Sunday, April 22, 2012

SUDAN YA KUSINI YAFUNGA USAFIRISHAJI WA MAFUTA KWENDA SUDANI YA KASKAZINI.

JUBA/ADDIS ABABA, Sudan ya kusini leo imefunga rasmi usafirishaji wa mafuta yake kuelekea Sudani ya Kaskazini hadi pale matakwa yake yatakapotekelezwa.matakwa yanayohusiana na kulipwa deni lake la dola bilioni 2.4, kuacha kuwasaidia waasi na kuachia eneo linalogembewa na mataifa hayo mawili la Abyei pamoja na kuchorwa kwa mpaka kamili wanchi hizo mbili.   
              Akiongea kwa niaba ya Serikali yake waziri wa mafuta  wa Sudan ya Kusini Bw.Stephen Dhieu Dau amesema Sudan ya kusini imesimamisha usafirishaji wa mapipa yapatayo 350,000 kwa siku kwenda Sudan kaskazini " ufungaji huo ni asilimia 100 na usafirishaji wake utaanza mpaka pale makubaliano yatakapofikiwa na kusainiwa' alisema waziri huyo.Waziri huyo alisema Sudan ya kaskazini ni lazima iheshimu mipaka iliyaokubaliwa mwaka 1956 na hivyo kurudisha maeneo yote iliyoyapora kutoka kwa Sudan ya Kusini.


               Akiongea katika baraza la umoja wa Afrika katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa bw. Ban ki moon alisema ana wasi wasi kuwa mgogoro huo utapelekea matumizi ya silaha na kuleta vita na akawalaumu marais wa nchi hizo mbili kwa kushindwa kufikia makubaliano.


               Sudan ya kaskazini ambayo imepata uhuru wake mwaka jana mwezi julai inaituhumu Sudan ya kusini kwa Kuipokonya eneo la abyei ambalo lina utajiri wa mafuta kwa kuweka vikosi vyake tangu mwaka jana, pia kwa kukisaidia kikundi cha Sudan People's Liberation Movement North (SPLM-N) kinachoipinga serikali ya Sudan Kusini pia inalalamikia gharama za usafirishaji mafuta inazotozwa na Sudan ya Kaskazini ambayo ndio mmiliki wa mabomba yanayosafirisha mafuta hayo licha ya Sudan ya Kaskazini kumiliki robo tatu ya eneo hilo. marais wa nchi hizo walikutana ijumaa iliyopita na kushindwa kufikia makubaliano.



Rais wa Benin Thomas Boni Yayi, achaguliwa kuwa Mwenyekiti Mpya wa Umoja wa Afrika.

  Adis Ababa,Ethiopia,

  Viongozi kutoka nchi 54 za afria wamemchagua rais wa benin Bw. Thomas                                               Boni Yayi kuwa mwenyekiti mpya wa Umoja huo akimbadili rais wa  Guinnea ya Ikweta bw. Teodoro Obiang Nguema aliyetumikia kwa mwaka mmoja uliopita. Akipokea wadhifa huo Rais huyo ameelezeaa furaha yake yakupewa heshima hiyo na kuahidi Kudumisha amani barani Afrika.


   Baraza hilo la umoja wa Afrika Linalokutana  kwa muda wa siku mbili mjini Adis Ababa kesho linatarjiwa kumchagua mkuu wa baraza la usalama na Amani ambaye pia atakuwa anampokea wadhifa huo ndugu
Jean Ping kutoka Gabon aliyekuwa madarakani tangu mwaka 2008, anayegombea nafasi hiyo ni mke wa zamani wa rais wa sasa Afrika kusini Bw.Jacob Zuma mama  Nkosazana Dlamini-Zuma ambaye pia ni waziri wa mambo ya ndani ya Afrika kusini.Afrika kusini imesema inaimani mama huyo atshinda na kuchukua wadhifa huo kutoka kwa Bw. jean Ping.

                                                                                                                                                                     Katika mkutano huo wa 18 wa kilele ajenda muhimu zinazojadiliwa ni pamoja na kuimarishwa bishara Afrika, mzozo wa Somalia, mgogoro wa mafuta kati ya Sudan na Suda kusini na pia suala la viongozi wa Afrika kung'ang'ania madaraka.  




MAJESHI YA SYRIA YAPAMBANA NA WAASI KARIBU NA DAMASCUS

SYRIA -Ikiwa ni miezi kumi tangu kuanza kwa maandamano ya kupingwa kwa utawala wa Rais Bashar Al-assad wa Syria mapigano yameripotiwa karibu na mji mkuu wa Damascus huku Douma tangu leo asubuhi. Imedaiwa waasi wamesogea mpaka eneo hilo wakielekea mji mkuu wa nchi hiyo huku gavana wa jimbo hilo akiongelea juhudi za kusitisha mapigano na kuzungumza  "Wengi tumezungumza nao na wameondoka natumaini wakirudi watarudi na njia nzuri" alisema gavana Hussein Makhloufa  alipokuwa akiongea na waangalizi kutoka Umoja wa nchi za kiarabu kabla hawajaingia katika mi mkuu wa nchi hiyo katika maeneo yenye vurugu.

             Jeshi la serikali tayari lipo eneo hilo na limeanza operesheni ya nyumba kwa nyumba kuwakamata watu linaowashuku kuhusika na uasi, ambapo waandishi wa habari walioneshwa silaha za Mabomu zilizotengenezwa kienyeji ambazo jeshi hilo limezikamata kutoka kwa wananchi.

Hata hivyo kikundi pinzani kinachoangalia haki za binadamu nchini Syria kimesema Serikali imewakamata watu 200 katika uvamizi huo wa Douma ambao ni moja ya miji yenye upinzani mkali kwa rais Al-assad.

Imedaiwa kikundi cha The Free Syrian Army (FSA) kimekamata baadhi ya maeneo ya Damascus, hallasta na Douma ingawa bado kinapata upinzani mkali kutoka kwa majeshi yenye silaha kali ya Serikali kama anavyokiri mmoja wa wapiganaji wa waasi kwa jina Abu Thaer. amabye anasema jeshi la nchi lina silaha kali ikiwamo ndege na magari ya kivita wakati wao wanabunduki aina ya Riffle, na mabomu madogo madogo.


Syria imekuwa katika machafuko kwa miezi kumi sasa ambapo wananchi wanomppinga rais wa nchi hiyo wanapambana na vikosi vya usalama kumtaka aondoke madarakani.