawala wa miongo minne(4) wa Rais Assad.
Vifo hicho vimeelezewa kuwa pigo kubwa kwa Rais Assad na serikali yake inayopigana kufa na kupona kubaki madarakani licha ya mashinikizo ya kimataifa kumtaka rais huyo kuachia ngazi