.Wanafunzi wa kidato cha pili katika shule ya sekondari ya Kambangwa iliyopo Kinondoni jijini Dar es Salaam,wakioneshwa na Meneja miradi na Mawasiliano wa Vodacom Foundation Renatus Rwehikiza moja ya progamu zinazopatikana katika Kompyuta zinazowawezesha kupata taarifa ya masomo mbalimbali kwa njia ya mtandao wakati alipotembelea shuleni hapo kwa ajili ya kujua maendeleo ya mradi wa TEHAMA uliofadhiliwa na Vodacom Foundation kwa kushirikiana na Kampuni ya Samsung.Zaidi ya wanafunzi elfu tano wa shule nne za sekondari jijini wanaendelea kunufaika na mradi huo.
Mwalimu Mkuu wa Shule ya sekondari ya Kambangwa iliyopo Kinondoni jijini Dar es Salaam Theresia Ng’wigulu (kulia) Meneja miradi na Mawasiliano wa Vodacom Foundation Renatus Rwehikiza(kushoto ) pamoja na Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania Matina Nkurlu (katikati)wakimsikiliza mmoja wa wanafunzi wa kidato cha pili katika shule ya sekondari ya Kambangwa,Matha Galus akiwaelezea jinsi anavyoweza kupata taarifa za masomo mbalimbali kwa njia ya mtandao, wakati walipotembelewa na maofisa wa Vodacom shuleni hapo kujua maendeleo ya mradi wa TEHAMA uliofadhiliwa na Vodacom Foundation kwa kushirikiana na Samsung.Zaidi ya wanafunzi elfu tano wa shule nne za sekondari jijini wanaendelea kunufaika na mradi huo.
Mwalimu Mkuu wa Shule ya sekondari ya Kambangwa iliyopo Kinondoni jijini Dar es Salaam Theresia Ng’wigulu (kulia) Meneja miradi na Mawasiliano wa Vodacom Foundation Renatus Rwehikiza(kushoto ) pamoja na Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania Matina Nkurlu (katikati)wakimsikiliza mmoja wa wanafunzi wa kidato cha pili katika shule ya sekondari ya Kambangwa,Matha Galus akiwaelezea jinsi anavyoweza kupata taarifa za masomo mbalimbali kwa njia ya mtandao, wakati walipotembelewa na maofisa wa Vodacom shuleni hapo kujua maendeleo ya mradi wa TEHAMA uliofadhiliwa na Vodacom Foundation kwa kushirikiana na Samsung.Zaidi ya wanafunzi elfu tano wa shule nne za sekondari jijini wanaendelea kunufaika na mradi huo.
Baadhi ya Wanafunzi wa kidato cha pili katika shule ya sekondari ya Kambangwa iliyopo Kinondoni jijini Dar es Salaam na Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Theresia Ng’wigulu watatu toka kulia pamoja na maofisa wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu wa kwanza kushoto na Renatus Rwehikiza(kulia)wakimsikiliza Mwalimu wa somo la kompyuta wa kidato cha pili Nicolas Wilson wa shule hiyo akiwafafanulia jambo kuhusiana na elimu ya mafunzo ya kompyuta wakati walipotembelewa na maofisa hao kujua maendeleo ya mradi wa TEHAMA uliofadhiliwa na Vodacom Foundation kwa kushirikiana na Kampuni ya Samsung.Zaidi ya wanafunzi elfu tano wa shule nne za sekondari jijini wanaendelea kunufaika na mradi huo.
Wanafunzi wa kidato cha pili wakiwa darasani katika shule ya sekondari ya Kambangwa iliyopo Kinondoni jijini Dar es Salaam,wakiwa na nyuso za furaha walipotembelwa na Maofisa toka Vodacom Foundation kwaajili ya kujionea maendeleo ya mradi wa TEHAMA uliofadhiliwa na Vodacom Foundation kwa kushirikiana na Kampuni ya Samsung.Zaidi ya wanafunzi elfu tano wa shule nne za sekondari jijini wanaendelea kunufaika na mradi huo.
------------------
Wanafunzi waendelea kunufaika na mradi wa elimu ya kompyuta wa Vodacom na Samsung
“Tumekuwa tukijifunza somo la kompyuta kwa nadharia kabla ya mradi wa Samsung Smart kuanzishwa hapa shuleni kwetu,baada ya kuanzishwa hivi sasa tunasoma somo la kompyuta kwa vitendo na ndoto yetu ya kuingia katika ulimwegu wa sayansi na teknolojia imetimia”Anasema John Mwasha mwanafunzi wa shule ya sekondari ya Kambangwa iliyopo wilayani Kinondoni mkoani Dar es Salaam akiwakilisha wenzake.
Mwanafunzi mwingine kutoka shule hiyo Mariam Abdallah amesema kuwa ipo idadi ya wanafunzi wengi mijini na vijijini wanamaliza elimu ya sekondari bila kujua matumizi ya kompyuta kiasi kwamba kifaa hiki wanakiona kama ni kigumu sana kukitumia, na kuongeza kuwa mradi huu ni muhimu katika shule za Tanzania na umeweza kuwaingiza katika ulimwengu wa teknolojia ya kompyuta.
Mradi huu ambao umeanzishwa kwa ushirikiano wa Vodacom na Samsung umeanzia katika shule nne za mkoa wa Dar es Salaam ambapo shule hizo zimepatiwa msaada wa kompyuta za kufundishi wanafunzi,kujengewa darasa la kusomea somo hilo pia kupatiwa jenereta inayomia teknolojia ya mionzi ya jua kwa ajili ya kutoa nishati ya umeme kwenye shule hizo.
Mwalimu Mkuu wa sekondari ya Kambangwa,Bi.Theresia Mwigulu, amesema mradi huu ni muhimu na umewawezesha wanafunzi katika shule yake kuingia katika ulimwengu wa kompyuta na hivi sasa wanaweza kumudu vizuri somo hilo kwa kuwa wanalisoma kwa nadharia na vitendo.
“Baada ya kupata mradi huu,somo la kompyuta imekuwa ni rahisi kulifundisha kwa nadharia na vitendo pia walimu na wanafunzi wamekuwa wakipata taarifa na maarifa ya kufundishi masomo kutoka katika mtandao wa internet.Huu mradi unaweza kuleta mabadiliko makubwa kielimu ukisambaa katika shule zote nchini”Amesema Mwigulu.
Kwa upande wake Meneja wa Mradi na Mawasiliano wa Vodacom Foundation Renatus Rwehikiza amesema kuwa amepata faraja baada ya kutembelea shule hiyo na kukuta wanafunzi wanaendelea kunufaika kwa kupata maarifa ya kutumia kompyuta na kupata habari na elimu kutoka sehemu mbalimbali duniani kupitia mtandao wa internet.
“Mawasiliano mazuri huwezesha watu kupata taarifa mbalimbali zinazotokea katika mazingira yao walipo na sehemu za mbali kwa urahisi.Kwa wanafunzi kompyuta zinasaidia sana kupata maarifa kupitia mtandao wa internet.Nawahasa msome kwa bidii na mtumie vizuri fursa hii kutafuta elimu na msiogope kusoma masomo ya sayansi maana mambo yote hivi sasa yamerahisishwa kupitia teknolojia hii ya kompyuta”.Alisema.
Mradi huu ulizinduliwa rasmi mwaka 2013 Kati ya ushirikiano wa kampuni ya Samsung na Vodacom Foundation na shule zingine za sekondari zitakazonufaika na mradi huu ni Kinyerezi,Makumbusho na Mtakuja beach.