Tuesday, May 01, 2012

JENERALI NTAGANDA ATEKA MIJI MIWILI DRC CONGO.

DRC-CONGO,Vikosi vinavyomtii Bosco Ntaganda, anayetafutwa na ICC vimeteka miji miwili ya mashariki mwa DRC.
Mwandishi wa BBC katika eneohiloanasema maelfu ya watu wanakimbiamapigano makali na kuelekea karibu na mjini Goma.
Mamia ya askari wenye silaha nzito wanaomtii Jenerali Ntaganda hivi karibuni walijitenga kutoka jeshi la nchi hiyo.
Akiwa anafahamikakama‘Terminator,’ Jenerali Ntaganda ameklanusha tuhuma za ICC kuwa aliwasajili watoto kuwa askari.


Mwandishi wa BBC Thomas Hubert akiwa Sake, kilometa 30 (18 maili) magharibi mwa Goma, anasema wakazi wamemwambia wamesikia mapigano kati ya vikosi vya Jenerali Ntaganda na vikosi vya serikali yakiendelea Jumapili usiku.
Askari wa serikali walirudishwa nyuma na kuondolewa katika miji ya Mushake na Karuba, mwandishi wetu anasema, na wamerudi nyuma kwa kilometa 12 mashariki mwa mji wa Sake, ambako wanajikusanya kupambana naye.
Askari hao waasi walikimbia jeshi la Congo lenye ngome yake Goma mapema mwezi huu, idadi kati ya 400-500, kwa mujibu wa vyanzo vya UN na Majeshi ya DRC.

‘NTAGANDA NI NANI?’

  • Alizaliwa mwaka 1973 nchini Rwanda
  • Alikimbilia DR Congo akiwa kijana baada ya mashambulizi dhidi ya kabila la Watutsi
  • Akiwa na miaka 17, anaanza siku za mapigano –akibadilisha kati ya waasi na askari, kote Rwanda na DR Congo
  • Akawachezaji wa kujitoa wa tennis
  • Mwaka 2006, alishtakiwa ICC kwa tuhuma za kusajili watoto kuwa askari.
  • Ni kiongozi wa vikosi vilivyofanya mauaji ya Kiwanji mwaka 2008
  • Mwaka 2009, anaujiunga na jeshi la Taifa la DRC na kuwa jenerali.
  • Mwaka 2012, anaasi jeshi na kujitenga.
Katika mapigano mengine katika eneo la kaskazini la Kivu ya kaskazini kati ya majimbo ya Mweso na Kitchanga, maafisa wa jeshi laCongowalimweleza mwandishi wa BBC kuwa wamesimamisha shughuli za watu wa Jenerali Ntaganda.
Kati ya mwaka 2002-2005, Jenerali Ntaganda alikuwa mkuu wa harakai za kijeshi wa waasi wa UCP wakiongozwa na mbabe wa kivita Thomas Lubanga – ambaye mwezi Machi alikuwa wa kwanza kukutwa na hatia na mahakama ya ICC baada ya kukutwa na hatia ya kusajili watoto kuwa aksari.
Jen Ntaganda mtuhumiwa mwenza – lakini Rais Joseph Kabila awali alikataa kukamatwa kwake kwa ajili ya amani ya DRC.
Rais mapema mwezi huu alitoa wito wa kukamatwa kwake lakini anasema hatampeleka ICC.
Licha ya kumalizika kwa vita vya DRC mwaka 2003, makundi kadhaa yenye silaha bado yanazunguka katika eneo lenye utajiri mkubwa wa madini mashariki mwa nchi lichaya UN na jeshi la nchi hiyo kuwanyang’anya silaha.(Habari kwa hisani ya BBC)


SIKUKUU YA WAFANYAKAZI DUNIANI( MEI MOSI)-KIKWETE AWASILI TANGA, KUWA MGENI RASMI.

RAIS KIKWETE AKIWASILI MKOANI TANGA KWA AJILI YA SIKUKUU ZA WAFANYAKAZI.



RAIS KIKWETE AKIPOKEWA NA MWENYEJI WAKE KATIBU WA SHIRIKISHO LA VYAMA VYA WAFANYAKAZI(TUCTA) NDUGU NICHOLAUS MGAYA.(Picha zote kwa hisani ya LUKAZA Blog)

HATIMA YA KUVUNJWA KWA BARAZA LA MAWAZIRI TANZANIA-MAWAZIRI WAGEUKA MABUBU.

Dar Es Salaam-Tanzania.


Siku chache baada ya kamati  kuu ya chama cha mapinduzi (CCM) kubariki kuchukuliwa hatua kwa mawaziri waliohusishwa na kashfa mbalimbali za kushindwa kuwajibika na matumizi mabaya ya mali za umma, mawaziri wanaoshinikizwa kujiuzulu wamegoma kutoa matamko yao huku wakisema kuwa hatima yao ipo mikononi mwa rais na wengine wakisema wao hawawajibiki kwa kamati hiyo ya chama.

