Thursday, October 30, 2014

Burkina Faso:Jeshi lachukua mamlaka

Bunge la Burkina Faso limetekezwa moto
Amiri jeshi mkuu wa jeshi la Burkina Faso <span > Jenerali Honore Traore ametangazwa kuvunjwa kwa serikali na bunge la taifa.
<span >Jenerali Traore hata hivyo hakutangaza ni nani atakayechukua uongozi wa taifa hilo.
Jenerali Traore aliwaambia waandishi wa habari kuwa kutaundwa serikali ya mpwito baada ya kufanyika mazungumzo baina ya wanasiasa wa upinzani na kiongozi Bwana Campaore.
Jenerali Traore alikuwa akiwahutubia waandishi wa habari baada ya kushuhudia fuzo la maandamano katika mji mkuu wa <span >Ouagadougou.
Mmoja wa wabunge nchini Burkina Faso akitorokea kuokoa maisha yake.
<span >Waandamanaji walivamia majengo ya bunge na majumba ya wafuasi wa rais<span >Blaise Compaore wakipinga azimio lake la kutaka kubadilisha katiba ya taifa ilikumruhusu kuwania kipindi kingine cha uongozi baada ya kutawala kwa zaidi ya miaka 27.
Awali <span >Waandamanaji waliteketeza majengo ya Bunge mjini Ougadougou, na kuwafurusha wabunge .
Runinga ya itaifa ililazimika kusitisha matangazo baada ya waandamanaji kuvamia shirika la utangazaji.
Waandamanaji kisha wameelekea Ikulu ya Rais na wanajeshi wamekua wakiwafyatulia risasi.
Vilevile baraza la jiji pamoja na makao makuu ya chama tawala yameteketezwa moto.
Umati mkubwa wa watu umeonekana ukielekea ikulu ya Rais huku uwanja wa ndege ukifungwa.
Rais Blaise Compaore ameomba utulivu ,katika ujume aliotumwa kwa Twitter.
Wabunge wamelazimika kuahirisha kura hiyo ya kubadilisha katiba kumkubalia Compaore kuwania tena Urais mwaka ujao.
Uharibifu katika majengo ya serikali Ougadougou
Watu watano wameuawa katika maandamanao hayo ambayo yametajwa kuwa mabaya zaidi kukumba utawala wa Blaise Compaore.
Awali wanajeshi waliwafyatulia risasi waandamanaji waliovamia majengo ya bunge.
Compaore alitwaa madaraka kupitia mapinduzi mwaka wa 1987.
Amekua akishinda uchaguzi lakini kura hio hukumbwa na utata.
Ufaransa na muungano wa Ulaya zimemuomba Rais Compaore kutobadilisha katiba ili kuwania tena.

