Sunday, July 29, 2012

MGOMO WA WALIMU WATHIBITISHWA -Kuanza kesho .

 

TANZANIA,
CHAMA cha Walimu Tanzania (CWT) kimethibitisha kuwepo kwa mgomo wa walimu Tanzania kuanzia

hapo kesho licha ya serikali kutangaza kuwa mgomo huo ni batili.

Rais wa CWT, Gratian Mukoba amesema kuwa Baraza la CWT lilitoa notisi ya saa 48 ambazo zimemalizika leo mchana na hivyo kesho mgomo utakuwepo na walimu watatakiwa kubaki majumbani kwao bila kwenda kazini. Mukoba pia alisisitiza kuwa mgomo huo ni halali kwani wananachama waliopiga kura kuhalalisha  mgomo walikuwa 153,000  ambapo kati ya 183,000   wakiwa sawa na asilimia 95.7 ya wanachama na hivyo kuhalalisha mgomo huo.


Rais huyo alimewataka walimu kutokuwa na hofu na ajira zao kwani mgomo huo umezingatia sheria.
Walimu wameingia katika mgomo huo wakiwa na  madai ya ongezeko la mishahara kwa asilimia 100, posho ya kufundishia kwa walimu wa Sayansi asilimia 55, asilimia 50 pamoja na posho kwa walimu wa masomo ya  sanaa na posho kwa  walimu wanaoishi katika mazingira magumu.

KAMATI YA NISHATI NA MADINI YAVUNJWA-Sababu ni ufisadi.

TANZANIA,
Kamati ya nishati na madini imevunjwa kwa tuhuma za ufisadi ndani ya Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), kitangaza uamuzi huo spika wa Bunge la jamhuri ya Muungano wa Tanzania Anna Makinda alisema vitendo kama hivyo havikubaliki hivyo anaivunja kamati hiyo ya nishati na madini na kupeleka pia suala hilo kwenye Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kwa hatua zaidi ikiwemo uwezekano wa kutajwa kwa wabunge wanaohusika katika sakata hilo.

Hatua hiyo ilifuatia hoja ya Mbunge Vita Kawawa wa jimbo la Namtumbo(CCM) aliyeomba Mwongozo wa Spika, akitaka jambo hili lijadiliwe na Bunge na Kamati za Bunge zinazotuhumiwa kwa rushwa zivunjwe, hoja ambayo iliungwa mkono na spika huyo na kuvunja kamati hiyo.
Habari za fununu kutoka  Dodoma zimeeleza kuwa katika mlolongo huo wapo pia wabunge  wanaotoka katika Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini, na wengine kutoka Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma.
Wabunge waliochangia waliomba uchunguzi zaidi ufanyike na hatua kali za kisheria zichukuliwe dhidi ya watuhumiwa.

MAJESHI YA SYRIA YAWASHAMBULIA WAASI KWA NDEGE.

http://s1.reutersmedia.net/resources/r/?m=02&d=20120729&t=2&i=635702901&w=&fh=&fw=&ll=700&pl=300&r=CBRE86R0GDQ00
Mtoto akiangalia nyumba iliyobomolewa kwa mashambulizi.

http://s1.reutersmedia.net/resources/r/?m=02&d=20120729&t=2&i=635702669&w=&fh=&fw=&ll=460&pl=300&r=CBRE86R1M9B00
Askari wa waasi akipita karibu na jengo lililobomolewa na ndege za jeshi la serikali.
SYRIA,
Vikosi vya serikali vimeripotiwa kuwashambulia waasi kwa helikopta za kijeshi na makombora asubuhi ya jumapili ya leo katika mapigano makali ya kugombea udhibiti wa mji wa pili wa Aleppo.Wanaharakati wameripoti mapigano katika baadhi ya Wilaya na vitongoji katika jiji hilo la kibiashara.

Msuluhishi wa mgogoro huo Bw.Koffi Annan na viongozi wengine wamesema hali katika mji wa Aleppo
 inaonesha umuhimu wa kumaliza mgogoro wa Syria.Kiongozi wa Baraza la kitaifa la Syria ambalo ni muunganiko wa vikundi vya upinzani dhidi ya serikali ya Syria Bw.Abdelbasset Sida amezitaka nchi marafiki na washirika wa Syria kuachana na baraza la Ulinzi la Umoja wa mataifa na badala yake waingie wenyewe Syria kuung'oa utawala wa rais Bashar al-Assad.
   
Mapigano nchini Syria yamedumu kwa takribani miezi 16 na kuua maelfu ya watu na hali hivi sasa ni ya vita nchini humo ambapo vikosi vya waasi vinapigana na majeshi ya serikali kuung'oa utawala wa rais  al-Assad.