Waziri wa fedha Mustafa Mkulo amenukuliwa na gazeti moja linalotoka kila siku akisema hana la kusema ingawa amedai pi hawajiki kwa kamati ya chama hicho ila serikali, huku mawaziri Maige, Omary Nundu, Nyalandu na George Mkuchika wao hawakuwa tayari kuongea kwa madai hawana la kusema.

Mawaziri hao wamekaa kimya bila kuonekana kama wanania ya kujiuzulu licha ya mashinikizo yote hayo huku wakisisitiza kuwa wao ni watu safi wasio na tuhuma.

CHARLES TAILOR ANAHATIA-MAHAKAMA.


Mahakama ya kimataifa ya makosa ya Jinai iliyoundwa maalum na umoja wa matifa kwa ajili ya kushughulikia makosa ya uhalifu wa kivita kwa kuwapa silaha waasi wa Sierra Leone kwa malipo ya almasi katika vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini humo rais wa zamani wa Liberia Charles Taylor  . Hii ni mara ya kwanza kwa mahakama hiyo maalum iliyoundwa na Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Sierra Leone kutoa hukumu hiyo.

Jaji Richard Lussick aliyekuwa akisimamia jopo la majaji alisema mahakamani "Mahakama imemkuta na hatia ya kusaidia na kuchochea uhalifu wote huu," akiongeza kuwa Taylor atahukumia adhabu Mei 30.
Taylor, mwenye umri wa miaka 64, alikutwa na hatia ya kusaidia waasi wa Sierra Leone kuendesha kampeni ya uhalifu dhidi ya watu nchi hiyo wakati wa miaka 10 ya vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyouwa watu wapatao laki moja ya elfu 20.

Taylor alilipwa na waasi hao kwa madini ya alhamisi yaliyokuwa yakichimbwa kinyume cha sheria na waasi wa kundi la Revolutionary United Front (RUF) ambao walijulikana kwa mauaji, ubakaji na kukata watu mikono au miguu kwa mapanga.
Taylor alisafirishwa kutoka Freetown kwenda katika mahakama hiyo maalum nje kidogo ya the Hague mwaka 2006 katika kesi ambayo ilikuwa na mashahidi kama vile mwanamitindo wa kimataifa Naomi Campbell na mcheza sinema Mia Farrow kutoka Marekani.(VOA)

MANCHESTER CITY WAIBWAGA MAN U!- Waifunga 1-0.

Manchester, Uingereza, 

Manchester City wamejiweka katika nafasi nzuri ya kuchukua tangu mwaka 1968 baada ya hapo jana kuifunga Manchester United kwa goli moja kwa bila kupitia nahodha wao Vincent Kompany katika uwanja wao wa nyumbani wa Etihad. Katika mchezo huo Manchester City ndiyo walikuwa timu bora katika kiwango huku wakitumia kikosi kile kile walichokitumia katika mchezo wao kabla ya huo dhidi ya Wolves tofauti na wapinzani wao Manchester United waliojaza viungo watano katikati ambapo Park Ji-Sung aliongezwa akisaidiana na wakongwe wengine Paul Scholes na Ryan Giggs.
Manchester United waliouanza mchezo kwa kasi walijikuta wakigeuziwa kibao katika robo ya mchezo huo na wenyeji kuanza kutawala huku Carlos Tevez alifanikiwa kuipenya ngome ya Manchester United katika dakika ya 16 na kutoa krosi ambayo hata hivyo iliondolewa na Phil Jones.

Hatimaye katika dakika ya 46 ya nyongeza ya kipindi cha Kwanza Vicent Kompany alifanikiwa kuunganisha vizuri kona iliyopigwa kutoka upande wa kushoto wa Man United  kwa kichwa na kuipa goli la kuongoza na la ushindi timu yake hiyo.

Hata hivyo baadae mchezo huo ulitawaliwa na misuguano ya hapa na pale ambapo katika kipindi cha pili kocha wa manchester City  Roberto Mancini na mwenzake wa Manchester United Alex Ferguson nusura wakunjane  baada ya Mancini kulalamikia kadi ya njano aliyopewa mchezaji wake Nigel De Jong  ambapo Ferguson alimshambulia Mancini na kumuonesha ishara kuwa yeye ni mlalamishi sana na walipokaribiana walizuiwa na kila mmoja kurudishwa upande wake, ingawa mwisho wa mchezo makocha hao walishikana mikono.

Licha ya kupambana kufa na kupona katika dakika za majeruhi Manchester United hawakuweza kubadilisha matokeo hayo.Kwa ushindi huo Manchester City inashikilia usukani wa ligi hiyo ikiwa na pointi 83 baada ya michezo 36 sawa na wapinzani wao wa karibu Manchester United  wenye pointi 83 pia ingawa wanazidiwa magoli ya kufunga na kuizidi magoli ya kufungwa manchester City.