Friday, May 24, 2013

"RAMA MLA WATU" AACHIWA HURU-KUPELEKWA DODOMA.


DAR ES SALAAM-TANZANIA,
Mahakama kuu kanda ya Dar es Salaam imeamua kumuachia huru Ramadhani Selemani Mussa ambaye alikuwa akikabiliwa na kesi ya kukutwa na kichwa cha mtu. Rama, ambaye muda wote huo alikuwa rumande gereza la Segerea akisota kusubiri hukumu yake, alikamatwa hospitali ya Muhimbili mwaka 2008 ambapo pia alikiri kuwa alikuwa na tabia ya kula nyama za watu ambayo amefundishwa kichawi toka alipokuwa mdogo. Mahakama imemuachia huru kwasababu mtuhumiwa alitenda kosa hilo pasipo kuwa na akili timamu. Hata hivyo mahakama hiyo imetoa agizo la kuendelea kumuweka kijana huyo katika hospitali ya wagonjwa wenye matatizo ya akili, hospitali ya Isanga iliyopo Dodoma mpaka pale atakapona ndipo aruhusiwe kurudi mtaaani.habari kutoka karibu ndani

MAELFU WAJITOKEZA KUMZIKA CHINUA ACHEBE,

Melfu ya waombolezaji walijitokeza kwa mazishi ya mwandishi mashuhuri wa nchi hiyo marehemu Chinua Achebe, katika jimbo la Anambra.
Wageni mashuhuri akiwemi, rais Goodluck Jonathan pia hawakuachwa nyuma,
Mamia ya watu walikusanyika kanisani baadhi wakivalia mavazi ya kitamaduni yenye picha ya Achebe.
Marehemu Achebe alisifika sana kama baba mwanzilishi wa fasihi ya kiingereza barani Afrika.
Mwili wa mwandishi mashuhuri wa vitabu barani Afrika Chinua Achebe uliwasili nyumbani kwake katika jimbo la Anambra nchini Nigeria siku ya jumatano.
Mwandishi wa BBC aliyekuwepo kwenye mazishi hayo alisema kuwa Achebe alipewa mazishi ya kiheshima, mjini Ogidi.
Hata hivyo, baadhi ya mambo aliyochukizwa nayo ikiwemo vubaraka wa kisiasa na mali wanayojilimbikizia, yalishuhudiwa katika mazishi yake.
Wanasiasa walisindikizwa kanisani na maafisa wa usalama wakiwa na sialaha za kisasa. Baadhi pia waligika wakiwa wamavalia mavazi yenye rangi ya vyama vya kisiasa.
Hafla mbali mbali ziliandaliwa nchini Nigeria kumuenzi bwana Achebe kabla ya mazishi yake kufanyika.
Mwandishi huyo mashuhuri alifariki mjini Boston,Marekani, akiwa na umri wa miaka 82 baada ya kuugua kwa muda mfupi.

Hayati Achebe, anasifika sana kwa kuwa mwanzilishi wa fasihi ya kiafrika kwa kiingereza.
Kitabu chake alichokianda cha kwanza, mwaka 1958, 'Things Fall Apart', ambacho kilizungumzia sana athari za ukoloni barani Afrika, aliweza kuuza zaidi ya vitabu milioni kumi.
Mwandishi huyo na msomi, aliendelea na uandishi wake na kuandika vitabu vingine 20 baadhi vikikosoa sana wanasiasa na kile alichokitaja kama ukosefu wa uongozi nchini Nigeria.
Alikuwa anaishi nchini Marekani tangu mwaka 1990 baada ya ajali ya barabarani kumjeruhi kiasi cha kumlemaza.
Makundi ya kitamaduni yalifanya tamasha mbali mbali nje ya uwanja wa ndege wa Enugu, huku ndege iliyokuwa inambeba marehemu Achebe ilipotua.
Inaarifiwa kuwa licha ya kuwa watu wana majonzi tele, lakini pia wanasherehekea maisha ya mwandishi huyo.
Achebe atazikwa karibu na nyumbani kwa familia yake mjini Ogidi, mji mdogo kwenye vilima vya jimbo la Anambra

UMOJA WA AFRIKA(A,U) WATIMIZA MIAKA 50,



ADDIS ABABA-ETHIOPIA,Wageni mashuhuri na marais wa Afrika wameanza kuwasili mjini Addis Ababa Ethiopia kwa sherehe za kuadhimisha miaka hamsini tangu kuanzishwa kwa Muungano wa Afrika.

Muungano wa Afrika wakati huo ukijulikana kama OAU,uligeuza jina na kujulikana kama AU mnamo mwaka.

Kauli mbiu ya sherehe za hapo kesho ni mjadala mkuu kuhusu ushirikiano wa nchi za Afrika na kuimarishwa kwa muungano huo.Hapo kesho Jumamosi kutakuwa na sherehe za kilele kuadhimisha miaka hamsini ya AU na Zitahudhuriwa na rais wa Kenya Uhuru Kenyatta pamoja na marais wengine wa Afrika.

Mwenyekiti wa tume ya muungano huo, Dr Nkosazana Dlamini Zuma, anaseme kuwa hii itakuwa fursa kwa AU kujadili kuhusu uwezo wa bara hili na ambacho kinaweza kufikiwa katika miaka hamsini ijayo.

Sherehe za AU zinakuja wakati swali kuu kwa AU ni kesi zinazowakabili washukiwa wakuu wa ghasia za baada ya uchaguzi wa Kenya mwaka 2007/08 Rais Uhuru Kenyatta na naibu wake William Ruto pamoja na mtangazaji wa redio Joshua Arap inaendelea katika mahakama ya kimataifa ya ICC.

Duru zinasema kuwa huenda mawaziri wa mambo ya kigeni wa nchi za Afrika wamekubaliana kuhusu azimio linalotaka kesi ya washukiwa hao kurejeshwa Kenya ambako inaweza kusikilizwa na hatua kuchukuliwa dhidi ya watakaopatwa na makosa.

Shereha hizi pia zinakuja wakati bara la Afrika linashuhudia migogoro nchini Mali, DRCongo huku Misri ikiwa bado haijatengamaa baada ya kufanyika mapinduzi ya kiraia yaliyomng'oa mamlakani aliyekuwa rais Hosni Mubarak.

Lakini mwenyekiti wa AU ana matumaini kuwa Afrika iko kwenye mkondo mzuri wa kimaendeleo.

Katika hotuba yake wakati wa ufunguzi wa mkutano wa 21 wa AU, Dlamini Zuma alisema kuwa Afrika imekuwa kiuchumi katika muongo mmoja uliopita, imeshuhudia maendeleo ya kiuchumi , ustawi wa kikanda , uimarishwaji wa miundo mbinu na ushirikiano wa kikanda.

Sherehe hizi ambazo zitafuatwa na mkutano wa siku mbili wa marais wa AU, zitatoa fursa kwa wananchi wa bara la Afrika kuangazia ufanisi wa Muungano huo.