WANAFUNZI WA KAMBANGWA WAENDELEA KUNUFAIKA NA MRADI WA KOMPYUTA WA VODACOM NA SAMSUNG



 .Wanafunzi wa kidato cha pili katika shule ya sekondari ya Kambangwa iliyopo Kinondoni jijini Dar es Salaam,wakioneshwa na Meneja miradi  na Mawasiliano wa Vodacom Foundation Renatus Rwehikiza moja ya progamu zinazopatikana katika Kompyuta zinazowawezesha kupata taarifa ya masomo mbalimbali kwa njia ya mtandao  wakati alipotembelea shuleni hapo kwa ajili ya kujua  maendeleo ya mradi wa TEHAMA  uliofadhiliwa na Vodacom Foundation  kwa kushirikiana na Kampuni ya Samsung.Zaidi ya wanafunzi elfu tano wa shule nne za sekondari  jijini wanaendelea kunufaika na mradi huo.
 Mwalimu Mkuu wa Shule ya sekondari ya Kambangwa iliyopo Kinondoni jijini Dar es Salaam  Theresia Ng’wigulu (kulia) Meneja miradi  na Mawasiliano wa Vodacom Foundation Renatus Rwehikiza(kushoto ) pamoja na Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania Matina Nkurlu (katikati)wakimsikiliza mmoja wa wanafunzi wa kidato cha pili katika shule ya sekondari ya Kambangwa,Matha Galus akiwaelezea jinsi anavyoweza kupata taarifa za masomo mbalimbali kwa njia ya mtandao, wakati walipotembelewa na maofisa wa Vodacom shuleni hapo kujua   maendeleo ya  mradi wa TEHAMA  uliofadhiliwa na Vodacom Foundation  kwa kushirikiana na  Samsung.Zaidi ya wanafunzi elfu tano wa shule nne za sekondari  jijini wanaendelea kunufaika na mradi huo.
 Mwalimu Mkuu wa Shule ya sekondari ya Kambangwa iliyopo Kinondoni jijini Dar es Salaam  Theresia Ng’wigulu (kulia) Meneja miradi  na Mawasiliano wa Vodacom Foundation Renatus Rwehikiza(kushoto ) pamoja na Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania Matina Nkurlu (katikati)wakimsikiliza mmoja wa wanafunzi wa kidato cha pili katika shule ya sekondari ya Kambangwa,Matha Galus akiwaelezea jinsi anavyoweza kupata taarifa za masomo mbalimbali kwa njia ya mtandao, wakati walipotembelewa na maofisa wa Vodacom shuleni hapo kujua   maendeleo ya  mradi wa TEHAMA  uliofadhiliwa na Vodacom Foundation  kwa kushirikiana na  Samsung.Zaidi ya wanafunzi elfu tano wa shule nne za sekondari  jijini wanaendelea kunufaika na mradi huo.
 Baadhi ya Wanafunzi wa kidato cha pili katika shule ya sekondari ya Kambangwa iliyopo Kinondoni jijini Dar es Salaam na Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Theresia Ng’wigulu watatu toka kulia pamoja na maofisa wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu wa kwanza kushoto na Renatus Rwehikiza(kulia)wakimsikiliza Mwalimu wa somo la kompyuta wa kidato cha pili Nicolas Wilson wa shule hiyo akiwafafanulia jambo kuhusiana na elimu ya mafunzo ya kompyuta wakati walipotembelewa na maofisa hao kujua  maendeleo ya mradi wa TEHAMA  uliofadhiliwa na Vodacom Foundation  kwa kushirikiana na Kampuni ya Samsung.Zaidi ya wanafunzi elfu tano wa shule nne za sekondari  jijini wanaendelea kunufaika na mradi huo.
Wanafunzi wa kidato cha pili wakiwa darasani katika shule ya sekondari ya Kambangwa iliyopo Kinondoni jijini Dar es Salaam,wakiwa na nyuso za furaha walipotembelwa na Maofisa toka Vodacom Foundation kwaajili ya kujionea maendeleo ya mradi wa TEHAMA  uliofadhiliwa na Vodacom Foundation  kwa kushirikiana na Kampuni ya Samsung.Zaidi ya wanafunzi elfu tano wa shule nne za sekondari  jijini wanaendelea kunufaika na mradi huo.
------------------
Wanafunzi waendelea kunufaika na mradi wa elimu ya kompyuta wa  Vodacom na Samsung
“Tumekuwa tukijifunza  somo la kompyuta kwa nadharia  kabla ya mradi wa  Samsung Smart kuanzishwa hapa shuleni kwetu,baada ya kuanzishwa hivi  sasa tunasoma somo la kompyuta kwa vitendo na ndoto yetu ya kuingia katika ulimwegu wa sayansi na teknolojia imetimia”Anasema John Mwasha mwanafunzi wa shule ya  sekondari ya Kambangwa iliyopo wilayani Kinondoni mkoani Dar es Salaam akiwakilisha wenzake.
Mwanafunzi mwingine  kutoka shule hiyo Mariam Abdallah amesema kuwa  ipo idadi ya wanafunzi wengi mijini na vijijini wanamaliza elimu ya sekondari  bila kujua matumizi ya kompyuta kiasi kwamba kifaa hiki wanakiona kama ni kigumu sana kukitumia, na kuongeza kuwa mradi huu ni muhimu katika shule za Tanzania na umeweza kuwaingiza katika ulimwengu wa teknolojia ya kompyuta.
Mradi huu ambao umeanzishwa   kwa ushirikiano wa Vodacom na Samsung umeanzia katika shule nne za mkoa wa Dar es Salaam ambapo shule hizo zimepatiwa msaada wa kompyuta za kufundishi wanafunzi,kujengewa darasa la kusomea somo  hilo pia kupatiwa jenereta inayomia teknolojia  ya mionzi ya jua kwa ajili ya kutoa nishati ya umeme kwenye shule hizo.
Mwalimu Mkuu wa sekondari ya Kambangwa,Bi.Theresia Mwigulu, amesema mradi huu ni muhimu na umewawezesha wanafunzi katika shule yake kuingia katika ulimwengu wa kompyuta na hivi sasa wanaweza kumudu vizuri somo hilo kwa kuwa wanalisoma kwa  nadharia na vitendo.
“Baada ya kupata mradi huu,somo la kompyuta imekuwa ni rahisi kulifundisha kwa nadharia na vitendo pia walimu na wanafunzi wamekuwa  wakipata  taarifa na maarifa ya kufundishi masomo kutoka katika mtandao wa  internet.Huu mradi  unaweza kuleta mabadiliko  makubwa kielimu ukisambaa katika shule zote nchini”Amesema Mwigulu.
Kwa upande wake Meneja wa Mradi na Mawasiliano wa Vodacom Foundation Renatus Rwehikiza amesema kuwa amepata faraja baada ya kutembelea shule hiyo na kukuta wanafunzi wanaendelea kunufaika kwa kupata maarifa ya kutumia kompyuta na kupata habari na elimu kutoka sehemu mbalimbali duniani kupitia mtandao wa internet.
“Mawasiliano mazuri huwezesha watu kupata taarifa mbalimbali  zinazotokea  katika mazingira yao walipo na sehemu za mbali kwa urahisi.Kwa wanafunzi kompyuta zinasaidia sana kupata maarifa kupitia mtandao wa internet.Nawahasa msome kwa bidii  na mtumie  vizuri fursa hii kutafuta elimu na msiogope kusoma masomo ya sayansi maana mambo yote  hivi sasa yamerahisishwa kupitia teknolojia hii ya kompyuta”.Alisema.
Mradi huu ulizinduliwa rasmi mwaka 2013 Kati ya ushirikiano wa kampuni ya Samsung na Vodacom Foundation na shule zingine za  sekondari zitakazonufaika na mradi huu ni Kinyerezi,Makumbusho na Mtakuja beach.