ZANZIBAR-TANZANIA,
Mhina amesema kwa sasa kiini cha shambulizi hilo hakijajulikana, lakini polisi inafanya msako wa kuwanasa majambazi hao. Mnamo siku ya Krismasi, watu waliokuwa na bunduki walimpiga risasi na kumjeruhi vibaya kasisi wa kikatoliki wakati akirejea nyumbani kutoka kanisani.
Haijabainika kama mashambulizi hayo mawili yanahusiana, au ikiwa yamechochewa na hisia za kidini. Mwezi Novemba mwaka jana, washambuliaji walimmwagia kemikali usoni na kifuani mhubiri mmoja wa kiislamu, na kumekuwa na hofu baina ya jamii hizo mbili kisiwani Unguja.