Saturday, February 11, 2012

NI GHANA VS MALI KUTAFUTA MSHINDI WA TATU AFCON.

Malabo-GUINEA YA IKWETA, Kikosi cha Mali

Kikosi cha Ghana

Ghana inaivaa Mali leo hii katika mechi ya kumtafuta mshindi wa tatu wa michuano ya Mataifa ya Afrika bila wachezaji wake wanne tegemeo katika mji mkuu wa Guinea ya Ikweta Malabo.

Kiungo wa kati Derek Boateng ana kadi nyekundu aliyoipata kwenye mechi iliyopita dhidi ya Zambia, beki wake wa kati John Boye anakadi mbili za njano katika mechi mbili zilizopita, wakati Kapteni John Mensah na Kiungo mwingine Emmanuel Badu ni Majeruhi.

Ghana imeingia katika nafasi hiyo baada ya kupoteza mchezo wake dhidi ya Zambia na Mali walipoteza dhidi ya Ivory Coast katika nusu fainali.
Ghana ambao mafanikio yao yalikuwa juu katika miaka ya hivi karibuni kutokana na kutinga kuvunjika moyo baada ya kushindwa kufika Fainali katika michuano ya mwaka huu.


Mali kwa Upande wao wanajipongeza kwa kufikia hatua hiyo bila ya nyota wao wa kipindi kilichopita Fredrik Kanoute, Mamadou Diarra na Mamadou Sissoko, huku wakiegemea kupata faida ya kukosekana kwa wachezaji hao muhimu wa Ghana.
.
Hata hivyo mchezo huo unategemewa kuwa wa ushindani ambapo ghana wana kumbu kumbu ya Kuwafunga Mali magoli 2-0 katika hatua ya makundi.


ROONEY AIPAISHA MAN UNITED KILELENI.




Wayne Rooney amefunga mara mbili katika ushindi wa magoli 2-1 wa Manchester United dhidi ya Liverpool kwenye Uwanja wa Old Traford na kuisaidia timu yake hiyo kukwea kileleni mwa ligi hiyo.

katika Mechi hiyo ambayo ilishuhudia Manchester United wakitawala sehemu kubwa ya kipindi cha pili Rooney alifunga goli la kwanza katika dakika ya 47 baada ya kona na kuongeza goli la pili katika dakika ya 50 huku goli la liverpool likifungwa na Luis Suarez katika dakika ya 80 .

Katika mechi hiyo pia kulishudiwa muendelezo wa uhasimu kati ya Mchezaji Luis Suarez wa Liverpool na Patrice Evra wa manchester united Baada ya mchezaji huyo wa Liverpool kukataa kupeana mikono.

Kwa matokeo hayo Manchester United Imeshika Usukani wa ligi hiyo ikiwa na pointi 58 mbele ya Manchester City wenye Pointi 57 wakiwa na mchezo mmoja mkononi wakati liverpool wao wanabaki na pointi zao 39 katika nafasi ya 7.

IRAN KUTANGAZA MAFANIKIO YAKE KATIKA MPANGO WAKE WA NYUKLIA.

 TEHRAN-IRAN,

Rais wa Iran Ahmadinejad amesema hivi karibuni nchi yake itatangaza mafanikio makubwa iliyoyapata katika mapango wake wa nyuklia.akihutubia makumi ya maelfuya watu   katika sherehe za kutimiza miaka 79 ya mapinduzi ya nchi Ahmedinedjad amesema katika siku zijazo dunia itashuhudia kutangazwa kwa tangazo muhimu la mafanikio ya Iran katika mradi wake wa Nyuklia bila kufafanua zaidi.

 Wafuasi wa Rais huyo wakiwa wamebeba bendera za Iran na picha za mwanamapinduzi na  kiongozi mkuu wa kidini Bw Ayatollah ali Khamenei walipaza sauti zao kwa maneno ya kuzilaani Israel na Marekani.
Naye kiongozi wa kundi la Hamas Ismail Haniyeh aliyekuwa moja wa waalikwa katika sherehe hizo amesema kamwe Hamas hawataitambua Israael kama taifa, kiongozi huyo amesema ingawa wapinzani wao wanawataka kuacha upinzani dhidi ya Israel na kutambua uvamizi wa Israel kamwe hawatofanya hivyo kama wawakilishi wa Wapalestina.

 Sherehe hizo  zilikuwa za kukumbuka mapinduzi ya serikali iliyokuwa ikiungwa mkono na Marekani ya rais Sha Mahammad Reza Pahlavi yaliyotokeaa  Mnamo mwezi Februari 11, 1979 ambayo yalifuatiwa na Uundaji wa taifa la kiislamu chini ya Kiongozi Ayatollah Ruhollah Khomeini.